1
Mimi nadhani Raisi Magufuli anatupeleka kwenye utawla wa KIIMLA ,maamuzi yote ya nchi yanafanywa na mtu moja,au mtu yeyote atakayefanya afanye kama apendavyo Raisi hata kama anakosea.Ndo maana utaona wakuu wa wilaya,Mikoa na hata Makamishna wa polisi,wana fanya kazi kama mkuu wao anavyofanya,kutumbua bila ya kuchunguza kwa kina chanzo cha kasoro zilizopo.
2
Nadhani kisiasa anauwa mfumo wa vyama vingi kimtindo ili uwepo wake usiwe na athari yoyote dhidi ya utawala wake.
3
Kuna uwezekano wa kutekeleza uwepo wa serikali moja,kwani akifanikiwa kulimiliki bunge 100% bila ya mpinzani,na Hao CCM wenyewe watakuwa ni wale tuu waliokubali matakwa yake kabla ya kuteuliwa kugombea,hapo ataianza kazi ya kuifuta serikali ya zanzibar kwa kuondoa kifungu fulani ndani ya katiba ya jamuhuri.Nia ikiwa ni kuimarisha Muungano atafuta vifungu :-(Katiba ya jamuhuri nyongeza ya pili orodha ya ii , kifungu No 5,6,7 na 8 ).Vifungu hivi huondolewa kwa 2/3 ya kila upande wa muungano kukubali ndo vitatolewa.Wale wote upande wa Zanzibar wanaoonekana kuwa kikwazo hawatopitishwa kamwe kwenye kura za maoni,ili atimize ndoto yake.
4
Akifanikiwa kuiondosha Serikali ya zanzibar 'automatically' serikali itakuwa moja tu ya jamuhuri na atamtafutia nafasi fulani raisi wa Zanzibar ili apate mlo hadi amalize muda wake.
AKIFANIKIWA HILO ATAPEWA SIFA KWA KUMALIZIA MFUPA ALOUACHA FISI BILA YA MIKIKI.
Baada ya hapo Tanzania itakuwa na Mfumo kama china,chama kimoja,Maendeleo kwa kasi,Ujamaa mbele kwa mbele.