Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Labda umepotea wewe,sie tuliemchagua,hatuna chembe ya wasi wasi nae acha mnyooke kwanza
 
Habari zenu wakuu.

KWANZA NAOMBA WATU WENYE UFAHAMU NDIO WACHANGIE MADA HII. KAMA HUJUI CHOCHOTE TAFADHALI KAA PEMBENI USOME TU.

Kwa mambo yanavyokwenda sasa hapa nchini yananifanye nihitimishe kwamba kiwango chetu cha elimu ni cha chini. Kuna vipaombele vingi vya kufanya kuwatoa watanzania katika umasikini lakini badala yake tunashuhudia yafuatayo:

1.Wapinzani kukamatwa
2. Mikutano ya wapinzani kufungiwa.
3. "Bei elekezi" kwenye bidhaa ya sukari
4. Kuhamia Dodoma.

Hivi kweli haya ndio mambo yatakayo wakwamu watanzania kiuchumi, kuwapa ajira na kuwaondoa kwenye umasikini?

Kuna watu watabisha na kusema kama suala la kuhamia Dodoma lilikuwepo kwenye ilani ya chama tawala, lakini lazima tujiulize, je hili suala lina kipaumbele?

Ukiunganisha na huu mfumo wa uchumi wa "bei elekezi" ndio nashindwa kabisa kuelewa tunakwenda wapi. Kanuni ya kiuchumi ninayoijua mimi nikwamba serikali inasimamia ufanisi wa masoko kwa ku adjust supply and demand ili kutaka kufikia equilibrium price, lakini haya ya "bei elekezi" sijawahi kusikia.

Naombeni maoni yenu wakuu.
 
Vipaumbele ni jinsi vile JPM mwenye PhD ya UDSM anavyoona. Kuna tatizo bila shaka sehemu fulani.
Eti anadai mikutano ya vyama itazuia panadol hospitalini lakini hatuelezi jinsi ziara za Kinana zilivyomzuia JK kufanya kazi.
 
Nisije nakajikuta nimetukana bure[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
me sina milioni saba aisee siwezi kuchangia!!! Mwaka wa nne huu natembea kiguu na njia natafuta ajira sipati....hapa kazi tu naamini ipo siku ntapata tu!
 
Nchi haiendeshwi kwa matakea ya rais ndiyo maana kuna miongozo kama ilani, mipango ya muda mrefu na mfupi, katiba, sheria, miongozo na nyaraka mbali mbali. Wananchi ni haki yetu kuhoji, kukosoa, kushauri na kulalamika kama mambo hayaendi vizuri. Tatizo linakuja pale anayehoji au kukosoa anapoonekana adui. Tabia hii siyo nzuri na haiwezi kutupeleka popote kama taifa
Sasa hapa mnalalamika ama mnashutumu? mnashauri ama mnatuhumu? mbona hamuelewi hata ni nini tofauti ya hayo mambo.
 
Nchi hii inaelekea kuwa nchi ya Maziwa na Asali. Chini ya uongozi wa Magu, tutafika tu... Mungu atusaidie
 
Kwa tunaomuelewa, tunajua anataka kutupeleka wapi ndio maana nchi imetulia tuli na wananchi wako tayari kusikiliza na kutekeleza kile Rais wetu anatuelekeza. Ninyi wachache mnaoongea mitandaoni tu hamtamkwamisha Rais wetu. Pia tumewazoea. Hata wakati wa kampeni mliongea sana. Ni wachache walihadaika wakajiunga nanyi, lakini mwisho wa siku kila mtu anajua matokeo.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
kwa hali ilivyo ndio tunaelekea kwenye shimo refu sana
 
Hali ya maisha imekua niya shida sana ukipata leo hujui kesho utaamkaje kuifipi hali ipo hvyo kuna kitu kimepelekea kukundikia ujumbe huu naona mtiririko wa kodi umekua mwingi ni jana tu nmesikia ya kwamba unamkakati wa kuwabana wenye nyumba na wao walipe kodi ni kweli unaitaji hela ili ukamilishe mambo yako lakini mtukufu sana huoni kama untuumiza ss wanyonge tusiojua kesho itakuaje tuonee huluma mtukufu sana hivi hujui ya kwamba pindi utakapo waambia walipe kodi wenye nyumba maumivi yanakwenda wpi yanarudi kwetu ss wanyonge tulio kupa kura na tulikua mstari wa mbele pale Lumumba kwenye ofc ndogo za ccm ili uje tushelekee ushindi wetu leo yamekua maumivu kwetu sasa hv mtukufu sana kila kitu ni hela huna hela upati kitu hata kitu kiwe cha selikari ni hela hata kuangalia habr kwenye ITV ni lamza ulipie na tunaona matangazo mengi ukisema sasa hivi mapato yemeongezeka sasa hayo mapato unayo kusanya yanaenda wapi kama sio kwetu ili utupe huduma nzuri na ikwezekana kutupunguzia mzigo wa majukum sisi wananchi wako wa hali ya chini tuonee huruma baba tunao umia ni sisi wapiga kura wako nakumbuka kwenye kampeni zako ulisema unataka masikini waishi kwenye nchi yao tz kwa raha na amani sasa hiyo raha na amani vpo wapi au kwakua wewe kila kitu unaudumiwa na selikari yako ndio maana uoni huruma kwetu ss mi nakuomba waambie TRA wasitishe swala lao la kuchukua kodi kwenye nyumba za kupanga na waambie tcra tanesko pamoja na mamlaka ya maji watupunguzie kodi pamoja na milpo ya ving'amuzi ni hayo mtukufu sana najua wewe ni msikivu na unamuamini mungu nakutakia jumamosi njema ya usafi
 
Nimejikuta napata hisia za ndani baada ya kuusoma Uzi huu na nikilinganisha na hali iliyopo hapa nchini.Wakati sisi tunaohitaji hela ya field kwa muda wa wiki mbili sasa hatuelewi nini hatima yake maana tuliambiwa twende nyumbani kisha tarehe 9/8 turipoti kwenye vituo tulivyopangiwa lakini mpaka sasa hatuelewi tunaendaje ilhali mfuko hauna kitu.Mbaya zaidi tunaambiwa rekodi za ukusanyaji wa mapato umeongezeka lakini ongezeko hili halijaonekana katika hali halisi ya maisha ya mtanzania.Mungu tusaidie tuvuke hiki kipindi kigumu.
Nawaza kwa sauti.
 
LEO HAKUNA AJIRA KISIGIZIO UHAKIKI WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KWENDA FIELD BILA PESA YA KUJIKIMU KISA KUSINGIZIA ZOEZI LA UHAKIKI NCHI HII HAINA HELA NIMETOA UZI HUU ILI MAGUFURI AJUE KUWA KUDANGANYA UMMA SIYO VIZURI NA JAFFO WAZIRI KUDANGANYA UMMA SIYO VIZURI MMEDANGANYA AJIRA ZA WALIMU MPAKA LEO KIMYA KIAMA KINAKUJA TANZANIA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom