Kuna msemo usemao kuwa siasa siyo uadui, na hilo lina ukweli ndani yake lakini pia wakati mwingine siasa inaweza ikageuka kuwa mwiba!
Mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi kulikuwa kuna wimbo uliokuwa na kiitikio kwamba tumeipenda wenyewe ambao ulipambwa na maneno matamu matamu pamoja na kuwa na vionjo vya aina yake, kitu kilichowafanya wapenzi wa chama kilichokuwa kikisifiwa na huo wimbo kuserebuka sana..
Sasa baada ya uchaguzi mambo yamegeuka kwa upande wa wale waliokuwa wakiserebuka, na ni kwamba wapo walioachishwa kazi, waliokatiwa mishahahara, waliokuwa na vyeti feki ambao wengi wameamua kuacha kazi wenyewe na kukimbia, waliofilisika na kufunga biashara zao, waliokuwa wakitegemea ajira serikali hadi sasa hawajapata, waliokuwa wakitegemea serikali iwape watoto wao mikopo ya elimu ya juu lakini wakanyimwa, n.k!
Kiufupi ni mengi yametokea na kila mtu ni shahidi, sasa hawa waliokuwa wakiimba hicho kibwagizo wamekuwa wakiwaangukia na kuwaomba msaada wale waliokuwa upande wa pili kwa aibu ili kuokoa jahazi, japo hizi namba zinasomwa pande zote lakini wafuasi wa kijani waliokumbwa na hayo yote wanatia sana huruma, na ni wepesi sana wa kusahau!
Hivyo siyo chuki wala kinyongo lakini....