Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Wewe ndio kabisa huelewi concept ya COVID-19 na namna inavyoambukizwa...
Mkuu hii kitu hata kama utajifungia ndani for 100% lakn bado kutakuwa na uwezekano wa kuipata ikiwa majority ni +, ebu fikilia upo home kwako unavuta hewa safi kumbe kuna kiswampa njia kapita karibu na home kwako kakohoa ama kapiga chafya na huyu kiswampa njia ni +. Lakin hajijui na haonyeshi dalili zozote zile.

Kama ukifutilia huu ugonjwa hapa nchini ilianza mugonjwa alisafiri hivi karibuni kwenye inchi ambazo zinamaambuki, tukaja mgonjwa hana history ya kusafiri. Na sasa tutakuja mgonjwa hana history ya kutoka ndan kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jenerali Ulimwengu: Kinachoendelea serikalini ni "Andrew The Lawgiver", Tumerudi nyuma miaka 50 kwenye demokrasia

Jenerali Ulimwengu akiwa kwenye kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema pamoja na hatua nzuri anazochukua Rais wa sasa, Mheshimiwa John Magufuli ambazo zimepongezwa lakini ukiangalia picha kubwa ni kwamba tumerudi nyuma kama miaka 50 kwenye demokrasia. Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ulimwengu kasema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Kikwete. Ulimwengu ameendelea kwa kusema Mheshimiwa Kikwete anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka kwa kusababisha hasara kubwa kwa serikali na pili kuzima matumaini ya wananchi na kuwaacha wanarandaranda ambayo inaweza kuleta machafuko baadae kama haitawezekana kutengeneza katiba ambayo itajenga mustakabali wa wananchi wa Tanzania.
Source : JamiiForums / ITV Tanzania
 
Mwanasiasa ni mwanasayansi ni watu wawili tofauti. Sasa kwenye hili janga tutajua nani wa kuwasikiliza..
Yeye anadai kuwa ni mwanasayansi mahiri na pia mwanasiasa mkubwa hivyo hahitaji ushauri wa mtu.
 
Kila mwanadamu hajakamilika ila kwa asiyeona jitihada za rais wetu mh John Pombe Magufuli katika kujenga upya taifa hili huyo anajivika upofu kabisa
 
Ulitueleza mwenyewe kuwa umepewa tayari kishika UCHUMBA na MABEBERU ukiwa na akili zako timamu. Ukatuahidi wageni waalikwa tutapewa Noah siku ya harusi yenu.

Hata harusi haijafanyika umedandia Mapapai na Mafenesi. Mzee hebu tulia kwanza ktk hoja moja tuimalize kwanza halafu tuingie nyingine. Unatuchanganya sana wewe mzee ujue. Hii ni dalili ya kukosa Agenda ya kufanya ndio maana unaanzisha Vita visivyo na Mantiki.

Habari za Vita vyako na MABEBERU tumechoka kuvisikia wananzengo. Kwanza havina tija. Ni vita hewa ukilenga kuonewa huruma kwa kushindwa kwako kufanya majukumu ambayo ulipaswa kufanya. Hizo ni dalili za kushindwa kizungu tunaita Defensive mechanism.

Umeshindwa kuzuia corona watu wako wanakufa unasingizia MABEBERU. Majirani zako sasa wanazuia raia wako kuingia nchini mwao baada kuona kuwa Umeshindwa kuongoza taifa lako, najua utasema nao pia ni MABEBERU.

MABEBERU unao pigana nao ni akina nani? Wahanga ulio wanyang'anya misaada walio ichanga wasamalia kule Bukoba ktk janga la tetemeko ni MABEBERU wale?

Wananchi ulio wanyang'anya Korosho zao kule Lindi na Mtwala na kukusudia kuwatwanga hadi Shangazi zao ni MABEBERU wale?

Wafanyakazi wa Serikali usio wapandisha mishahara na vyeo kwa makusudi tuu miaka mitano sasa wakiishi kwa dhiki ndio MABEBERU hao?

Wananchi ulio wabomolea nyumba zao pale kibamba kisha ukaagiza kule Mwanza wasibomolewe kwa kuwa walikupigia kura ndio MABEBERU hao?

Wewe Mzee umekosa Agenda na hoja za msingi sasa umebakia kufanya vihoja. Unataka kuficha udhaifu wako kupitia MABEBERU hewa. Hiyo porojo yako ya Vita na MABEBERU pigana mwenyewe sie tunataka maendeleo sio porojo zako.

Maendeleo hayanaga vyama.
 
Yuko bize sana amekazana kutupeleka Jamhuri ya Watu wa Chato
 
Sijui kama niko sahihi kuiweka na CCM au abaki mwenyekiti peke yake mtasahihisha wenyewe

Japo wengi hatuzijui sheria ila hatukuzoea kuona waziri anaapishwa kwenye makazi binafsi ya mtu

Japo mambo hubadilika hatukuzoea kuona Spika anapewa kiburi na Rais

Japo dunia inaenda kasi hatukuzoea kuona Rais anatoa kauli za kuchanganya wakati wa majanga

Japo kila mtu na tabia zake ila hatukuzoea kuona mtu akihamia CCM au akiwa mwana ccm anakuwa huru kufanya analolitaka

Bungeni sheria hazifuatwi,

Mahakamani mashauri ili kuamliwa yanasikiliziwa kwanza,

Watumishi wa umma hawana tena uwezo wa kunyanyua mdomo kudai haki zao

Mapolisi wanaamrishwa kufanya chochote na wakubwa zao,

Wapinzani wanajiongelesha ongelesha tu ila hawana wanachoweza kufanya,

Vyama vya wafanyakazi vinajiongelesha tu havina la kufanya,

Mawaziri wanajiongelesha tu hawana la kufanya wala la kushauri wapo kama bendera tu,

Spika wa bunge na hata Jaji nao wameshakuwa bendera

Kama sio kutuona mazwazwa ni nini?

Hebu niambieni kundi gani sasa hivi hata likifanyiwa uonevu gani linauwezo wa kujipigania na likashinda.

Umenikumbusha Selasini na Komu wapo Nccr mageuzi lakini bungeni wanaiwakilisha Chadema!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom