Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana ! Ni hivi , uongozi mkubwa kama urais ni karama kutoka kwa Mungu , karama hii hailetwi na vifaru .

Mimi nimeshukuru sana kwa haya yanayotokea na naombea Hawa Masikini wa nchi hii waendelee kukomeshwa kwa dhiki na shida nyingi zaidi ili iwe fundisho kwa masikini wengine duniani .

Tumekuwa tukiwaelimisha kwa miaka mingi sana lakini hawaelewi , sasa Mungu kawatandika kibao cha uso waache wakome , asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu .

Adui mkubwa wa nchi hii ni ccm hakuna fukara yoyote wa nchi hii asiyelijua hili , akifuatiwa kwa mbaali na mwovu shetani , lakini wao wameendelea kumkumbatia tu , wacha wakione cha moto .
Wewe jamaa kiboko una hasira na masikini wa Nchi hii hadi unawaombea wapate shidaaaa mpaka wajue kuwa adui yao ni ccm!! nimecheka mpaka basi,sijawahi kucheka hivi maishani mwangu.
 
ENDELEENI KUPIGA DEBE NA KELELE HUMU JF,SERIKALI NI HII HII YA JPM NA SIO MIAKA 4 NA NUSU TU ILIYOBAKI NI MIAKA 9 NA NUSU ILIYOBAKI,WENGINE TUNACHANGAMKIA FULSA ZILIZOPO,WENGINE ENDELEENI KULALAMIKA HUMU HUMU TU TUONE MTAPATA NINI.,MUITE RAISI JINA LOLOTE LILE MTAKALO HAMUMBADILISHI KITU SANA SANA MTAISHIA KUKAMATWA MKIZIDISHA MAJINA.RAISI ANAFANYA KAZI NZURI SANA,NA WENGI TUNAMSAPOTI.MNAOJITOA UFAHAMU ENDELEENI TUONE MWISHO WENU.
wewe si umeambiwa ujiunge ili umtetee! wenzako tuna maisha tayari, wewe ndio unaanza kuchangamkia fursa leo?
 
Ni rais gn unahisi anaweza kutatua changamoto hii ndani ya wiki moja hasa ktk nchi ambayo wataalamu wa uchumi na wasemaji maarufu wanaziba midomo yako kwa karatasi nyeupe a.k.a "Don't dirty my mouth"
Labda tukuulize wewe , watu walioshindwa kwa miaka 60 kuleta angalau nuru tu kwenye nchi hii utawaongeza muda gani tena wa kuleta maendeleo ? Maana hata vipofu wanao uwezo wa kupapasa basi .
 
Wewe jamaa kiboko una hasira na masikini wa Nchi hii hadi unawaombea wapate shidaaaa mpaka wajue kuwa adui yao ni ccm!! nimecheka mpaka basi,sijawahi kucheka hivi maishani mwangu.
Vitabu vyote vitakatifu vimeandika kwamba UMASIKINI NI DHAMBI , maana yake ni kwamba ukiwa masikini unaweza kununuliwa hata kwa wali mkavu ili kukwamisha neema kwenye nchi .
 
Vitabu vyote vitakatifu vimeandika kwamba UMASIKINI NI DHAMBI , maana yake ni kwamba ukiwa masikini unaweza kununuliwa hata kwa wali mkavu ili kukwamisha neema kwenye nchi .
Kweli bwana umasikini ni noma sana. Siku hizi yule mpolepole toka apate ukuu wa kawilaya fulani kawa mtulivu anaspend my money zake!
 
UKAWA wameanza kulia lia. Kweli wameanza kuismoa namba
kwa kwi mama yako na wasukuma wenzako kwani wanaishi peponi si ndio wanaisoma namba mara mia treni imekuwa ndoto kwao ,mbegu za pamba wanapewa mawe, ng,ombe wanafukuzwa kwenye malisho, migodi kila siku inawauwa, samaki wanamalizwa kazaneni muwape pepo badala ya wao kuisoma namba mpaka Mwanza geita inakuwa mikoa ya mwisho kwa umaskini
 
Labda tukuulize wewe , watu walioshindwa kwa miaka 60 kuleta angalau nuru tu kwenye nchi hii utawaongeza muda gani tena wa kuleta maendeleo ? Maana hata vipofu wanao uwezo wa kupapasa basi .
Kukuwezesha wewe kupapasa na kupata simu nzuri ya namna uliyonayo na kuwakosoa kadri itakavyo nafsi yako ni sehemu ya nuru waliofanikiwa kukupa kwa miaka 60. Ni wajibu wako kujivunia nuru hiyo na kuwa balozi mzuri kwa vipofu unaowasemea
 
Napita tu mtanzania mwenzenu nikisoma ndiyo nitoe maoni.
 
Katika lugha huwa kuna maneno ya msimu kwa hivyo hilo lisikupe hofu muda wake ukipita litatoeka.... ni kama lilivyo neno mwendo kasi nk
Hivi kwanini mnapenda sana kutumia maneno haya "kubaka demokrasia" ..."katiba kubakwa" ..."ubakwaji wa haki"... Kwanini msitumie maneno kama "kukiukwa kwa katiba" ....." demokrasia kuwekwa kando" ......"sheria kutozingatiwa" .... Ila nyie mmekazana na kubaka tu, mara hiki kimebakwa, kile kimebakuliwa....
 
Nchi haiendeshwi kwa matakea ya rais ndiyo maana kuna miongozo kama ilani, mipango ya muda mrefu na mfupi, katiba, sheria, miongozo na nyaraka mbali mbali. Wananchi ni haki yetu kuhoji, kukosoa, kushauri na kulalamika kama mambo hayaendi vizuri. Tatizo linakuja pale anayehoji au kukosoa anapoonekana adui. Tabia hii siyo nzuri na haiwezi kutupeleka popote kama taifa

From Kudi Shauri;

Someni Hii Article:

President Magufuli: Tanzania’s Robin Hood

By Global Risk Insights Published: June 17, 2016, 6:37 am

Print

clip_image001.jpg
thehabarinetwork.com

President John Magufuli may be reducing corruption and security risks but has also influenced a trend toward increased risk of expropriation, creating uncertainty for foreign investors.

By Elliot Kratt ~ From Global Risk Insights

Tanzania’s government has commenced a national project which will see undeveloped land larger than 20 hectares seized from investors and given to farmers. In May 2016 alone, the government expropriated over 1,800 hectares of land and allocated it to poor Tanzanians; 80% of whom rely on agriculture for their livelihood.

The programme is being implemented because of the widespread problem of investors in agriculture and energy not meeting the requirements of their title deeds, which stipulate that a title holder should develop land within three years rather than holding onto it for ‘speculative value’.

William Lukuvi, Minister for Lands, Housing and Human Settlements Developments, claims that this policy will reduce security risks, such as clashes between communities competing over scarce resources.

The government and particularly President Magufuli have also made significant efforts to curb corruption, which has generated substantial popular support and impressed international donors. He has removed 10,000 ‘ghost workers’ from the government payroll and has on multiple occasions fired officials on the spot for suspected corruption or poor work-ethic. Most recently, he fired Charles Kitwanga, Minister of Home Affairs, on May 20th for attending parliament whilst drunk.

Such policies are undeniably beneficial for marginalised Tanzanians, but have at the same time led to uncertainty in the business environment – a trend that has characterised Magufuli’s presidency since he stepped into office in November 2015.

Understanding Magufuli’s mentality

For investors struggling to understand what influences his decisions, it may be helpful to think of him as a politically astute Robin Hood. Whilst he makes good political decisions in the interests of a poor population, they often have serious economic implications for those with capital, namely foreign companies.

However, Daudi Riganda, the Public Relations Manager of the Tanzanian Investment Centre, has recently stressed that since Magufuli has stepped into office, the number of investment projects in the country has increased by 20%. Evidently, the country remains an attractive destination for foreign investors but this is not without risk.

For agricultural or energy investors to effectively manage political risks, notably expropriation associated with the President’s mode of rule, it is important to understand his relationship to the political environment.

As an outsider during the leadership selection process, Magufuli has since made a conscious effort to assert his authority within the government. In order to manage political divisions in his party Chama Cha Mapinduzi (CCM) without resorting to corruption, he has employed a strategy of offering no carrot but a big stick (the potential for rapid redundancy and political alienation). The President seems to be ruling Tanzania through a negative or inverted patronage system. How sustainable this is remains to be seen.

Magufuli’s various crackdowns and policies may help him make gains politically – through generating popular support from Tanzanians and enforcing loyalty within the cabinet – but they also threaten to alienate key political figures whilst increasing political risks for investors.

Robin Hood’s impact on investors and economy

Tanzania’s economy may take a hit from political bullishness and various interventionist policies. The Tanzanian shilling is expected to experience a slowdown in depreciation. As a result, the government reportedly want to curb inflation and cut interest rates through controversial means, such as regulating the dollar accounts businessmen, forcing individuals to comply with new transparency principles and justify to the Bank of Tanzania their reasons for opening these accounts.

Magufuli’s policies often seem to spell trouble for investors. With little warning, the President is prone to make high-impact decisions with ostensibly little commercial consideration. In this respect, the expropriation, particularly of land, is rapidly increasing in frequency.

To manage risks and uncertainty in Tanzania, foreign investors should pursue a dual strategy of strict compliance with local laws and effectively engaging stakeholders to build strong political relationship with the government. This will be key in shielding investments from Magufuli’s fearless approach to “Robin Hood-onomics” of taking from the rich – in his view, investors that do not add value and corrupt government officials – and giving to the poor, his electorate, the Tanzanian farmers.

- See more at: President Magufuli: Tanzania’s Robin Hood
 
1. Serikali ya Magufuli ni Serikali ya Viwanda.

Swali: Nani atajenga viwanda? Serikali au Wananchi au Wageni?

2. Nitawashusha waishio kama Malaika ili waishi kama shetani?

Swali: Shetani ndio kipimo cha Mafanikio ya Serikali?

3. Nimejitoa Mhanga kutumbua majipu?

Swali: lugumi, escrow, Richmond, meli Chakavu, nyumba za serikali, kiwira, rada, kagoda, IPTL, .... Ni vipele?

4. Vyama vya siasa havitakiwi kufanya siasa mpaka baada ya miaka mitano.

Swali: CCM itakapokuwa inamkabidhi Magufuli uenyekiti hapo July 2016, itakuwa inaeneza injili?

5. Haiingii akilini mtu ana division 4 halafu anasoma degree.

Swali: yule Binti mwenyewe 4.30 anaesoma degree pale udom alifikaje?

6. Tumesitisha ajira zote Serikalini mpaka tuhakikishe tumeondoa wafanyakazi hewa.

Swali: Mfanyakazi akistaafu, kufariki au kuacha kazi Serikalini inachukua muda gani hazina Ku update database ya watumishi?

7. Elimu bure mpaka sekondari. Atakaechangisha wazazi atakiona.

Swali: Hii michango ya madawati huku mitaani kwetu ya kazi gani?

Utulivu wa mawazo, Hekima na busara ni vitu muhimu sana kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi.
 
