Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Yeye badala ya kwenda nchi kama malaysia na singapore kuuliza na kudadisi uchumi wa viwanda unafikiwaje? Yeye yuko kuhama na nzega anasema mimi sijaribiwi! Kweli maajabu yako Tanzania ambako mtu hajafanya mtihani ila anasubiri matokeo!
Nafikiri upinzani kuna kifu walifikitia, sasa naona huu mtego unaenda kunasa.
 
Viwada ilikuwa kuzugia tu.Hapa ni kupiga na kuua tu
 
Mta unda ngonjera sana awamu hii ya Magufuli
Nabado Magu kaza kaza zaidi.


"Nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni’"
 
Mimi pia naona tutafika,tena tutafika zaidi ya wenzetu wenye majeshi makubwa walivyofika,mwenye kunielewa ameelewa
 
..lakini katibu mkuu mpya anaonekana amepooza.

..jitihada za kukitangaza chama na kupata wanachama wapya hazionekani.

..bado tunasubiri ccm na serikali wakosee ndiyo viongozi wetu wanaibuka na matamko.

..jumuiya ya vijana wanaonyesha jitihada. Lakini hawa ni vijana.

..jumuiya ya wanawake imepooza kabisa. Ccm wanatushinda kwasababu wanawake hawaungi mkono Cdm.

..tunatakiwa tuanze kujipanga upya sasa hivi.

Nb:

..tuelekeze nguvu zaidi kupata madiwani na wabunge wengi zaidi.

..pia tutafute wagombea wazuri na mahiri wa Uraisi.
Ndugu unataka katibu Mkuu akitangazie wapi chama,chumbani kwake au??
 
Mta unda ngonjera sana awamu hii ya Magufuli
Nabado Magu kaza kaza zaidi.


"Nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni’"
Wewe si mtumwa tu, huna hata cha maana.
 
We MB.wa tunaounga mkono upinzani tupo zaidi ya miloni sita tena hapo ni baada ya kumleta huyo fisadi,tukileta fyoko hii nchi haitakalika,HUYO FISADI ALIPATA KURA MILIONI SITA NA LAKI SAB,SEMA MILIONI NANE

Kama upinzani hauna wafuasi wawaache wapinzani wajinadi
 
Ndugu unataka katibu Mkuu akitangazie wapi chama,chumbani kwake au??

..akitangaze vijijini.

..umemsikia amefanya ziara yoyote kukagua uhai wa chama?

..sijaona cdm wakija na mbinu mpya na hoja mpya.

..mateso tunayoyapata sasa hivi ni kwasababu ya kuwa na wabunge wachache wasioweza ku-influence maamuzi bungeni.
 
Serikali hii imeibua watumishi hewa, imewachukulia hatua wezi wa mali za umma pamoja na kuanzisha mahakama ya mafisadi, imethibiti mapata bandarini, imeleta nidhamu kwa watumishi wa umma, inasimamia ukusanyaji wa kodi n.k, haya yote yameokoa mabilioni ya fedha.Hahaha! Katika Serikali hii ikiwa inaendelea kutumbua majipu Wale wa upande ule wakaanza kuwatetea wale wezi na waliowanyonya wanyonge kwa muda mrefu. Katika serikali hii upinzani unaendelea kupotea kwakuwa mpaka sasa wanatapatapa kwa kukosa hoja zenye mashiko. Ila si haba kwani tumeshuhudia wakifanya maigizo bungeni kitendo ambacho kilichekesha wengi na kuona wamepotoka. Hawa watu ni wa kupuuzwa.
Kama serikali ni nzuri kama unavoisifia kwann inazuia freedom of speech kwann wanaziba midomo wapinzani wasiongee..?
I doubt huo uzuri wake...
 
..akitangaze vijijini.

..umemsikia amefanya ziara yoyote kukagua uhai wa chama?

..sijaona cdm wakija na mbinu mpya na hoja mpya.

..mateso tunayoyapata sasa hivi ni kwasababu ya kuwa na wabunge wachache wasioweza ku-influence maamuzi bungeni.
Tuombee basi kwa mtukufu rais,maana toka jamaa ameteuliwa tunazuiwa kufanya kila kitu,hata kuingia ofisin Shinyanga tulizuiwa
 
Hii speed ni ya kuelekea kuzimu.Tukianza kuchinjana sijui tutakimbilia wapi​
 
Hellow jf..
kwa wale wataalam wa haya mambo naombeni ufafanuzi wa hili swala.
raisi amekuwa akitoa matamko na maagizo mbalimbali yafatwe. mfano ktk hotuba yake ya leo hapa kahama ameagiza wafanyabiashara wa kipato cha chini wasitozwe kodi.
Ni jambo zuri lkn kipi kinamlinda huyu mwananchi ni tamko la raisi ama katiba ambayo ndio tunaifata na inaelekeza kipi kifanyike.

Hebu chukulia mfano wewe ni mwananchi cha chini anakuja mtumishi wa serikali kukutoza kodi we unagoma kisa raisi kasema hakuna kutozwa kodi,lkn tukija kwenye katiba inaruhusu mfanyabiashara yeyote lazima atoe kodi.
Kwa wenye uelewa wa haya mambo nijuzeni inakuwaje ktk hili.

Karibuni
 
wakati Dar anasema tuombe risiti hata ya biscut,huyu jamaa hajielewi nawaambia,kigezo cha kuwa mfanyabiashara mdogo ni kipii?
 
Utawala wa kidikteta chini ya Rais Magufuli, ni kovu la kudumu litakalobaki milele yote endapo hataamua kubadilika. Kigezo Cha kuleta maendeleo huku ukiminya demokrasia na Uhuru wa habari haikubaliki. kwa sababu hata Hitler aliiletea German maendeleo, Lakini wajerumani hawakumpenda. Sababu kubwa ni kuwa hakuna maendeleo ya kweli kama huna Uhuru na amani moyoni ukiwa na furaha na raha kwenye nchi yako. Maendeleo ya kweli ni Yale yanayompa mtu furaha ya kijisikia huru akiwa na haki ya kuzikilizwa na wajibu wa kuwasikiliza wengine Wenye mawazo tofauti.

Haina maana yoyote kuwa na Mali kisha ukakosa Uhuru wa mawazo na haki ya kusikilizwa. Hiyo ni sawa na familia tajiri yenye baba katili. Daima huwa haidumu.

Rais Magufuli badilika. Mabadiliko tunayoyataka ni pamoja na wewe kubadilika kutoka kutawala kibabe na kufuata KATIBA YA NCHI.
 
Huu mwendo wa dereva wetu naona umekua mkali sana. Yeye haoni cha matuta wala mawe yeye speed yake ni 180. Abiria wanapiga kelele lakini wapi hataki kuachia usukani. Kuna harufu za tairi kwa nnje abiria wanaomba gari isimame iangaliwe lakini dereva kagoma anasema anaijua gari yake tusiwe na wasiwasi,anasema kama kuna mtu hataki ashuke atembee kwa miguu. Nna wasiwasi kama dereva huyu atatufikisha salama na kama tufika basi lazima tuwe na manundu ya kujigongagonga kwenye gari kutokana na kurushwa sana.
Kuna abiria ni washkaji zake tumewaambia wakamshauri dereva lakini wanaogopa eti atawashusha njiani waliwe na simba.
Kwa kweli kama ni dereva tumempata na tutajuta kumpa usukani.
 
"JK aliwabatiza kwa Maji, JPM atawabatiza kwa Moto",
- Y. Makamba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom