Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kumekuwa na lawama zinazomkabili mkuu wa nchi kuhusu mambo mbalimbali. Je shida iko wapi? Ni uelewa wetu mdogo hivyo hatujui afanyalo au uelewa wetu mkubwa zaidi tunaona anaboronga?
Tatizo rais kakamata maslahi ya watu wenye pesa hivyo wanatumia kila jitihada kuonyesha hamna kitu lakini wanaoelewa hawana shida. Rais endelea na majukumu yako usikatishwe tamaa na kundi hili la watu wanaokodishwa kuongea upuuzi katika mitandao ya kijamii. Wao jambo jema huligeuza kuwa baya. Komboa hii inchi kutoka kwa matapeli
 
Sitegemei mods waondoe Uzi huu na sitegemei wachangiaji watukane kama unaisi utatukana tafadhari usichangie hii ni kwa wale wenye upeo wa kufikiria kwa umakini.

Jumapili ya leo tu discuss hii kitu kwa umakini.

Mimi ni Catholic pure lakini jinsi maamuzi yanayofanywa na serikali sikatai kutumbuliwa kwa baadhi ya watu wezi wa serikali hii lakini hakuna really image inayoonekana baada ya kutumuliwa kwa baadhi ya watu kuendelea kuwepo kwa check and balance. Sehemu zingine akitolewa muislamu anawekwa mkiristo lakini akitolewa mkiristo analudishwa mkiristo why?

1: Katibu mkuu kiongozi
Alitumbuliwa Mkiristo - akaingia mkiristo

2: Afsa usalama wa taifa.
Aliondolewa muislamu- akaingia mkiristo ( tena mchungaji wa kanisa)

3: NSSF.
Aliondolewa muislamu - akawekwa mkiristo

4 : Sasa hivi mkurugenzi wa makosa ya jinai kaondolewa na ni muislamu nitashangaa akiletwa tena mkiristo .

Ukienda kwenye wizara waislamu ni kama 10% .

Sijagusa na kwingine maana ni kinyaa kitupu.

Kikwete aliwezaje kubalance cabinet yake na Taasisi zake?
 
Serikali inayo dini ila imejificha .chunguza wakuu wa wilaya wakurugenz na nyadhifa zote kama bodi ni 80% kwa 20%
 
Serikali sikivu sana, inawajali wananchi kwa kila namna, hata pale wapatwapo na majanga ya tetemeko la ardhi imekuwa mstari wa mbele kuwahi kuwaokoa kwa kutuma helikopita zenye misaada ya chakula na mablanketi pamoja na kuwajengea makazi ya dharura kwa haraka. CCM hoyee.
 
Kuna haja ya Watanzania kufanya maandamano....Makubwa na makundi yote yatoke

Sababu zipo na uwezo upo......uoga wako...ni umasikini wako

Uonevu ni Mwingi....Sababu ni nyingi..

A - Muswada wa habari na rushwa kwa wabunge

B- Mikopo ya wanafunzi

C- Fao la Kujitoa

D - Hali Mbaya ya uchumi kitaa

E - Wakulima kuzuiwa kuuza mazao yao popote (kwa nini wakulima wazuiwe?

Onyo: Wale misukule walio shiba unga m mbichi watakuja mbio na vijembe na vitisho

Ooo mara polisi or mara jeshi....

Watanzania wana wajibu wa kudai haki kwa namna yoyote
 
Wadau kwa siasa nilizoziona Tanzania hii ni utapeli mtupu napenda kuwashauri vijana wenzangu tusichague kazi hasa sisi tuliomaliza vyuo na level mbali mbali za masomo (O level & A level)
Nchi yetu wananasiasa wetu wametufanya wajinga yaan tumekua wakudanganywa na kunyonywa pia ahadi tulizoahidiwa kipindi cha kampeni hakuna dalili ya kutekelezeka tumerudishwa enzi za utumwa.
NB:2020 sio mbali sasa waache watutese tuu kwa hali hii IPO siku watu watashindwa kuwa wavumilivu vijana tunaonyesha utii na uzalendo juu ya serikali naiomba serikali pia kutuangalia wapiga kura.Kumbukeni wanasiasa sisi ni waajiri wenu na 2020 sio mbali mtakuja tuu kutuomba ajira na hatutafanya makosa walahi nawaambieni.
 
hakuna mtanzania yeyote atakaye niambia anasubiri 2020 ili kuutoa uongozi uliopo nikamwamini. Zaidi ukiamini unajitakia laana kwa Allah.
 
Kiukweli siji jutia kura yang kwa Hali ya uchum na ugum wa maisha ninao uona mtaani, kila mtu analia mama ntilie wateja hamna buchan nyama zinaoza wateja hamna, nyanya, mishahar inapunguzwa sekta binafs kutokana na kushuka kwa uzarishaji, Bill 850,ajira nje, watumishi hewa, posho za kutosha, mirad ilitekelezeka, madawa yalikuwepo, mikopo kwa wanachuo, safari za nje ndege kupishana angan, mchakato wa katiba mpya ulianza, bembejeo zilifika kwa wakati, increments on time , tusimtukane mamba kabla hatuja vuka mto , ubora wako mheshiwa Sasa nimeona ama kweli tuzo ulizo chukuwa ulistahili kuzipata kama kiongoz bora, mung akujalie maisha marefu, til 1.3 hakuna ajira mwaka mzima, mikopo shida, hamna safari za nje, madawa shida, bank Zina kufa, watumishi hewa nje, hamna increments, ajira kusitishwa, labda cjajuwa kanun za uchum,mung barik Tanzania na watu wake
 
Usipojutia ukijutia hiyo haituhusu...Ni maamuzi yako mwenyewe kwa utashi wako mwenyewe. Kama ulikuwa una akili za kuwapigia kura wasanii wa siasa ina maana level yako ya akili haipo pana sana kiasi cha kumuelewa nini JPM anafanya. Yeyote aliyepigia kura wasanii wa siasa hawezi keulewa sababu z waliompigia kura JPM sababu level yake ya akili ni ndogo sana kujua maendeleo yanapatikanaje katika nchi yeoyote duniani. Utakuja kumuelewa JPM sio sasa ila wenye maono wa wapi nci inapaswa kwenda tunamuelewa sana sababu tunajua gharama ya mafanikio ni kubwa sana. Usipokuwa tayari kuyagharimia mafanikio basi hustahili hata kuyapata mafanikio..
 
Wala hamna anaye mdrive, ni kwa pressure ya uraisi hawezi ndomana analalama lalama tu, mbona waliopita walikua hawalalami, he is unfit to be URT president, njia rahisi ni yeye kujiudhuru na sio kututesa wananchi.
[emoji28] [emoji28] [emoji85]
 
Anatupekeka kwenye neema baada ya majizi, mafisadi wakwepa kodi kubanwa
Kwahiyo wahitimu wa vyuo wanaosubiri ajira, wanafunzi wa vyuo vikuu waliokosa mikopo, wafanyakaz waliositishiwa ajira na nyongeza ya mshahara ndio majizi, mafisadi na wakwepa kodi? Tutake radhi bhana, mafisadi na majizi ni wale wa Richmond, iptl, escrow, lugumi, kigoda, etc na kwa bahat mbaya wanaishi kama Malaika, hawajaguswa mpaka leo, kazi yake kuonea tu wanyonge.
 
Safi ndio mana huwa kunakuwa na wa kwanza kufauru kutokana na uelewa wake na wa mwisho kuelewa kutokana na uelewa wake the same to say that? there's fast learners and slow leaners, for this situation let's wait for the coming year
 
JPM......tuangazie wananchi wako Hali si hali
Dollari inazidi kupandisha morii
Shambani jua linakuwa Kali na hali si shwari, ya kaisari anapewa askari Wajasiliamali tunabaki na mabakuli

Maisha yanageuka tofani tukumbuke asilani Wanazuoni kamwe hawawezi kuelewa hapakazi tu na njaa mifukoni, Elimu ya juu sasa imekuwa anasa maskini ni adimu kuipata.

Mapenzi kwenye familia yanazidi kuyeyuka na wazazi majukumu kuyatelekeza bila sababu kuzingamua

Sasa imekua pambio hatujinyongi, hatunywi sumu CCM mbele kwa mbele tumekubali sasa yetu ni matembele Na kande

Waacha waisome namba weeeee......CCM mbele kwa mbele
 
Tulipenda wenyewe.....ndi ndi!
Chaguo letu wenyewe...ndi! Ndi!
Wavimbe wapasuke...ndi! Ndi!
Wataisoma nambaaaaa....ccm mbele kwa mbeleeeee! Mmeipenda wenyeweeeeeeeeeee......chaguo lenu wenyeweeee,
Acha muisomeee nambaaaaaaa......... Ccm mbele kwa mbeleeeeeeeee WAPI HAMJAISOMA? INAKUJA SOON!
 
Hili ni ombi kwa mheshimiwa raisi kiukweli si ombi la kupuuzwa nchi inaelekea sehem ambayo si salama kabisa kuna mambo mengi yanatokea mabaya zaidi tunayoyajua na tusiyoyajua huu ni wakati mgumu sana zaidi ya ufikiriavyo kwa taifa letu inabidi tumweke Mungu asimame kutuongoza kuvuta salama katika kipindi hiki hivyo naomba mheshimiwa raisi tangaza japo siku moja tu watanzania wote tufunge Na kuliombea taifa tena kwa kulithamini hilo wewe kama kiongozi ndo uwe wa mfano
Kweli ndugu zangu haya mambo yanayotokea hapa kuna kitu ambacho kinaendelea kisichoonekana kimwili lakini tukiungana kumwomba Mungu naamini atatuepusha Na mengi yanayokuja
Muhimu sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom