Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
Hata wakati wa kumuapisha nchemba kamuweka mbali kabisa.Mods naomba muuache huu uzi
Wakati Corona imeingia Brazil raisi wao alikuwa na tambo kama za Jpm kuwa tutakufa siku moja tusitishwe, Brazil mambo yamekuwa magumu Raisi kawageuka anasema sasa yeye afanye nini
Ugonjwa ulivyoingia Dar Makonda alitoka akipaza sauti watu waache uwoga wapige kazi ugonjwa wenyewe kama mafua, lakini wakati akihojiwa na Clouds akasema watu wanapukutika, na sasa yupo kimya kama sio yeye
Russia Raisi wao Vladmir Puttin naye mwanzoni alisema Kwao Corona si ishu pamoja na lockdown ndani wa siku tatu tu russia ina wagonjwa wapya 14,000 hapo watu wapo ndani, na wana wagonjwa 140,000 kwa nchi nzima, Now Puttin kageuka anasema Watu wawe makini nchi ipo kwenye janga
Ndio hivyo hivyo kwa Raisi wetu ameshaleta mzaha mapema kwenye issue serious kama hii, Tena baada ya kuwasikiliza wataalam yeye anapambana nao ona hatari hiii, hapa tutegemee Bomu ambalo litalipuka or limeshaanza kulipuka, Watu wataambukizana kwa kasi ya 5G
Kosa alilolifanya ni kuwadharau wataalam wa Afya mwishowe watakata tamaa na wataona liwalo na liwe watakaa pembeni now ukienda kupima hata ukikutwa na Covid utaambiwa una UTI ili wamfurahishe mkubwa maana hataki kusikia idadi kubwa mwishowe utarudi nyumbani na kuambukiza wengine
Ishu ni kuwa JPM hataki kusikia habari za maambukizi kuongezeka wakati hakuchukua hatu zozote za kujilinda mapema, mambo yashaharibika now hata wataalam wake hawaamini, anaona wanadanganya, sasa anaingilia kazi yao
Kajifungia mkoani hata misibani haendi kwa uwoga lakini anawapa moyo watu waache uwoga, Sasa anaangalia zaidi mapato kuliko afya za walipa kodi, Miradi aliyoingia ni mikubwa so ni lazima aje na sound kupumbaza watu ili pesa itafutwe na ndio maana anapambana na ukweli na hataki taarifa za kweli zitolewe akiogopa makusanyo kushuka
Akili yake yote ipo kwenye makusanyo lakini mwisho wa siku hata hayo makusanyo hatayapata kama corona ikishika kasi, ni swala la muda tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila jamaa anakohoa kohoa ..