Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Huyo baba ana gubu, ana chuki, ana kisirani, ana hinda, ana visasi na roho mbaya
Halafu Msajili wa Vyama vya Siasa haongei jambo kwa vile yameongelewa na CCM. Ingekuwa ni upinzani umeongea tayari angeshaita waandishi na kutoa maneno.

Angalia hata uchumba wa TLP, UDP na CCM hajaongea kitu. Upinzani umeongea kidogo tupeana nguvu tayari kimewaka, msajili keshatwanga maneno.

Hivi hawa wateule wamesomea wapi hadi kudhani Watanzania ni wajinga?
 
Je anavuruga au anapalilia vyama vingi ulitaka afanye nini kwenye siasa za ushindani humsemi vizuri mshindani wako. Hiyo hakuna.

Anatakiwa kusema amefaulu wapi katika miaka mitano maana wapinzani wanasema alipofeli tu. Anajisahau sana, mimi tangu alipo mtoa Prof Assad nikajua kabisaa hapa hakuna issue tena ni ujingaa tu. Tutaendelea nao mpaka basi
 
Anatambua uwepo na umuhimu wa vyama vingi japo kuwa watu wengi hatuutaki mfumo huo kwa kuwa wafuasi na viongozi wa vyama Vya upinzani kikiwemo chadema wanafikiri ugomvi na ubabe ndio upinzani wakati Siasa haitaki mabavu.

JPM aliposema tufanye kazi uchaguzi ulipoisha ndio Sawa, hata hizo Nchi zilizoendelea ndivyo zinavyofanya.

Baada ya uchaguzi wote mnaweka harakati pembeni na mnashirikiana kuleta maendeleo .

Sasa tujifunze kwanza Siasa halafu tufanyeni mifumo sahihi ya Siasa na baadae tutafute dola. Wapinzani bado hawajaiva.
 
Mwaka 2015 wakati awamu ya tano inaingia madarakani cement ilikua 11,500 kwa Dar ,Leo hii cement Ni tshs 15,000. Mikoa mingine 18,000 Hadi 20,000. Tumewakosea Nini watawala?

Nondo, bati, tiles nk vyote vimepanda mara dufu huku tuliambiwa tuna viwanda vya ndani, hivi viwanda vimekuja kutunyonya? Kama bidhaa ya cement ilizalishwa Mtwara tukanunua 11,500 Dar leo inakuwaje bidhaa hiyo hiyo izalishwe hapa Tanga tununue 17,000?

Awamu ya Tano mmetutesa kwa kutuziba mdogo, mmetunyonya.
 
Halafu wanakwambia wanaosema maisha magum ni wale waliokuwa wanachakachua vya umma.

Haya majamaa yataharibu sana hata bei ya bando kwenye simu ni mbaya
 
Nikisikia agenda za uchumi wakati najiuliza huo uchumi upo kwenye makaratasi au maisha na shughuli za kila siku. Anyway zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Ukweli ni kuwa hali maisha ya watanzia sio shwari.

Wengi kwa sasa wana msongo wa mawazo

Wengi wanaamka asubuhi hawana uhakika wa kula,wala kupata kipato.

Ukweli ni kuwa mkuu wa kaya amelitambua hili,na kama ingekuwa ni nchi kama Kenya alitakiwa apewe adhabu kwenye box la kura.

IMG_20201010_094212.jpg
 
MTU na kiongozi a nchi wametutesa site, na halo sio halo kimaisha. Kiongizi jeuri hata vyama vya wafanyakazi vilishindwa kufurukuta kutetea maslahi ya wafanya kazi wao.

Vitisho nabkejeri zilitawala, kiongozi alikanyaga katiba bila kujari kwamba cheo ni dhamana. Na alijua hii ni haki kikatiba kuaongezea mshahara watumishi na sio fadhira. Kwa maksudi CCM na wabunge wake na kiongozi waandamizi walikaa kimia na kutucheka sie watumishi wakati wao wanakula vizuri na maposho mengi tuu.

Hakuna hata mbunge au waziri mmoja alijitokeza hadharani kukemea huo uwonevu. Wote walikaa kimia! Leo wanaomba kura kwenda bungeni kufanya mini ma kumtetea nani? Wakati miaka mitano iliyopita waliungana na serekali kukandamiza watanzania.

Leo wanajitokeza watanzania kukitetea CCM na kiongozi wake kisa SGR, Ndege, Bwawa la Nyerere eti kafanya makubwa sana.
Mbona alikua waziri waujenzi Barbara zilikua zinajengwa na watu maisha yalikua nafuu sana tuu. Huwezi umiza watu halafu unakuja kuomba kura tens, ili iweje? Uendele kutunyanyasa?

Watanzania wanafiki na wenye yoga, wanawaunga mkono CCM. Ubungo inter-exchange inamsadia mini was Tandahimba, au Kigoma na hata Kagera? Tujiulize!

Unafiki wakujifanya mulifurahia sana awamu ya Huyu ndugu Rais na kumuombea kura tens, inanishangaza sana. Tufike mahali tuwe wakweli na sio kushabikia tuu.

Hata angekua kiongozi wa Chadema, CUF, NCCR or any polical party akafanya tuliofanyiwa for the last 5 years, ningesema hayahaya.
Wananchi wako kwanza, tenda haki kwa watu ako kama kiongozi. Usiwadhalilishe wananchi wako. Usiwe na jeuri sana na unawaongoza. Mwisho wasiku unakua dictator.

Unafiki wa watanzania na acheni uongo na semeni nyeusi no nyeusi na blue ni blue ja sio kujifanya hamuoni na wala hamsikii kilio cha wengi.

Inavyoonekana, akirudi ndugu raid, chamtema kuni tutakiona na tusije kujutia. Namuona anahasira sana, anaona watanzania hatuna fadhila.

28/10/2020, maamuzi ni yenu! Ika tusije laumiyana! God bless Tanzania, and may Peace Reign
 
Walianza na tamko usipotoa risiti au huombi risiti unatandikwa faini.

Wakaongeza kodi za kuagiza magari

Wakatoa tamko kwamba ukaguzi wa magari utakuwa unafanyikia Tz na sio huko japan, na ikiwa gari halijakizi vigezo basi inabidi uwalipe wakalitengeneze wao.

Huko JKT wamepiga stop watu kwenda

Walionufaika na mikopo chuoni, Taarifa zao za nida zinaunganishwa ma account za benki ili kuweka urahisi hata kama huna ajira inabidi ulipe marejesho

Hatujakaa sawa tunaona matrafki wanang'oa plate kwenye magari yaliyopaki yanayodaiwa.

Duhh
 
Nadhani Watanzania wengi walikuwa na matarajio makubwa sana Magufuli alipochaguliwa kuwa Rais, kwamba atazuia ufisadi, kusimia kuwajibika na maisha yatakuwa bora sana zaidi ya viongozi waliopita. Hata tukatangaziwa elimu bure na kujua ndio mwanzo wa neema za uraisi wa Magufuli.

Lakini sasa najiuliza sana, mbona maisha bado ni magumu sana na tuko mwaka wa sita wa Urais wa Magufuli? Hizo neema za Urais wa Magufuli tutafaidika nazo lini, mwaka wake wa mwisho wa uraisi? Maana kimsingi bado miaka kama minne tu Rais Magufuli aondoke.

Nadhani kila mtu atakubali katika hiii miaka sita ya Magufuli maisha ni magumu sana kuliko ilivyokuwa kipindi cha Kikwete kwa kila Mtanzania. Sasa ni nini hasa ambacho tunaweza kusema uraisi wa Magufuli umetufaidisha sana wanananchi? Flyovers, Dreamliners, SGR?

Hivi kama sisi watu wa mjini, tulioajiriwa, wafanya biashara nk, tulalalamika maisha ni magumu sana, huko vijijini hali yao ikoje? Hao wanyonge wanaotakiwa kufaidika kipindi cha uongozi wa Magufuli ni kina nani na watafaidika lini?

Au itabidi tubadilishe Katiba ili aendelee kuwa raisi na tupate matunda ya uraisi wake miaka 20 ijayo, kama Corona haijatumaliza?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom