Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Nilidhani umeandika kitu kipya kumbe wimbo ni ule uke tu. Safari hii mtapiga mayowe sana, mlizoea kujichotea na kuwaibia watanzania.
Binafsi nilikua siitaki CCM lakini hapa kwa Magu nampa support yangu.
Hayo uliyo yataja ni ya uongo na mengine hayana tija. Raisi hajakataza mikutano alichokataza ni mikutani ya hadhara na inayo vunja amani. Kuhusu bunge live? Kwani wewe hyna kazi ya kufanya? Wataga uangalie bunge halafu ukae tu bila kufanya kazi? Basi we ni mzembe. Na kwani hao wabunge tuliowachagua hatuwaamini huko bungeni? Hadi ukae uangalie bunge live?
Na hilo unalosema raisi ana ubinafsi na anajifanyia kama nyumba yake, kwani anachofanya anapelek nyumbani kwake? Yote aliyi fanya kwa muda huu mfupi ni mengi sana kuliko makosa anayo fanya.
 
Naiona Mpasuko ndani ya nchi,hakuna uzalendo tena,watanzania tumeanza kupoteza umoja,lakin enzi zina mwisho wap akina gadafi,mabutu,mubaraka n.k.leta maendeleo via haki lkn hili la maendeleo bila haki na sheria ndo yaliyomkuta gaddaffi.
 
Inasikitisha na inahuzunisha sana kwa Tanzania kuwa na Rsis wa aina ya Magufuli!
Tangu ameingia madarakani mheshimiwa JPM amekuwa ni mtu wa kutoa matamko yasiyo zingatia Katiba na Sheria na hii ni hatari sana! Rais anayeongoza Taifa lenye takribani watu milioni 50 kwa kuongozwa na hisia au mihemko ni janga kwa Taifa!
Kila kitu au mtu kuna sehemu ya uzuri na ubaya na huo uzuri au ubaya unapimwa kwa kuangalia upande upi unaoelemea mwingine!
Pamoja na sifa ya JPM kupambana na Ufisadi na kusaidia vijana wetu kielimu katika machache mazuri mizani inaelemea kwenye Wingi wa ubaya. Kitendo cha kuendesha nchi bila kufuata Katiba au Sheria ndiyo inabeba ubaya wa JPM kwa asilimia kubwa kama ni kwa aslimia basi ni 60-80%!
Kwa kiwango hichi cha ubaya wa JPM anajitengenezea kaburi lake na la chama chake cha CCM! Laiti JPM angelikaa siku moja na kutafakari kura alizopata mwaka jana 58%(8m votes) zidi ya UKAWA/Lowassa aliyepata 40%(6m votes) kati ya Watz milioni 40 alitakiwa kuwa mpole na kuwaheshimu wale 6m na wengine zaidi ya 25-30m ambao hawakupiga kura kabisa!
Kwanza Rais anapotamba na kuanza kuzuia mikutano ya siasa kwa kisingizio cha Hapa Kazi Tu siyo sawa! Rais anapozuia Bunge la JMT kuonyeshwa LIVE siyo sawa! Rais anapotumbua/fukuza/simamisha kazi watu bila kufuata taratibu na sheria za kazi hiyo si sawa!
Rais anapotisha wanachama tena wa Chama chake watakaompinga kuwapoteza hiyo si sawa!
Rais anapowatisha Wapinzani kuwa yeye Hajaribiwi na atakayejaribu ataona siyo sawa hata kidogo! Hawa Wapinzani wana haki na wana nguvu ya Kikatiba kufanya hivo na si kumjaribu JPM! Wana haki kuwatembelea na kufanya mikutano na wapiga kura wao zaidi ya 6m!Sasa unapozuia wasikutane eti tu kwa sababu hawakupata kura za kuingia Ikulu si sawa! Kwa maana hii JPM hatakiwi kufanya mikutano kwenye Majiji,miji na Majimbo yanayoobgozwa na wapinzani maana hawakumchagua! Je, hiyo ni sawa????
Nimalize kwa kusema kuwa OGOPA SANA MTU ANAYETANGULIZA UMIMI/UBINAFSI kwenye maswala ya kitaifa kana kwamba Tanzania ni nyumbani kwake,mkewe na watoto!
Sina hakika kama JPM amebahatika kusikiliza hotuba za wagombea Urais wa Marekani wa Demokratiki na Republican hasa mama Hillary Clinton ambsye Hotuba yake imesheheni "WE BELIEVE IN....." yaani Tuna amini na tutafanya 123,tuta...tuta....n.k! Na siyo NITA...... na majigambo kibao kama ya"Tanzania ya Magufuli,Serikali ya Magufuli n.k,n.k. Huo ni uzuzu wa kisiasa kutaka kuonyesha kuwa wewe peke yako unaweza na cyo Katiba ya nchi!
Kwa sheria na Katiba hizi anazotunga Rais majukwaani na kuungwa mkonon na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ni hatari sana kwa mstakabari wa nchi!
Watu waombe na kusali sana ili Mungu aondoe moyo wa kiburi na jeuri ndani ya Rais wetu vinginevo.........!!!!!????
Rais kachaguliwa na Watanzania awaletee maendeleo. Kama kawaida palipo mende na sisimizi hawakosi lakini tukishajumlisha kura Mshindi ndiyo huwa Rais hadi uchaguzi ujao. Tumechoshwa na wajanja wachache kutumia vipengele vya sheria kutufisadi kwa faida yao binafsi. Kaanzisha Mahakama ya Mafusadi lakini wajanha wachache Bungeni wakawatetea mafisadi kwa kutoka nje ya Bunge na kufunga midomo kwa cellotape. Wametuonea vya kutosha sasa tumechoka nao waache walielie.
 
Kuna watu wanazaliwa ili wawe viongozi?
Kuongoza nchi inatakiwa uwe na maono,hekima na,busara!

Ova
 
Chadema bana,eti mikutano nchi nzima kwa siku moja,kwa ajili ya nini?
Waliacha kutumia fursa hizi wakati wa Kakaya,wangeandamana kutaka elimu bure,kutaka mafisadi wa kwenye list yao wapelekwe mahakamani lakini waliishia kufanya operation za kisanii
Sasa mambo yamebadilka,serikali inafanya maamuzi yanayogusa watu wa kawaida,chadema inatetea wahalifu na wazembe kuwa wanadhalilishwa
Magufuli hajaribiwi,atatia ndani kamati kuu nzima,ndio maana zoezi limepelekwa mbali sept01,ili kupima upepo,baadae Mbowe atasema acheni waache wafu wajizike
 
Ninachokiona nikuwa waTz tumegawanyika sana kimawazo kuhusu uendeshaji wa nchi yetu. Na ni vizuri iwe hivyo lakini hili la mtu moja kuendesha nchi kama taasisi yake na maamuzi yote afanye yeye nafikiri si sawa .

WaTz tulikuwa na nafasi ya kufanya mabadiliko kiuchumi na kisiasa kwa AMANI bila vitisho e.g. mimi sijaribiwi, mtaona cha mtema kuni nk. Viongozi wote duniani waliotumia majeshi yao dhidi ya raia wao wenyewe mwisho wao haukuwahi kuwa mzuri (historia ni mwl).

CCM ilitakiwa ijue kuwa kwa kura za halali bila figisu ni zaidi ya nusu ya waTz waliwakataa . Sasa idadi hiyo ya wananchi hawatakiwi kuswagwa kama ng'ombe au kondoo bali ni kwa uongozi uliotukuka na wa kuheshimu watu. Lakini bahati mbaya watawala wanawachukulia wapinzani kwa kuangalia uongozi wa taifa (Mbowe, Lowassa, Seif nk) badala ya kuangalia ni kwa nini idadi kubwa ya wananchi watz waliwakataa.
 
Rais kimbia tu ukpotea njia utarudi kuanza, ila utafanya kosa kubwa sana kuwasikiliza watu wanachotaka wakati kinachotakiwa kinaonekana na kila mtu anakitaka kimoyomoyo.
Kuna sababu gani ya kumuuliza mtoto wako achague elimu au ujinga wakati elimu hailinganishwi na ujinga? Kiongozi bora ni yule anayejua wananchi wangu wanataka nini na wanatakiwa kuwa na nini hata kama hao wananchi hawajui wanataka nini. Kwanini uwaulize je mnataka maji safi na miundombinu wakati unajua hivyo ni muhimu kwao? Ukitafuta kuungwa mkono kwenye majukumu yako umekwisha na utachekwa.
Watanzania wanataka maendeleo na sio sauti za busara na maneno ya bublia na qur'an.
Mh. Lowasa hakuwa hata na sauti ya kuhamasisha au kauli nzuri za kuvutia zaid ya kutetemeka ila wananchi walikuwa wanampenda kwa kuamini ataleta maendeleo ndio maana walijazana kumuona wala sio kumsikiliza kwasababu hakuwa kusikika vizuri.
Endelea mbele maadui ni wengi sana, sio kazi ndogo kuwafyeka wote ila baada ya muda watakuelewa ulimaanisha nini
 
Mimi binafuc nimeanza kuwa na mashaka naye. Inawezekana akawa si mtanzania kaja kutuvurugia nchi yetu iliyokuwa na amani. Ona sasa nchi imetenganishwa katka magroup mawili tyar. Wapinzani na Wana CCM. Hwa kipind cha nyuma walikuwa wakikaa pamoja na kujadili mambo ya kimaaendeleo. Leo jamaa kaweka ukuta mkubwa kat yao. Eeeh Mungu Tunaomba umpe busara Raic wetu hata kidogo 2.
 
Tukisema hapa kuwa magufuli is one term president kuna watu wanatokwa na mapovu na makamasi.
Lazima hili litimie.
 
Mimi binafuc nimeanza kuwa na mashaka naye. Inawezekana akawa si mtanzania kaja kutuvurugia nchi yetu iliyokuwa na amani. Ona sasa nchi imetenganishwa katka magroup mawili tyar. Wapinzani na Wana CCM. Hwa kipind cha nyuma walikuwa wakikaa pamoja na kujadili mambo ya kimaaendeleo. Leo jamaa kaweka ukuta mkubwa kat yao. Eeeh Mungu Tunaomba umpe busara Raic wetu hata kidogo 2.
Walioanza ubaguzi ni wapinzani,walitoa tamko kutosalimiana wala kushirikiana na ccm mkaa kimya
UKUTA umeletwa na chadema ili kutenganisha watanzania
 
Nilidhani umeandika kitu kipya kumbe wimbo ni ule uke tu. Safari hii mtapiga mayowe sana, mlizoea kujichotea na kuwaibia watanzania.
Binafsi nilikua siitaki CCM lakini hapa kwa Magu nampa support yangu.
Hayo uliyo yataja ni ya uongo na mengine hayana tija. Raisi hajakataza mikutano alichokataza ni mikutani ya hadhara na inayo vunja amani. Kuhusu bunge live? Kwani wewe hyna kazi ya kufanya? Wataga uangalie bunge halafu ukae tu bila kufanya kazi? Basi we ni mzembe. Na kwani hao wabunge tuliowachagua hatuwaamini huko bungeni? Hadi ukae uangalie bunge live?
Na hilo unalosema raisi ana ubinafsi na anajifanyia kama nyumba yake, kwani anachofanya anapelek nyumbani kwake? Yote aliyi fanya kwa muda huu mfupi ni mengi sana kuliko makosa anayo fanya.

Wewe ni yule hater ambao huna mtu au ndugu aliyearthirika na kukurupuka kwa huyu jamaa.Wewe ni kimaskini fulani ambaye kutwa unawatakia wengine walio juu yako mabaya.

Sio kila mtu aliyenazo ni mwizi na sio kila tu anayelalamika ujinga na upumbavu wa kuwagawanya watz ni maskni tu hata matajiti wapo. Uongozi unahitaji hekima na sio kuropoka na kufanya mambo bila kuangalia kona zote.
 
Mapema hivi mumeshaanza kulia kuunguzwa na ubatizo wa moto?. Kweli mlizoezwa vibaya.
 
Kuna ufahamu na ufahari pia kuna viongozi na viangazi
 
Ukiwa wataendelea kuwa wakiwa mpaka 2020 maana hawajitambui, hivi halima mdee yupo wapi jamani?
 
Kwani wewe una ramani ya kujua unakokwenda? Wacha kukariri leadership style Nchi ilioza kweli kweli acha Mkuu aisafishe utaona ramani mbele kama, ufisadi, uzembe, uonevu, upendeleo makazini,matumizi mabaya ya madaraka / Ofisi na wizi ndio umeziba ramani ya nchi kaa utulie utajua unakoelekea kwa kwenye maguezi yoyote makubwa hatajua unaelekea wapi mpaka vifusi vilivyo barabarani vitolewe
 
Rais kimbia tu ukpotea njia utarudi kuanza, ila utafanya kosa kubwa sana kuwasikiliza watu wanachotaka wakati kinachotakiwa kinaonekana na kila mtu anakitaka kimoyomoyo.
Kuna sababu gani ya kumuuliza mtoto wako achague elimu au ujinga wakati elimu hailinganishwi na ujinga? Kiongozi bora ni yule anayejua wananchi wangu wanataka nini na wanatakiwa kuwa na nini hata kama hao wananchi hawajui wanataka nini. Kwanini uwaulize je mnataka maji safi na miundombinu wakati unajua hivyo ni muhimu kwao? Ukitafuta kuungwa mkono kwenye majukumu yako umekwisha na utachekwa.
Watanzania wanataka maendeleo na sio sauti za busara na maneno ya bublia na qur'an.
Mh. Lowasa hakuwa hata na sauti ya kuhamasisha au kauli nzuri za kuvutia zaid ya kutetemeka ila wananchi walikuwa wanampenda kwa kuamini ataleta maendeleo ndio maana walijazana kumuona wala sio kumsikiliza kwasababu hakuwa kusikika vizuri.
Endelea mbele maadui ni wengi sana, sio kazi ndogo kuwafyeka wote ila baada ya muda watakuelewa ulimaanisha nini
Nani alikwambia wananchi wanataka maendeleo bila kujali kama wanaongozwa kwa mujibu wa sheria? Leo kura zikipigwa tena Magufuli anaweza kupata kura za watumishi anaowafukuza bila kufuata sheria? Anaweza kupata kura za wanafunzi aliowaita vilaz.a? Anaweza kupata za walimu aliosema wakatwe mishahara madawati yakivunjika?
Kwa nini tunamdanganya rais wetu akosee baadae tuanze kumcheka kama Kikwete? Lakini akiiharibu Tanzania tunafaidika nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom