Iwapo unasimamia ukweli daima utasimama peke yako (Lucky Dube if you stand for the truth you will always stand alone).
Katika jamii ambayo ukisimamia ukweli unahatarisha maisha yako na pengine kuyapoteza basi tusiendelee kuwa waoga tuseme ukweli lakini tukiweka ukweli huo Katika kumbukumbuku za maandishi, sauti, video nk ili kesho ukipotezwa vizazi vijavyo vikuone katika maandiko yako yaliyojaa ukweli tena ukweli wa ukombozi wa kifikra
Tutaogopa nini tena kama shule hazijengwi wala hospitali vinavyojengwa ni magereza ya kuweka wasemaji wa ukweli.
Tuogope nini tena Kama walimu na madaktari hawaajiriwi tena wanaoajiriwa ni washika bunduki.
Tutaogopa nini zaidi kama dawa hazinunuliwi kwenye hospitali zetu kinachonunuliwa ni risasi na bunduki.
Tuogope nini zaidi ya mateso tuliyonayo ya watu kufukuzwa kazi bila utaratibu, watu kutekwa, watu kupigwa risasi hadharani. Tuogope nini zaidi
Tuogope nini zaidi katika mazingira ambayo sheria na katiba haziheshimiwi anaye heshimiwa ni mtu mtu mmoja.
SIMAMIA UKWELI SIMAMA PEKE YAKO USHINDI WETU UPO KARIBU
Mwanahabari Huru
Swali la Kizushi: " WATU WASIOJULIKANA NI WATU KUTOKEA NCHI JIRANI?"