Naam wanajamvi!
Unaweza kusema sasa watanzania tumekuwa certified fools. Ukiwaangalia wale wote wanao sema apende asipende unaweza kuhitimisha kuwa they are fools of their own kind ! Hawana sababu ya msingi. Nilimsikiliza mmoja anasema kwa mambo haya aliyo fanya Magufuli aendelee mpaka mwisho wa nguvu zake!! Najiuliza kafanya yapi hayo? Maana mimi nikiorodhesha mambo aliyo fanya Nyerere Magufuli hata 10% hajafika na kamwe hatafikia.
Orodhesha mambo aliyo fanya Rais Mwinyi ndio utajua kuwa kuna mtu anajipigia debe yeye kwa kuwatumia the least educated fools. Mwinyi aliingia madarakani akakuta serikali ina balance zero. Kwa kushirikiana na akina Dr Ngasongwa wakakope fedha kwa Rais Mugabe ili kufufua uchumi. Kweli President Mugabe aliisaidia Tanzania bure kabisa dollar million 500! Wakakubaliana fedha hizi wasizitumie kwenye recurrent expenditure bali wazipeleke Bank kuu ili wafanya biashara wenye uwezo waagize bidhaa kutoka nje ili baadae serikali ianze kuwatoza kodi. Mpaka kufikia 1994 uchumi ukawa umefufuka. Uchaguzi mkuu wa 1995 pamoja na juhudi alizo fanya hatukusema APENDE ASIPENDE LAZIMA AENDELEE! Kwanini? Tuliheshimu KATIBA.
Njoo kwa mkapa. Alifanya kazi kubwa sana.Barabara nyingi nzuri zilijengwa wakati wake. Daraja la Mkapa kule Kibiti limejengwa wakati wa utawala wake. Daraja la mto Malagalasi lilianza kujengwa utawala wa Ben! Wakati anaingia madarakani GDP ilikuwa US Dollar million 29 ameondoka GDP ikiwa US dollar mill 45. What a good work. Pamoja na yote hayo hatukusema APENDE ASIPENDE LAZIMA AENDELEE! Kwanini? Tuliheshimu KATIBA.
Rais Kikwete ameingia madarakani amekuta GDP ni US dollar million 45, ameondoka madarakani GDP ikiwa ni US dollar million 58! Aliajiri kila mwaka, alipandisha wafanyakazi kila mwaka, nyongeza za mishahara kila mwaka. Ndiye aliye leta uchumi wa kisasa na maendeleo ya watu na vitu. Aliimarisha Demokrasia ya vyama vingi. Vyuo vikuu vingi vimeanzishwa wakati wake. Alipendwa ndani ya Chama na nje ya Chama. Ni rafiki wa watanzania. Muda wake ulipo isha akaondoka zake.
Sasa huyu Mwana kwetu John Pombe Magufuli, ameingia madarakani amekuta deni la Taifa ni shs trillion 45 ndani ya miaka mitano deni limefikia trillion 53. Kwa miaka mitano hajatoa ajira kwa vijana wala kuongeza mishahara kwa watumishi Wa umma. Kati ya 2016 mpaka 2021 mabenki 10 yamefilisika na kufunga shughuli zao. Hotel kubwa zenye hadhi ya nyota tano zimefilisika, shule nyingi za binafsi zimegeuzwa hostel. JE NI WATU WANGAPI WAMEKOSA AJIRA AU KUACHISHWA KAZI KWA TAASISI ZAO KUFUNGWA?
Sawa amejenga fly over, unaweza kulinganisha na daraja la Mkapa? Anajenga SGR, sawa , unaweza kulinganisha na reli ya TAZARA ya NYERERE? Anajenga sijui nini huko, sawa lakini unaweza kulinganisha na Mashirika ya umma 457 aliyo anzisha Nyerere? Kwanini APENDE ASIPENDE? Naona slowly we are becoming certified fools. Tunashangilia nini hasa?