Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
ilikuaje sasa akaaminiwa chadema hadi kupata nafasi ya kugombea uspika??chadema hawana intelijensia?? au chadema walikurupuka?

Mbona alikuwa naibu Waziri ccm unataka kuniambia ccm walikuwa hawana intelligence?
 
Duh! Vipi kuhusu Lowasa? Ina maana ninyi CHADEMA mnawaacha tu watu wasio wana CHADEMA wanakuja kuchukua vyeo kwa mgongo wenu? Kweli ninyi ni mazoba

Mimi sio mwanacdm japo nawakubali kwenye mambo mengi. Hilo la kumpa Medeye na EL nafasi yakugombea msimamo wangu uko wazi hapa jukwaani. Sikuwa na imani nao wala sintokaa niwe na imani nao.
 
Serikali iliyofeli kabisa ndani ya miezi sita tu! Huyu dereva wetu ana mori ya kufanya mazuri tatizo hana dira.
Ni sawa na catapila liache kulima barabara livamie mashamba
 
Serikali iliyofeli kabisa ndani ya miezi sita tu! Huyu dereva wetu ana mori ya kufanya mazuri tatizo hana dira.
Ni sawa na catapila liache kulima barabara livamie mashamba
kwahiyo tinga tinga limejigeuza kuwa trekta mkuu?
 
Mi nawashangaa sana mnaolia lia...subirini mpaka mwakani ndo tutajua tunaelekea wapi..ndo kwanza anafanya service ya gari mnalia..akianza safari je ?

Wekeni siasa pembeni tuijenge nchi yetu.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Acha kabisa kumsingizia Mwl. Nyerere! Kama Mwalimu Nyerere angelikuwa hai angeunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuhangaikia maendeleo ya wananchi. Labda angeweza kumshauri ktk mambo kadha wa kadha kwa manufaa ya wanyonge na si vinginevyo.

Ambaye hajui Rais Magufuli anafanya nini ni we we tu kwa sababu huenda ulikuwa jipu ukatumbuliwa ama una hofu ya kutumbuliwa. Kama ni 'ushauri wa mkewe' basi unafaa sana maana sisi Watanzania wenzio tunafurahia kazi nzuri inayofanywa na iliyofanywa na Rais Magufuli na Serikali yake ndani ya miezi sita tu! Huku niliko haijawahi kutokea! Mwenyekiti wetu mtaa anafanya kazi kubwa na nzuri. Kila Jumapili anafanya mkutano na wana mtaa kuhamasisha maendeleo, kushariana na kusikiliza kero nk. Wananchi wa mtaani kwetu tumekubaliana kuweka vyama pembeni hadi kipindi cha uchaguzi!
 
Mi nawashangaa sana mnaolia lia...subirini mpaka mwakani ndo tutajua tunaelekea wapi..ndo kwanza anafanya service ya gari mnalia..akianza safari je ?<br /><br />Wekeni siasa pembeni tuijenge nchi yetu.
 
utajenga nchi bila hela? watu ratiba ya kula imebadilika alf hio nchi itajengwa vp
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
This is explicit content [emoji106]
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
Acha UNAZI thread inajieleza fact za ukweli
Tatizo ULUMUMBA ndo unakuponza [emoji83]
 
Nchi haiendeshwi kwa matakea ya rais ndiyo maana kuna miongozo kama ilani, mipango ya muda mrefu na mfupi, katiba, sheria, miongozo na nyaraka mbali mbali. Wananchi ni haki yetu kuhoji, kukosoa, kushauri na kulalamika kama mambo hayaendi vizuri. Tatizo linakuja pale anayehoji au kukosoa anapoonekana adui. Tabia hii siyo nzuri na haiwezi kutupeleka popote kama taifa
Kweli kabisa mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom