Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Yeye anapenda kuonekana mkombozi wa mwisho.
 
Umakini wa rais wetu mpendwa ktk nyanja zote umenifanya kuhitimisha kuwa siyo rais wa kawaida, ni rais wa ajabu sana! i Marais wa aina yake hawatokeagi mara kwa mara duniani!

Huyu rais ktk oparesheni alizofanya kutembelea sehemu tofauti nchini kote aliibua madudu na kuyatolea utatuzi na kuwaacha wataalamu husika midomo wazi!

Kama yale yote hayatoshi, kila alipoibuka kutolea ufafanuzi na kutoa dira ya taifa amekua akija na mambo yanayowafanya wataalamu husika kujitathmini! Ktk secta ya afya, huyu mkuu wetu kwa uvumilivu sana aliwaacha wabwabwajaji waendelee kufanya yao wakati yy rais akifuatilia kwa karibu kwa kutumia vyombo vyake na alivyotokeza leo, mmesikia wenyewe...amewaziba midomo wabwabwajaji akina Mbowe na kundi lake ambao wameonekana majuha!

Huyu rais tulie naye siyo wa kupambana naye kwa akili ndogo...huyu ni mtumishi wa Mungu Aliyehai, tumwache aendeshe nchi ktk direction inayofaa! Vivi vijimikingamo vya uongo na kweli vya akili ndogo za kina Mbowe na washirika wake kamwe siyo level ya huyu rais wetu!

Mungu azidi kumbariki rais wetu na serikali ya awamu ya tano! Mungu azidi ibariki Tz!
Povu ruksa
 
Yeye kajificha kijijini kwake alafu anahimiza waTZ wajichanganye changanye ili yeye na genge lake wakusanye kodi, hapana hii siyo sawa kwa wakati huu...
 
Jpm ni very very unique, watanzania tutembee kifua mbele ,we have the best president ever,hata informers wake vizuri sana Mungu mbariki JPM bariki na serikali yetu kwa ujumla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningejinyonga kama ningewaza kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati Corona imeingia Brazil raisi wao alikuwa na tambo kama za Jpm kuwa tutakufa siku moja tusitishwe, Brazil mambo yamekuwa magumu Raisi kawageuka anasema sasa yeye afanye nini

Ugonjwa ulivyoingia Dar Makonda alitoka akipaza sauti watu waache uwoga wapige kazi ugonjwa wenyewe kama mafua, lakini wakati akihojiwa na Clouds akasema watu wanapukutika, na sasa yupo kimya kama sio yeye

Russia Raisi wao Vladmir Puttin naye mwanzoni alisema Kwao Corona si ishu pamoja na lockdown ndani wa siku tatu tu russia ina wagonjwa wapya 14,000 hapo watu wapo ndani, na wana wagonjwa 140,000 kwa nchi nzima, Now Puttin kageuka anasema Watu wawe makini nchi ipo kwenye janga

Ndio hivyo hivyo kwa Raisi wetu ameshaleta mzaha mapema kwenye issue serious kama hii, Tena baada ya kuwasikiliza wataalam yeye anapambana nao ona hatari hiii, hapa tutegemee Bomu ambalo litalipuka or limeshaanza kulipuka, Watu wataambukizana kwa kasi ya 5G

Kosa alilolifanya ni kuwadharau wataalam wa Afya mwishowe watakata tamaa na wataona liwalo na liwe watakaa pembeni now ukienda kupima hata ukikutwa na Covid utaambiwa una UTI ili wamfurahishe mkubwa maana hataki kusikia idadi kubwa mwishowe utarudi nyumbani na kuambukiza wengine

Ishu ni kuwa JPM hataki kusikia habari za maambukizi kuongezeka wakati hakuchukua hatu zozote za kujilinda mapema, mambo yashaharibika now hata wataalam wake hawaamini, anaona wanadanganya, sasa anaingilia kazi yao

Kajifungia mkoani hata misibani haendi kwa uwoga lakini anawapa moyo watu waache uwoga, Sasa anaangalia zaidi mapato kuliko afya za walipa kodi, Miradi aliyoingia ni mikubwa so ni lazima aje na sound kupumbaza watu ili pesa itafutwe na ndio maana anapambana na ukweli na hataki taarifa za kweli zitolewe akiogopa makusanyo kushuka

Akili yake yote ipo kwenye makusanyo lakini mwisho wa siku hata hayo makusanyo hatayapata kama corona ikishika kasi, ni swala la muda tu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…