Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kama mpaka leo baadhi ya watu mmeshindwa kusoma tabia ya huyu bwana mkubwa,basi ni wazi upeo wenu ni mdogo mno.

Eleweni tu mtu huyu ana sifa kuu hizi;

1.Si mkweli
2.Anaongea asichomanisha
3.Anamanisha asichongea
4.Msanii/muigizaji
5.Hana aibu
6.Mtu wa fitina.

Endeleni kumuamini wale mliochagua kumuamini/kujifanya vipofu na viziwi.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa
 
Kutokana na wapinzani kuhamasisha Wananchi wasijiandikishe kwenye daftari la wapiga kura

Hali ni Mbaya huko mtaani Wananchi wanawakimbia sasa

Wengi wanasema bora tujichagulie Mzalendo Magufuli tu
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa
Hati chafu ipo CCM hata wakurugenzi wote wa wilaya wenye hati chafu ni wanachama wa CCM
 
Tumechoka siasa za uwongo za upinzani,

Walisema Nchi isiyomiliki usafiri wa anga ni sawa na Nchi iliyokufa kiuchumi leo wanasema Ndege za kazi gani!

Tuwakatae hawa matapeli wa siasa
 
Kutokana na wapinzani kuhamasisha Wananchi wasijiandikishe kwenye daftari la wapiga kura

Hali ni Mbaya huko mtaani Wananchi wanawakimbia sasa

Wengi wanasema bora tujichagulie Mzalendo Magufuli tu
Mzalendo wa nini? Mzalendo kuondoa CAG olijino kuweka CAG feki ndiyo uzalendo?
 
Tumechoka siasa za uwongo za upinzani,

Walisema Nchi isiyomiliki usafiri wa anga ni sawa na Nchi iliyokufa kiuchumi leo wanasema Ndege za kazi gani!

Tuwakatae hawa matapeli wa siasa
Acha kuwasema wengine umechoka na nani? Ujinga wako binafsi usilazimishe kuwa ujinga wa wengi, kununua ndege kifisadi siyo sera ya upinzani utapeli upo CCM anza kuwakataa huko huko kwanza.
 
1
Mimi nadhani Raisi Magufuli anatupeleka kwenye utawla wa KIIMLA ,maamuzi yote ya nchi yanafanywa na mtu moja,au mtu yeyote atakayefanya afanye kama apendavyo Raisi hata kama anakosea.Ndo maana utaona wakuu wa wilaya,Mikoa na hata Makamishna wa polisi,wana fanya kazi kama mkuu wao anavyofanya,kutumbua bila ya kuchunguza kwa kina chanzo cha kasoro zilizopo.
2
Nadhani kisiasa anauwa mfumo wa vyama vingi kimtindo ili uwepo wake usiwe na athari yoyote dhidi ya utawala wake.
3
Kuna uwezekano wa kutekeleza uwepo wa serikali moja,kwani akifanikiwa kulimiliki bunge 100% bila ya mpinzani,na Hao CCM wenyewe watakuwa ni wale tuu waliokubali matakwa yake kabla ya kuteuliwa kugombea,hapo ataianza kazi ya kuifuta serikali ya zanzibar kwa kuondoa kifungu fulani ndani ya katiba ya jamuhuri.Nia ikiwa ni kuimarisha Muungano atafuta vifungu :-(Katiba ya jamuhuri nyongeza ya pili orodha ya ii , kifungu No 5,6,7 na 8 ).Vifungu hivi huondolewa kwa 2/3 ya kila upande wa muungano kukubali ndo vitatolewa.Wale wote upande wa Zanzibar wanaoonekana kuwa kikwazo hawatopitishwa kamwe kwenye kura za maoni,ili atimize ndoto yake.
4
Akifanikiwa kuiondosha Serikali ya zanzibar 'automatically' serikali itakuwa moja tu ya jamuhuri na atamtafutia nafasi fulani raisi wa Zanzibar ili apate mlo hadi amalize muda wake.
AKIFANIKIWA HILO ATAPEWA SIFA KWA KUMALIZIA MFUPA ALOUACHA FISI BILA YA MIKIKI.
Baada ya hapo Tanzania itakuwa na Mfumo kama china,chama kimoja,Maendeleo kwa kasi,Ujamaa mbele kwa mbele.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Umedandia gari naona, shuka tu sisi tunaendelea na safari.
 
Mimi naipongeza serikali yangu ya awamu ya tano kwa maendeleo makubwa tuliyoyapata na hata sasa maisha yetu ni mazuri sana bigup my presida
 
Kwa MTU asiyeona mabadiliko makubwa kiuchumi,kijamii na kusiasa katika awamu ya tano huyo atakuwa na upungufu wa akili hongera sana raisi wangu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom