Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
ANATUPELEKA MAHALI AMBAPO TANZANIA NCHI YETU ITAKUWA HEAVEN ON EARTH! anaye amini itakuwa kwake! asiye amini imekula kwake! HAPA KAZI TU!
 
Kila siku mimi nasema,watu kama ninyi mnaokosoa utawala wa Magufuli muwe mnakuja na ushauri pia kuwa atawaleje. Tena kwa kutolea mfano kuwa "ningekuwa mimi rais ningefanya 1,2,3", tukaona mawazo yako.
Maana nchi inajengwa na wenye nchi na kila raia ana uhuru wa kutoa nchango wa mawazo yake.
Lakini hii tabia iliyojitokeza sasaiv jf ya kukosoa bila kutoa mchango wa mawazo mbadala, mtakuwa wale mliokaririshwa kitu,kama walivyokaririshwa kitu wajumbe wa bunge la katiba.
Wasomi ngazi ya maprofesa walijifyetua akili kwa ajili ya manufaa ya matumbo yao, na si kwa manufaa ya umma mpana.
Toa mchango wako wa mawazo binafsi tukupime.
Raia tusiofungamana na upande wowote,tunaona utawala huu umeanza vizuri na ndiyo tuliokuwa tunautska sisi. Nyota njema huonekana asubuhi.
Tena mliotumbuliwa ama kuguswa na fyagio la Magufuli ndomnatokaje povu!
Mwacheni rais wetu atawale mbona anatawala vzuri tu? na kwa taarifa yako sisi raia wapenda maendeleo tupo nyuma yake na tunamuunga mkono kwakuwa hadhulumu mali za wanyonge.
 
Hebu tusaidie naww maana umelaumu wenzio kisha umepita mlemle...VAT kwenye miamala ya PESA anatakiwa alipe nani..Kampuni inayotoa huduma aww
 
Hebu tusaidie naww maana umelaumu wenzio kisha umepita mlemle...VAT kwenye miamala ya PESA anatakiwa alipe nani..Kampuni inayotoa huduma aww
Ni Kampuni inayotoa huduma ndiyo jibu. Lkn kwa kuwa limejitokeza kundi linalo kwenda "against" na yeye, kama vile shetani afanyavyo kwa M/Mungu. Tunachoshukuru, kila anayeonekana anahujumu harakati zake anamuweka pembeni sawia na wembe wake wa kutumbulia haupotezi makali
Atafanikiwa kwa sababu anataka haki itendeke,watumishi wawajibike nk nk. Watu washazoea sana "kupiga" bila kuwajibika,ndovilio unavosikia. Ivi kama wewe ni mwizi ushazoea kukwapua,kwanini mwenye mali anapostuka akaweka geti kali kuzuia mali zake zisiibwe zibaki salama,wewe mwizi unahakigani ya kulaumu mwenye mali pale na kuanza vijembe? Kisa eti umewekewa getikali! Ndo nikasema? Sisi wapenda haki na maendeleo tunamuunga mkono. Na mara zote mwanzo huwa mgumu, tutavumilia kwa sababu serikali ipo kwenye mstari.
 
Unauhakika naulichoandika kuwa maKAMPUNI ndio yanalipa au umekariri...Hadith za Dr MAPANGO!!,,,Mara ya mwisho lini kufanya muamala aidha wa Bank au simu....
 
Unauhakika naulichoandika kuwa maKAMPUNI ndio yanalipa au umekariri...Hadith za Dr MAPANGO!!,,,Mara ya mwisho lini kufanya muamala aidha wa Bank au simu....
Ww haujanisoma vzuri. Bora ukafuatilia kwa makini niachoandika, itafikia sehemu twende sambamba. Nimesema hivii? Wanaotakiwa kutoa hiyo kodi ni makampuni. Ila kwakuwa kila jema analolifanya kwaajili ya wananchi,kunakikundi kinachompinga na kufanya maagizo yake hayatekelezeki. Haiwezekani Waziri aseme kodi zutalipwa na makampuni,af'asimame cjui director kukanusha! "Contridiction" hii ndoupinzani wa chinichini niliouleza na ndiyo majipu menyewe hayo anayohangaika nayo.
 


Can you distinguish between Macroeconomic and micro economic theories? tafuta elimu utajua maana ya mleta uzi
 
Nchi hii inaendeshwa kwa Taratibu na Sheria haindeshwi kwa Matamko....Bungeni ilipitishwa Sheria kwamba VAT ilipwe inavyojulikana VAT anailipa mlaji wa Mwisho nivipi leo useme maKAMPUNI ndio yalipe..huoni kama kuna blah blah ukiona watu hawatekelezi manake wanafata Sheria sio amri ya MTU sikiliza ndugu Serikali hii imeamua kuumiza watu wadogo ingawa yenyewe inajinasibu kwamba inasaidia wanyonge...Umesikia CRDB kuhusu Mikopo?
 
Tatizo hana maono ya wapi anatupeleka ,zaidi sana anajaribu kurudisha utendaji Wa kawaida Wa jinsi serikali ipasavyo kufanyakazi ,hila tatizo tena Sijui ni aina gani ya utawala anao taka urudi !!!??
 

Nadhani mtoa mada anamaanisha jukumu la Rais kiutendaji na kiutawala kwa maana ya kuzitumia fursa na changamoto za kitaifa kujikwamua
 
Habari za weekend wadau. Wote tumeona jinsi Rais wetu alivyojitahidi kutumbua tumbua wezi na wabadhirifu wa mali ya umma waliokwiba sana kwenye vipind vya tawala zilizopita hasa utawala wa awamu ya nne. Mimi nampongeza kwa hilo kwa moyo wa dhati kabisa.
Rais pia ameonyesha dhamira yake Kwa kujenga mahakama ijayo shughulikia kesi za wizi wa mali ya umma ili kurahisisha uendeshaji wa kesi hizo.

Tatizo langu ni kwamba hivi wezi wa mali ya umma walikua ni wafanyakazi tu. Mbona wanasiasa na wafanya biashara wakubwa hawaguswi.
Nakumbuka hata kwenye wizi wa epa tuliambiwa warudishe kimya kimya?
Hivi mnatuaminisha kitu gani hapa? Akihutubia bungeni Rais alituhakikishia hakuna mwizi atakayesalimika na aliongea kwa tone kubwa.. Ndo imeishia hapo kweli? Labda tumkumbushe huyu mkuu Kuna wezi wanasiasa huku :

1.tumbua wezi wa ESCROW
2.Richmond
3.mabehewa feki
4.kivuko kibovu
5.epa
6.kagoda
7.uda
Na kadhalika.. Msipofanyia kazi kashifa hizi na zingine nachelea kusema hapatakua na tofauti yoyote na tawala zilizopita.. Kwani pamoja na baadhi ya mzuri tuyaonayo kuna mapungufu mengi yameanza kuonekana kwenye utawala huu. hata Baba Riz kuna mengi mazuri kayafanya ukiacha mabaya yanayo tamkwa.
Mfano mwingine nguvu ya kupambana na vyeti feki imeelekezwa kwa wafanyakazi wa umma kwa kiasi
Vipi kwa wanasiasa? Au ndio kwamba wao hawagusiki.. Ukiacha wale wa upinzani mnao waweka ndani kila uchao. Kagueni na huko muone vituko

Nawasilisha.
 
Ukisema Watumishi WA umma unakosea, sema WALIMU ndio kutwa wanapigwa mikwara, Leo WAZIRI mkuu ameagiza Wakuu WOTE WA SHULE wasio NA shahada wakasome o.s watatumbuliwa. Pia waratibu Elimu Kata wakapige book wapate degree Sasa huku sio kudharirishana? Mbunge ajue kusoma na kuandika, Mkuu WA SHULE awe na sifa kama mgombea urais? IMBOMBO NGAFU NKAMU
 
kama ufisadi umetokea mahali watu wa kwanza kushughuliwa ni waliosaini makubaliano au mikataba husika. wanasiasa huwa hawasaini wenyewe huwa wanakaa pembeni wanashinikiza wapozwe au watapiga kelele.
hapo ni ngumu kumtia hatiani mwanasiasa maana hakuna ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja
 
Kaaazi kweli kweli nchi ya maagizo hii na kwa walimu na wakuu wa shule ndio zaid but all in all time will tell
 
Hapana mkuu.. Ukweli ni kuwa wanasiasa wanalindana sana. Mifano hii hapa

1.Rada
Upinzani : kuna ufisadi kwenye rada na mhusika makengeza
CCM na serikali : hakuna ufisadi kwenye rada, makengeza hausiki

Uingereza : kuna ufisadi mhusika mkuu makengeza
CCM : butwaa..
Serikali : tunaomba hiyo chenji tununulie vitabu

Hatua gani ilichukuliwa kwa makengeza???
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…