My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,306
Hatimaye kumekucha tena, hili tulilitarajia siku nyingi, tangu aingie madarakani Magufuli ameigeuza Tanzania Kama Kampuni yake binafsi huku akiwa na ndoto za kutaka kuabudiwa na kila raia.
Tunatambua wazi kuwa yeye ni Rais wa nchi na anastahili kuheshimiwa kwa mamlaka aliyonayo lakini mamlaka yake yana mipaka kwa mujibu wa Katiba aliyoapa kuilinda.
Haruhusiwi kutoa uhai wowote ule isipokuwa kuidhinisha hukumu ya mahakama kuu.
Amekuwa mtu wa chuki tu na mataifa ya magharibi bila sababu yoyote ile.
Aliingia madarakani na kuikuta Tanzania ikiwa na mahusiano mazuri tu na mataifa makubwa Duniani, kwa makusudi kabisa bila sababu za msingi amekuwa akifanya jitihada za kuibomoa nchi kwa nguvu zake zote.
Ni mara kibao anasema hadharani kauli za chuki dhidi ya mataifa makubwa na wananchi wake, kauli Kama "nyie mlinichagua hamwezi kubomolewa nyumba "kauli hii aliwaambia wananchi wa Mwanza na ushahidi upo YouTube.
"Nimekupa gari, nimekupa nyumba,nakulipa mshahara halafu unamtangaza mpinzani kashinda ".
Kauli hii aliwaambia wakurugenzi kuwatisha. Rais Magufuli ni mtu asiyeamini ktk ushindani wa haki bali mabavu, waandishi wamepotea, wakosoaji wamepotea halafu anadai tusiinyoshee kidole serikali eti hao waliopotea wapo kwa wapenzi wao.
Watu karibia 350 walipotea kibiti wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola, Azory Gwanda alipotaka kuandika Habari za watu hao naye akatekwa na kupotezwa.
Wahalifu wote hufikishwa mahakamani na siyo kuwaua, kuwaua ni uhalifu tena mwingine. Mataifa makubwa yanapolalamika juu ya ukandamizaji wa haki za Binadamu, eti wanajibiwa kwa kuambiwa ni mabeberu, kwa hiyo nyie muuwe watu hovyo kisa ni nchi huru?
Mna Uhuru gani wakati kila mwaka mnakinga bakuli la uombaomba?
Eti nyie ni matajiri, mna utajiri gani nyie? sasa vikwazo hivyo vinakuja mpambane navyo. Taifa haliwezi kuendeshwa kwa mawazo ya mtu mmoja utadhani yeye ni Mungu.
Yeye ndo Bunge, yeye ndo mahakama, yeye ndo Ikulu, ndo maana hakimu Simba anaboronga sheria ili kumridhisha na kumfurahisha Magufuli, which means anafanya kazi kwa shinikizo maalumu.
Mtakuja kustuka mjikute mpo Kama Zimbabwe. Eti wazungu wanawaonea wivu Tanzania, wawaonee wivu mna nini nyie maombaomba? na nchi yenu imechoka, imechakaa na kupauka kwa dhiki.
Haki huinua taifa, mnatenda dhuluma huku mkijifanya wacha Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app