Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Sio kweli Magufuli hajatugawanya
Tumwache Rais afanye kazi
Mbaya zaidi, anataka kuligeuza Taifa hili kuwa la wanaccm pekee.......

Ukiwa mpinzani Tanzania unahesabika kuwa siyo mzalendo, msaliti na mhaini ndani ya nchi yako!
 
Sio kweli Magufuli hajatugawanya
Tumwache Rais afanye kazi

Ukiona waziri anapata ajali watu wanashangilia, ukiona ndege inakamatwa watu wanashangilia, ukiona kuna tetesi za mkulu kufa watu wanaadaa mvinyo wakisubiri confirmation ujue watu wamegawanyika na taifa siyo moja.

Chanzo cha haya kwa mujibu wa science ya jamii na development studies ni kundi moja kulinyanyasa kundi jingine kwa muda mrefu. Sasa kama na hizo dalili huelewi basi tutakuacha ulivyo.
 

Yaani wanazingua sana na wanataka kiwe chama kimoja kitawale hali ya kuwa wananchi hawatakuwa na uhuru wa kuchagua mtu wanae mtaka bado tupo kwenye ukoloni hakika
 
Muelekeo wa kimaendeleo anajitahidi ila anaharibu pale anapowahesabu wapinzani kama ni maaduwi zake.
 
Bunge tu halina ushawishi ata wa kulifuatilia kiukweli anapotupeleka anajua yeye maana ata wanachama wenzie hawamuelewi anakowapeleka wameamua kuzingatia kaz zao wasitumbuliwe
 
Muelekeo wa kimaendeleo anajitahidi ila anaharibu pale anapowahesabu wapinzani kama ni maaduwi zake.
ccm yenyewe hawaelewani,wanamlamba kisogo ili afeli.
Na yeye kashika kasi kwa kusifiwa .Soon or later time will tell
 
Matendo ya serikali ya Magufuli ya kufuta haki za msingi za raia za kuchagua na kuchaguliwa yameipa Tanzania doa lisilofutika milele.

Matendo haya ni mwanzo wa kuingiza nchi kwenye machafuko ya lazima kwa tamaa za umwagaji damu alizonazo mwenyekiti wao anayejiita jiwe.

Ni lazima watanzania tushikamane kuukataa huu uhuni. Ni lazima tuwaeleze wazi viongozi wote waliosimikwa kidikteta kuwa hatukuwachagua sisi.

Wakitaka waende mtaa wa Lumumba wakaongoze ofisi iliyowachagua.

Nawasilisha.
 
Ni kweli kabisa. Kuna wengi hawaoni athari ya matendo ya watawala. Tanzania imekuwa taifa la kuzungumzwa kwenye vikao vya COMEDY. Kiongozi mkuu amekuwa kichekesho duniani. Kuna scandal ya ndege kuzuiwa. Hamna njia ya kujitoa ila kulipa deni la watu. Kuna kesi ya Zanzibar korti ya afrika mashariki ambayo hadi sasa serikali imeshindwa kuitetea na wanatumia kila njama kuhakikisha walioshitaki na mawakili wao hawafiki kortini kwa njia moja au nyengine na hawajui athari yake. Kuna maiti zinazookotwa kwenye maziwa huko na kuna wengi waliopotezwa ki aina. Bado kuna wanaosota magerezani bila mashtaka. Yooote haya yapo documented na itafika wakati muafaka kujibiwa na watawala.Watanzania wamaechoka. Huyo raisi akienda kwa ziara anaona anashangiliwa lakini kiukweli hasa , wana mramba kichogo. Yeye anafikiri anapendwa kumbe watu wanamuona kinyago cha mparure.
 
Authoritarianism
  • In authoritarian governments, the people have no power or representation and it is characterized by absolute or blind obedience to formal authority, as against individual freedom and related to the expectation of unquestioning obedience. The elite leaders handle all economic, military, and foreign relations. A prime example of authoritarianism is a dictatorship.
  • Totalitarianism is the most extreme form of authoritarianism because it controls all aspects of life including the communication between citizens, media censorship, and threatens by the means of terror.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…