Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Una poit mzeya. Yani ni upuuzi kuamini et Ukwa wangeweza kuitoa CCM madarakani wakati tume ya UChaguz ni branch ya CCM. Jeshi la police ni vibaraka wa CCM. Katiba nayo mbovu. Yani upinzani wasipotaka Reform katika Tume ya uchaguz na katiba. Ikuru wataisikilizia kwa jiran.
Hakuna Tume huru ya Uchaguzi Duniani labda iundwe na malaika period!
 
Bado sijaona chochote kilichofanyika awamu hii kumsaidia mtanzania wa hali ya chini badala yake msosi umetoka kwenye mara 3 kwa siku mpaka mara 1 kwa siku.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Sio Magufuli au serikali itakayo kuletea maendeleo, ni wewe ndio utakayeleta maendeleo. Magufuli anakufagilia njia, ana ondoa uwizi, ukandamizaji na usmbufu na amefungua milango kwa wawekezaji na hadi sasa kwa miezi minane kumesha kua na mikakati mikubwa kadhaa itakayo anzishwa.
Siko nchini kwa sasa lakini hivi karibuni nimeogea na jamaa zangu huko kila mmoja anakuambia sasa hivi kuna heshima kubwa huko maofisini na bado. Tukijali maslaha na tukaacha malumbano ya siasa tutakuja kupata maendeleo na hayo tunayaona wazi kabisa sasa.
. Tatizo la watanzania wanataka hayo maendeleo wayapate mara mmoja, wakilala usiku na kuamka asubuhi waone maendeleo lakini hawajiulizi wao walifanya juhudi gani ya kuleta maendeleo.
 
Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo tu.
Anakotupeleka hata njiani hakuna pa kununua chakula, na kuchimba dawa ni porini!
Tuombe tusitobozee kismayu
 
Magufuli atafanya yaliyoko kwenye ilani na atapimwa kwa ilani ya CCM iliyopendwa na wapiga kura wengi....waliokosa muelekeo ni wale walioahidi kwenda kuchunga ng'ombe mara wakaahidi kwenda ICC na mara waahidi kuzunguka nchi na blah blah kibao.

Wakati wa Uchaguzi tuliwaonya sana muache kuwa Nyumbu na wazungusha mikono na badala yake msikilize sera na kupima kama zinatekelezeka....

Kama mngesikiliza Ilani ya CCM kama ilivyonadiwa na Magufuli usingekuja kuuliza pumba hizi unazouliza leo hii...

Magufuli aliahidi kupambana na Rushwa(Ni mgombea pekee aliyeongelea rushwa kwa hisia na kweli)....Mwezi wa Saba Mahakama ya Mafisadi inaanza kazi

Magufuli aliahidi kushughulikia Tatizo la mikopo elimu ya juu....Wanafunzi wamepata mikopo,bodi imefumuliwa na mikopo imeanza kurejeshwa.

Magufuli aliahidi elimu bure...Imeshaanza pamoja na changamoto zake.

Magufuli aliahidi kukusanya kodi na kuondoa viushuru vya ajabu ajabu...Salamu za bandari za nchi kavu umezisikia na kama unafuatilia kuna viushuru vya kwenye kahawa vimeanza kuondolewa.

Magufuli aliahidi kupunguza msongamano Dar....Mabasi ya mwendo kasi yameanza ns hapa majuzi kitwanga anaongelea kuhusu flyover kuanza kujengwa...

Magufuli aliahidi kurejesha nidhamu kwa watumishi wasio waadilifu....unataka niongee??

Magufuli aliahidi kuwanyang'anya mashamba wale wasioendeleza ....unataka kuniambia hujamsikia lukuvi??

Hivi hujasikia kiwanda cha tiles kilichoanza kujengwa Mkuranga ?hivi hujamsikia rais akiwaasa NSSF PPF kujenga viwanda badala ya maghorofa yasio na tija??

Pale Muhimbili CT SCAN ilikuwa ni kipimo adimu sana kukipata nadhani unaweza kuona nini kinaendelea Baada ya Rais kuzuru Muhimbili consistently (Changamoto ya dawa na vifaa tiba kuwepo kwenye vituo pamoja na ujenzi wa zahanati)....universal coverage ya bima ya afya ni sheria inayonukia mwezi septemba.

kuhusu maslahi ya wafanyakazi PAYE imeanza kufikia single digit as per july this year.

Kuhusu kuulinda muungano...Rais ametuvusha salama salmini bila tone la damu kumwagika kule Zanzibar pamoja na hila zenu zilizokosa uzalendo na za kuwategemea mabwana wa kizungu.

Ndio maana narudia tena kuwaita Nyumbu au pengine ni fisi mnaofuata mzoga ulipo maana hamjielewi mshike kipi.....

Matatizo yenu ya kupokea makapi na mizoga muyamalize huko huko msituletee shombo sisi wastaarabu!!!


MAGUFULI AMEFANYA ZAIDI KABLA YA MUDA WAKE KUANZA!!

Ndugu tatizo la baadhi ya watanzania hasa wanao shangilia siasa kama washabiki wa mpira ndio wasio ona hayo yote. Wao wanachotaka wapate maendeleo na waone kila kitu kine tekelezwa kwa siku mmoja. Na wengine ndio hao wanao omba serikali ishindwe ili wapate la kusema.
 
Naomba tmakuful



Naomba makufuli arudishe utawala wa kijerumani ukiokota sanduku la pesa upeleke polic
 
Ukipenda kupigiwa makofi na kushangiliwa,ni lazima kwanza uahidi makubwa kama vile kujenga mwezini au chini ya habari,ujaribu kufanya mambo makubwa kama vile kuhamisha bahari, n.k.

Hata hivyo,ukwel ni kwamba,ahadi za aina hiyo ni ngumu kuzitekeleza na hata ukijaribu kuzitekeleza utaishi kujaribu tu na kuharibu na mwisho wa siku mikono hiyo hiyo iliyotumika kukupigia makofi, ndio hiyo hiyo itakayotumika kukuzaba makofi kwa kushindwa kutimiza ahadi zako.

Hili ndio somo letu la leo na mwalimu wako Salary.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom