Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa....

HAYA ZUNGUSHAA ZUNGUSHAAA TENAA ZUNGUSHA MIKONOOO....MABADILIKOOOO!!!
Watu hawasomi wanakurupuka tu!
 
Namba tumeanza kuisoma moja baada ya nyingine. Uzuri wa namba haibagui, Namba haina tofauti ya matamshi inasomeka vilevile kama ni 1 ni 1.

Mwanafunzi ataisoma, mbunge ataisoma, mkulima ataisoma , Mnywaji itaisoma, mpangaji ataisoma, mfanyakazi ataisoma hata wale wazee wa kupiga virungu budget hii VAT itawahusu. Unaona njisi gani namba haina ubaguzi.

Ni muda muafaka serikali kuweka kodi ya kichwa kwa kila alietimiza miaka 18. Hi itasadia kujitegemea mapema na wananchi kujishughulisha sana na shughuli za uchumi.

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wahenga walisema isipokufa haizai; huenda pia ni kweli Tanzania ya kale isipokufa mpya haiwezi kuzaliwa. Tukubali kuinywa sumu ilimradi inahuisha; anachofanya Magufuli ni sumu kwa wengi, maisha yatatetereka, mazowea yatakoma hata yale tunayoyapenda sana. Bunge litaonekana kama sio lenyewe linaburuzwa, demokrasia itaonekana inahujumiwa, nk. hilo ndilo tanuru la moto; natung'ate meno tupite humo kwa uchungu kwa manufaa ya kesho. Mradi wote tunakubali tumepata jembe, basi tuweke tumaini letu sote hapo. Wote tumuunge mkono, tukae nyuma yake, tuone anatufikisha wapi; hili lisijalishe upinzani wala jumuia za kijamii. Kiongozi wetu jembe anayo maono, si vyema kukwazwa na vibwagizo vya demokrasia za majukwaani au makelele ya kila uchao hata hajapata wasaa wa kusimamisha agenda yake na mizizi kuota. Tena ingefaa siasa za majukwaani zikome kwa mwaka mzima au hata miwili; kama jembe anatufikisha kwa njia ya mkato shida iko wapi? demkrasia ni njia na udikteta ni njia pia, lakini ya mkato. Suala hapa ni kufika na kama hatufiki si itakujaonekana tu? si kila mwananchi atajionea mwenyewe? kuna haja gani kuwalazimisha watu kuvuka daraja ambalo hawajalifikia? Watanzania sio wajinga wa kufanya kujulishwa matatizo yao; wanayajua kama yapo.
 
Kwa dalili ninazoziona kila kona ya nchi hii ni harufu mbaya ya vurugu na machafuko kama serikali haitachukua tahadhari ya kujiepusha na ubinyaji wa demokrasia unaochomoza.

Kuna mbinyo mkubwa hivi sasa unaanza kujitokeza miongoni mwa uhuru wa vyama na wa mtu mmoja mmoja kiasi sasa kunaanza kujengeka hofu kwa watu. Hali hii inajenga chuki ya chini chini kwa wananchi.
 
Hakyamungu Sitawaangusha:

1. Hakuna kuonyesha bunge laivu
2. Haki ya kujieleza na kupata habari ipo majaribuni
3. Sukari kilo sh 3000-5000 ( bei elekezi sh 2000)
4. Sheria ya mtandao moto wa kuotea mbali
 
Hakyamungu Sitawaangusha:

1. Hakuna kuonyesha bunge laivu
2. Haki ya kujieleza na kupata habari ipo majaribuni
3. Sukari kilo sh 3000-5000 ( bei elekezi sh 2000)
4. Sheria ya mtandao moto wa kuotea mbali
Acha kuweweseka wewe,tulieni dawa ifanye kazi,HAPA KAZI TU.
 
Hakyamungu Sitawaangusha:

1. Hakuna kuonyesha bunge laivu
2. Haki ya kujieleza na kupata habari ipo majaribuni
3. Sukari kilo sh 3000-5000 ( bei elekezi sh 2000)
4. Sheria ya mtandao moto wa kuotea mbali
Inavyoonekana watawala hawajiamini na waoga wa kuambiwa ukweli wanataka kusifiwa hawapendi kukosolewa.
 
Hivi uchaguzi ukifanyaka leo hii jamaa atashinda kweli naona kapoteza kabisa mvuto.
 
Anapambana na ufisadi kidogo sana kuliko anavyopambana na demokrasia!

Nafikiri adui mkubwa kwake ni uhuru wa habari na demokrasia zaidi ya umasikini na ufisadi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom