Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Chagueni mbadala. Mbona simple ila mwisho wa siku wengi watashinda.
 
Wabunge zaidi ya 30+ na wanasiasa kutoka upinzani ambao tayari wana vyeo ndani ya vyama vyao zaidi ya 200+ kutoka chama pinzani na kuja Katika chama chetu kwa kweli ni jambo ambalo sijawahi kulisikia popote duniani.
 
Haya nenda kwa Dj ukachukue mshahara wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu niambieni kundi gani sasa hivi hata likifanyiwa uonevu gani linauwezo wa kujipigania na likashinda.
Mimi nasubiri tu nione maajabu ya nchi yangu ya Tanzania.

Kama Coronavirus haitakuwa kikwazo cha kuvuruga ratiba yetu ya uchaguzi mkuu, au kufanywa kuwa kisingizio cha kuahirisha uchaguzi huo.

Nasubiri kuona maajabu ya waTanzania wakijitokeza kwa wingi kwenda kuwachagua viongozi hawa hawa wa CCM. Hili litanishangaza sana.

Na sio kuwa sijui kwamba CCM wanazo njia zao mbalimbali za kutulazimisha wabaki kwenye madaraka hata kama hatukuwapigia kura. Kukubali kulazimishwa huko pia itakuwa ni sehemu ya maajabu ninayosubiri kuyaona.

Wengi tunasema hatuoni mbadala wa kuwapa madaraka, isipokuwa CCM tu ndio wanaostahili madaraka hayo.
Kama hivyo ndivyo, basi tuwasihi CCM wasilazimishe, watuache tu sisi wenyewe tuendelee kuwaweka kwenye madaraka hayo.

Kutunyima haki ya kufanya hivyo hilo ndilo kosa lisiloweza kusameheka; na hiyo ndiyo sababu inayofanya baadhi yetu tuone ni bora kuwaweka wapinzani kwa muda ili tuone kama watafaa kuwa mbadala. Wasipofaa, tuwaondoe kabla hawajachukua tabia mbaya za kutulazimisha wao wabaki kwenye madaraka kwa nguvu kama wanavyofanya CCM sasa hivi.
 
Wabunge zaidi ya 30+ na wanasiasa kutoka upinzani ambao tayari wana vyeo ndani ya vyama vyao zaidi ya 200+ kutoka chama pinzani na kuja Katika chama chetu kwa kweli ni jambo ambalo sijawahi kulisikia popote duniani.
Wamefata pesa sio itikadi
 
Unashauri tufanyeje.

Mitandao ya kijamii imetuharibu. Tunakimbilia kulalamika basi. No action taken. Zaman watu walikuwa wanafikisha message zao kwa maandamano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani wakuandamana! Kama vyombo vya habari vyenyewe vinachaguliwa cha kusema itakuwa maandamano.

Wala si kweli kwamba social media ndo zimezuia maandamano. Kilchozuia ni uzwazwa wa watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo mkoloni ni muoga Ila watawaliwa ni waoga zaidi.Uoga wao ndio kaburi lao
 
Hapa ndo tunapokwama na wao ndio wanapotuona hatuwezi kuwafanya chochote!

Kwamba watuache tupige kura kihalali, kura zihesabiwe kihalali, na mshindi atangazwe kihalali! Kuwaza hivi ndo kunatufelisha

Nchi nyingi zilizofanikiwa kubadili uongozi zilijipanga kwa kuweka plan B. Wabongo plan B yetu iko wapi?

Wanajua hatuna plan B ndiomaana wanafanya wanavyotaka wao wala sio sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…