Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Kwa kifupi rais Magufuli ndiye rais atufaaye watanzania kwa hali ambayo tulikuwa tumefukia, amekuja wakati sahihi naye amekuwa mtu sahihi. Hawatakosa kutokea ambao hawata muona sahihi ila wengi ni wale wasio amini mabadiliko huweza kuletwa na mmoja miongoni mwa wengi ambao hawakuweza kuleta mabadiliko haya tusiyo yakubali.
Viva Magufuli. 2020 -
 
mabadiliko gani hayo aliyoleta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna tatizo linaitwa Magufuli hata tufanye juhudi gani hatuwezi kwenda kupata katiba, tume huru, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mtanzania wa chama chochote kufanya siasa sehemu yeyote nchini.

Kila mnachokiwaza yeye anawaza kinyume chake lazima tufike sehemu tukubaliane tumwambie hakuna maendeleo yanayokuja kwa chuki visasi na siasa chafu hakuna.

Kwa umoja na mshikamano tuliojengewa na baba wa taifa sidhani kama tulitakiwa kuwa na rais wa design hii hata kwa muda wa mwezi alitakiwa kuwa ameshafulushwa Ikulu.

Rais anawaza kuwanunua wapinzani wake kisiasa ili tu waunge mkono mambo ya kihuni ya utekaji na mauaji kibaya zaidi pesa za walipa kodi ndio zinatumika upuuzi mtupu.
 
Tuna tatizo linaitwa Magufuli hata tufanye juhudi gani hatuwezi kwenda kupata katiba, tume huru, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mtanzania wa chama chochote kufanya siasa sehemu yeyote nchini.

Ww umeweka ukweli hadharani. Mimi nasema huenda kuna miaka mingine mitano ya siasa chafu hapa nchini. Na muhusika wa siasa chafu yuko wazi peupe
 
Zanzibar walichakionja kikombe cha utawala wa kidikteta wa Salmin Amour kwa kipindi cha miaka 10, na sasa ni zamu ya watu wa Bara kukionja kikombe hicho. Na kuanzia hapa mchakato wa kumpata kiongozi wa nchi utakuwa ukifanywa kwa umakini mkubwa. Usiyempenda uko naye mpaka 2025, labda mabadiliko yapitie ktk mpango mbadala wa Mola mwenyewe, na wala si vinginevyo.

Umeandika mambo mazito sana wewe jamaa.
 
Dikteka mliwa 0719 ...alioa mke geresha ..yule mama sasa hivi anadanga tu
 
FB_IMG_1583146215208.jpg
 
Nakumbuka maneno ya RIP KOLIMBA " NCHI IMEPOTEZA DIRA NA MWELEKEO" BAADA ya kuhojiwa juu ya kauli yake hiyo, kilichofuata kwake ni kuwa MAREHEMU.
 
Dereva ilitakiwa apewe mkokoteni Na sio semi hawezi panda mlima.Kuendesha GARI ni akili sio nguvu
 
Wananchi kwa umoja wetu tunaishi na viongozi wa taifa Kama c majirani zetu ni ndugu au maswahiba!

Hebu tuwaulize hao watu kwa upole na unyenyekevu Nini ambacho tumewakosea!

Swali hili liwe la mwisho katika mioyo yetu kabla ya kuchukua hatua binafsi.

Wengi tutaenda kushtaki kwa mizimu. Ila Kuna watakao kuwa majaji wenyewe kuamua hatma Yao kwa mikono yao.

Sijataja nchi yoyote hivyo sitegemei Uzi kufutwa au kupigwa ban labda muovu mzandiki katili na dikteta awaye yote ajishtukie.

Wasalaam. .....!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom