Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Kwahiyo sasa wale wabunge wa ccm wanaishi Dar ambao huwa hawaendi majimboni kwao sasa wamepata kisingizio cha kutoitisha mikutano ya wananchi kuwapa milejesho!!Mustakabali wa kinachoendelea kwa sasa utatoka ndani ya ccm yenyewe! Chama kimesurrender kwa mtu mmoja wote wanamsikiliza yeye tu! Anasema hadi 2020 serekali itakuwa imehamia dodoma kesho yake unasikia mawaziri kila mmoja anatamka tarehe ya karibu kuhamia dodoma kumshinda mwenzake, anasema sukari bei elekezi ni 1800 viongozi wote hadi Waziri mkuu nae anacheza wimbo huo bila hata kuhoji, anasema kuna watu walikuwa wanaimba tuna Imani na mtu fulani ningekuwa mimi mwenyekiti ningewapoteza watu wazima wanacheka kama mazuzu hata hawahoji ungewapotezaje? Anasema hapa kazi tu kila mtu anacheza hapa kazi tu wakati hamna kazi, anasema mikutano ya siasa hadi 2020 watu bila kuhoji wanacheza nyimbo yake hadi Waziri mkuu, hamna mwenye courage ya kumwambia umekosea, wakitoka njee ndio unasikia wanaulizana umemwelea muheshimiwa? Wengine ndio unasikia huyu jamaa haeleweki nakwambia hii nchi itamshinda. CCM ya sasa inaendeshwa na mtu mmoja wenye weledi wamebaki kushangilia ili wapate chakula cha kuishi!
Na vyama vya mfukoni kama cha Dovutwa nadhani wanafurahia ili wasiwajibike kutumia pesa zao kuandaa mikutano mpaka 2020 ccm itakapowapa fungu lingine la kufanyia maigizo ya siasa.
Matokeo yake Dovutwa anagombea urais uzinduzi mbagala kampeni ni kubandika posters tu kamaliza pesa iliyobaki anaitafuna na familia yake.