Ndivyo hali ilivyo. Inawezekana mwenyewe na wasaidizi wake wakaona wanapatia lakini kwangu mimi anabomoa tena sana.
Uchumi. Tunaambiwa makusanyo yamepanda hadi 1.3 Bill kwa mwezi lakini fedha haionekani na maisha yamezidi ugumu. Mizigo bandarini imepunguwa sana na hali ya uchumi hairidhishi.
Watu hawana ajira na ajira hazipo zimeyeyuka na ndio kwanza uhakiki wa wafanyakazi hewa unaendelea na ni zoezi endelevu sijui litaisha lini.
Huduma. Madawa hospitalini hayatoshi, idadadi ya wanafunzi waliokatiwa mikopo imeongezeka na malalamiko ya idara za serikali kukosa mafungu ya uendeshaji yapo japo kwa usiri mkubwa.
Hali ya Siasa. Mivutano na kuvurugwa kwa demokrasia, malalamiko ya kukiukwa katiba na haki za kisiasa yameongezeka ndani ya muda mfupi. Uvumilivu wa kisiasa unaelekea kuibuka na kupotezeana muda kwa kufanywa vitimbi vya makusudi vinavyoashiria kubomoka kwa misingi ya demokrasia iliyokwisha jengwa kwa muda wote wa siasa za vyama vingi tena sehemu zote mbili Bara na visiwani. Watu wananyimwa haki za kisiasa na uhuru wa kuzungumza . Kuna viashiria vya kidikteta kila eneo ambalo mtawala anaona ni hatari kwake. Mambo ni mengi tu.
Malalamiko ya wafanyakazi. Wafanyakazi wanatishwa na kutumbuliwa bila kufuatwa taratibu kazi iliyopo ni "Kutumbuwa, Kuteua na Kutengua" (KKK) hatuoni ufanisi. Kuna visasi na kutoaminmiana. wafanyakazi hawako huru kutumia weledi wao, wanasubiri maelekezo. Maelekezo hayana formula. Unaweza UKATUMBUWA KWA NAFASI YAKO KAMA MKUBWA WA ENEO LAKINI GHAFLA MAAMUZI YANATENGULIWA. Kumekosekana mfumo kuna maagizo tu kutoka juu.
Sera. Mimi siioni, sijui tunelekea wapi tena katika nyanja zote. Si kiuchumi ingawa tunaambiwa wa viwanda lakini siuoni msingi wake. Si kisiasa naona tunarudi nyuma sana na kupandikiza uadui na kushutumiana bure. Si kijamii nako kunaathiriwa na siasa mbaya vile vile. Sera ya mambo ya nje siijui, Tunaondowa na kuweka , Inasikitisha kwa mara ya Kwanza Tanzania Kuripotiwa Vibaya huko UNHCR na UN, tumeanza kupoteza heshima yetu na kutofautiana na rafiki zetu wa muda mrefu.
HITIMISHO. Kwa ufupi wa maneno wa makala hii fupi, ni muda wa mwaka tu tokea awamu hii ya tano iwepo lakini tumeshuka sana katika maeneo yaliyotajwa. Kwa mtazamo wangu malalamiko yamezidi, ajira hakuna, wafanyakazi wanalalamikia mengi, wanasiasa wanalia na kupaza sauti za demopkrasia, ajira hakuna na mengine mengi Hii si ishara nzuri.
Katika hali hii ,umoja wa kitaifa na amani ya nchi inakwazwa na uadui unajengeka miongoni mwa Watanzania. Kipindi hiki kifupi kimekuza nyufa kati ya WADAU wa kujenga Taifa letu na ukinzani wa mawazo kati ya Dola na watawaliwa umeanza kuibuka. Misingi ya Umoja hujengwa kwa sera madhubuti na kufuatwa KATIBA ambayo kwa sasa inasiginwa sana.
Kwa muhtasari huu Rais JPM kama kiongozi Mkuu wa Nchi hawezi kuepuka lawama na kwangu mimi anabomoa zaidi kuliko kujenga.
Kishada.