Serikali hii kwa muda wote imekuwa ikijinasibisha ni wanyonge na masikini kwamba wao walichaguliwa na masikini, lakini ebu tuone hapa jinsi serikali hii ilivyo ya wanyonge
1.Serikali ya wanyonge ikawafukuze watoto wa wanyonge pale UDOM kama mbwa ikamuacha mtu aliyeingia pale kimagumashi.
2.Serikali ya wanyonge iliingia madarakani sukari ikiuzwa kwa kilo Tsh 1800 lakini wakazuia sukari kutoka nje huku wakijua viwanda vyetu haviwezi kukidhi mahitaji leo hii mnyonge ananunua sukari Tsh4000~5000.
3.Serikali ya wanyonge imekuwa ikijinasibu kuwa imeongeza ukusanyaji wa mapato lakini imeshindwa kuwapatia wanafunzi watoto wa wanyonge pesa zao za kujikimu kwa muda wa miezi miwili.
4.Serikali ya wanyonge imezuia ajira za wanyonge kwa kipindi kilichojulikana huku wao wakiajiri vyeo vikubwa visivyo vya kinyonge kama haitoshi mnyonge aliyekuwa anapata nyongeza kwa kila mwaka nyongeza hiyo imefutwa kwa sababu isiyo na mantiki.
7.Serikali ya wanyonge imesababisha wanyonge wanaofanya biashara ndogo ndogo kufunga biashara zao baada ya hali kuwa ngumu.
8.Serikali ya wanyonge huwachukua takribani mwezi mmoja kuendesha kesi na kumfunga mtu mnyonge aliyetukana lakini majizi yaliyoliibia taifa mpaka sasa hakuna aliyefungwa.

Neno ni moja tu Mungu huwa hawaafichi wanafiki.
 
Serikali hii imeibua watumishi hewa, imewachukulia hatua wezi wa mali za umma pamoja na kuanzisha mahakama ya mafisadi, imethibiti mapata bandarini, imeleta nidhamu kwa watumishi wa umma, inasimamia ukusanyaji wa kodi n.k, haya yote yameokoa mabilioni ya fedha.Hahaha! Katika Serikali hii ikiwa inaendelea kutumbua majipu Wale wa upande ule wakaanza kuwatetea wale wezi na waliowanyonya wanyonge kwa muda mrefu. Katika serikali hii upinzani unaendelea kupotea kwakuwa mpaka sasa wanatapatapa kwa kukosa hoja zenye mashiko. Ila si haba kwani tumeshuhudia wakifanya maigizo bungeni kitendo ambacho kilichekesha wengi na kuona wamepotoka. Hawa watu ni wa kupuuzwa.
 
Inabidi watanzania wajitambue hapa hakuna mnyonge anafaidi Bali in hii serikali hii ya ccm inaendelea kujitia kipato kwa sababu ni walewale
 
Serikali hii kwa muda wote imekuwa ikijinasibisha ni wanyonge na masikini kwamba wao walichaguliwa na masikini, lakini ebu tuone hapa jinsi serikali hii ilivyo ya wanyonge
....
8.Serikali ya wanyonge huwachukua takribani mwezi mmoja kuendesha kesi na kumfunga mtu mnyonge aliyetukana lakini majizi yaliyoliibia taifa mpaka sasa hakuna aliyefungwa.

Neno ni moja tu Mungu huwa hawaafichi wanafiki.
Serikali inajitahidi kumtumikia mnyonge. Serikali inajitahidi na imeweza kukopa fedha nyingi ili kizazi cha mnyonge wa leo kinyongwe kesho. Serikali inambebesha mnyonge deni ambalo mnyonge huyo haoni hayo maisha bora yanayopigiwa vuvuzela. Wanyonge wanajua kusoma namba? Isomeni hapa.
Habari ya mjini ni hii. link Raia Mwema - Kila Mtanzania sasa adaiwa milioni moja

Wanyonge na masikini ni lazima wafundishwe kusoma namba. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuwaamsha. Ndugu zangu wanyonge na masikini, tujitahidi kukaza mkanda. Kukaza mkanda na kukamuliwa kodi ndio zawadi inayomstahikia kondoo.

Wanyonge na masikini msiwe wenye kulalamika sana, cha kaizari apewe kaizari ili ajenge viwanda vya bei elekezi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom