Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Wakati lowasa anawaambia elimu bure mpk chuo kikuu walimwona kenge na kumtukana matusi yote mara mgonjwa,fisadi sasa hao mliowaona watakatifu ndio wanawanyoosha leo.tutaimba wote wimbo mmoja tu!..mpk akili zitakapowarudia.mtalimia meno
 
Walidahaliwa na nani?

Na wapiga madili wanaoshughulikiwa na MAGUFULI hivi sasa. Na ndio wanaopiga mayowe humu ndani wakidai "TUNAISOMA NAMBA!!!" Tuisome tu, DISCIPLINE lazima irudi. Akina JK na akina Lowasa waliifanya nchi hii kuwa ya HOVYO sana.
 
Wakati lowasa anawaambia elimu bure mpk chuo kikuu walimwona kenge na kumtukana matusi yote mara mgonjwa,fisadi sasa hao mliowaona watakatifu ndio wanawanyoosha leo.tutaimba wote wimbo mmoja tu!..mpk akili zitakapowarudia.mtalimia meno

Lowasa aliyasema hayo kwa sababu alijua kuna mazuzu yanayomwamini.
Harambee za kumwaga mabilioni misikitini na makanisani ziiliishia wapi siku hizi? au "marafiki zake" waliokuwa wakimchangia wanasubiri 2020?
 
Hahahahhaaaa
What Are Counting Numbers?
Counting numbers are the set of numbers that we use to learn how to count. 1, 2, 3, 4, 5, and so on. They are also called natural numbers—maybe since they feel natural to us because they are naturally the first numbers we learn. Sometimes they are also referred to as positive integers. In this lesson, we will learn what counting numbers are and what they are not and also look at some examples for clarification. Copied from study.com
Kitu kama Form njuka hiyo mkuu.
 
Ni lazima abomoe kwanza ili ajenge vizuri. Nyufa zilikuwa kubwa mno. Linchi lilikuwa linajiendea endea tu. Mavyeti feki kibao! wafanyakazi hewa kibao! wanafunzi hewa kibao! ufisadi kibao kiasi kwamba kulikuwa hakuna hata haja ya mtu kustrugle, maana kufanikiwa kwa mtu kulitokana na madili na kufahamiana tu. Si elimu wala strugle ya mtu. Nchi ilikuwa imeharibika sana na ilikuwa ikikatisha tamaa watu ambao kweli wanastrugle kufanikiwa. Mtapiga mayowe sana lakini MAGUFULI anainyoosha nchi na kurudisha utaratibu. Sasa tutaheshimiana tu. Asante Baba Magufuli Mungu azidi kukutia nguvu uirejeshe heshima ya kufanya kazi kwa bidii na watu kufanikiwa kwa bidii ya kweli na si kwa madili.
APA kaz tu
 
Muda mwingine unaweza kuona upo sahihi sana, ila mbeleni ukajua kuwa hukuwa sahihi.

Hivi ilivyo ndivyo imepangwa kuwa na Muweza wa yote, ndio maana hakushinda baba yako uchaguzi.

Alieshinda ni mtu na fikra zake na maono yake kwa sababu hakuzaliwa kwa bahati mbaya, na hakuwa pale alipo kwa bahati mbaya, ila kwa mapenzi yake Mungu.

Kumuunga mkono Kiongozi wako, hasa mkuu ni ushindi tosha dhidi ya maadui wengi. Usio wafahamu na unao wafahamu.

Kutokuwa na nidhamu, utulivu na usikivu ni moja ya kurudisha maendeleo ya Nchi yako nyuma kimaendeleo.

Ni vizuri kuwa namchango postive kuliko kuwa na mchango negative kwa Taifa letu lenye nia ya kufikia uchumi wa kati.
 
Nadhan hakuna kitu cha uhakika kama muda yaani muda haudanganyi tutasema sana lakini muda utasema 2020 siyo mbali kama ni mazingaombwe au ni nini kitajulikana kwa wakati huo, In short wananchi wamechoka sana kama wapo wanaofaidika na keki ya nchi hii basi ni 0.1 the rest are worse
 
Muda mwingine unaweza kuona upo sahihi sana, ila mbeleni ukajua kuwa hukuwa sahihi.

Hivi ilivyo ndivyo imepangwa kuwa na Muweza wa yote, ndio maana hakushinda baba yako uchaguzi.

Alieshinda ni mtu na fikra zake na maono yake kwa sababu hakuzaliwa kwa bahati mbaya, na hakuwa pale alipo kwa bahati mbaya, ila kwa mapenzi yake Mungu.

Kumuunga mkono Kiongozi wako, hasa mkuu ni ushindi tosha dhidi ya maadui wengi. Usio wafahamu na unao wafahamu.

Kutokuwa na nidhamu, utulivu na usikivu ni moja ya kurudisha maendeleo ya Nchi yako nyuma kimaendeleo.

Ni vizuri kuwa namchango postive kuliko kuwa na mchango negative kwa Taifa letu lenye nia ya kufikia uchumi wa kati.
Washauri wake tu hawasikilizi akusikilize ww?ndio shida ya kua na mtu aliezoea taabu anataka atutese na sisi
 
Leo kelele kibao mara ooh mikopo ya Chuo hakuna!Mara bank zimesitisha kutoa mikopo kwa watumishi wa umma, mara sukar imefichwa, mara yamebakia makopo mawili ya paracetamol,.....Hadi namba zote zitasomeka kuanzia real number,natural number,complex number, .....Si mlituona wajinga, tuone push-up zitafika wapi
Mhhhhhh....
 
uzuri mmoja tunaisoma namba wote sema wengine ni wabishi tu, bado miaka minne, wale wabishi nao ipo siku mtanyoosha mikono juu! nipo nachukua tu statistics humu
 
Niliposikia mizigo bandarini mizigo imekata nimefurahi kweli maana barabara zetu zimepona!,,,!, afu bado tunadai tuna kiongozi
 
uzuri mmoja tunaisoma namba wote sema wengine ni wabishi tu, bado miaka minne, wale wabishi nao ipo siku mtanyoosha mikono juu! nipo nachukua tu statistics humu
Mkuu mimi mmoja wapo ..huyu mzee Juma nilimuunga sana mkono nikijua ni mkombozi..ila kwa sasa nimegundua ni bomu la kutupa kwa mkono
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom