Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Haya mambo sio mageni,yameshafanyika sana tu kuanzia enzi za mwalimu.Ambae hataki,halazimishwi kuamini.
 
Unafiki mtupu, siku ya kufa kwako utabaki mdomo wazi, huko hatujafika hata kidogo na hatutafika, tender hutangzwa na hutolewa kwa yule aliekidhi vigezo na si vinginevyo.

Kama huko nyuma taratibu zilikiukwa na upendeleo ulitawala kwa wasio na vigezo kupewa tender, zama hizo zimepita, hanyimwi mtu tender kwa kabila lake, acha kupanda chuki, hailisaidii taifa, sanasana ni kuliangamiza
Open your eyes
 
Haisaidii nchi ni ya wote pambana na hali yako kama IPO IPO tu watatubania kila kona but mungu atazidi kutupatia mbinu zaidi za utafutaji
 
Mkuu huu mjadala nimekutana nao na wanatoa shuhuda mbalimbali. Yupo mmoja amesema kuwa aliomba mkopo ila alitakiwa kuthibitishwa na hazina ili benki imkopeshe. Jamaa kasema alinyimwa mkopo kutokana tu na kabila lake. Hii ni baada ya msajili wa hazina kumkataa. Tena ni huyu msajili wa sasa.Alipopeleleza akaambiwa kuwa kabila lake limemponza. Wanajiapiza kwa majina yao ya asili wanayaacha.
Tatizo mlishajimilikisha mali na miradi ya nchi hii. Kila penye pesa ninyi tu ndiyo mpate, wakipewa wengine UKABILA! Kwenda zakon. Hata makanisani kelele ni hizohizo. Matapeli wakubwa na wachonganishi nyinyi.
Kama haya ni ya kweli ambayo wanafanyiwa kabila hili basi nchi yetu tayari imegeuka. Ingawa tunaweza kusema ni ya kweli au siyo ya kweli, vipo vihashiria vinavyosema ni ya kweli.

Wapo watu fulani wakubwa tu wenye makampuni yao ambao walikuwa wamekaa kama kamati fulani kujadili namna ya kukabiliana na kile walichokiita changamoto wanazokabiliana nazo katika biashara. Watu hawa ni wa kabila moja maarufu sana Tanzania linalotoka kanda ya kaskazini. Kiukweli ni maneno ambayo nimeyasikia wakiyaongea tena wanayapa mkazo kwelikweli na mbinu ili kujikwamua.

Jamaa mmoja akasema yeye ni mtu anayeomba tenda mbalimbali za kusambaza vifaa kwenye taasisi za serikali ila amekuwa akipata changamoto ya kunyimwa tenda lakini akakiri wazi kuwa kabla ya utawala wa awamu ya tano mambo hayakuwa hivi! Huyo akadiriki kusema kuwa aliamua kuanza mchakato wa kubadili jina lake la ukoo kwenye documents anazoombea tenda ili tu asikatwe kwa kigezo hicho. Anakiri wazi kuwa walau hilo limeanza kumpa uhai. Naomba ninukuu baadhi ya maneno aliyosema "Siwezi kutumia tena jina la TARIMO kwenye kuomba zabuni. Limekuwa likiwa kikwazo kwangu! Hata wanangu wote nimewaambia wabadili jina lao la ukoo kwenye mambo yao ya shule! Wasitumie kabisaa jina hilo" Mzee huyo kweli akawa anasisitiza hivyo.

Katika maongezi yao kumbe kuna mama mmoja mfanya biashara ambaye alishauriwa asiweke jina lake la asili kwenye makabrasha yake ya kuomba tenda ya mabilioni ya fedha kwenye moja ya mashirika ya serikali. Nadhani aliyemshauri ni mmoja kati ya wazee waliokuwa wakijadiliana katika mjadala huu. Mara lile jina lake likaanza kujadiliwa. Nadhani hili jina linaweza kuwa linatokea Maeneo ya Wilaya ya Moshi. Lakini katika mjadala wao wakagundua kuwa jina hili halifahamiki sana kama jina la kikabila. Mara nikaona mzee mmoja akinyanyua simu na kumpigia yule mama na katika maongezi yake akamuambia "Kwenye documents usiweke jina la ukoo la mume wako! Hilo linajulikana, tumia jina la upande wa baba yako ambalo linaonekana siyo maarufu kulitambua" Kwakweli nimeacha mjadala ukiwa hot sana na inaonekana hili kabila limeanza kukutana na adha kubwakubwa za hapa na pale katika miangaiko yao ya kutafuta riziki.

Pamoja na hayo nalisifu kwa kung'amua hilo na kuanza kutafuta mbinu za kukabiliana na hili jambo.

Hayo ndiyo niliyokutana nayo kijiweni moja ya maficho maalum ya wazee maalum ambapo nilibahatika kuingia hapo baada ya kuwa nimempeleka boss fulani kumkutanisha na mtu ila huu mjadala umechukua muda mrefu nawanajadili kwa umakini na wanaweka uthibitisho! Wengine wanasema kuwa wanapigiwa simu kutoka huko juu na watu wanaowapenda na wamekuwa wakiwapa huo ushauri wa kuondoa kabisa majina ya koo zao au kuyaandika kwa herufi moja tu pale wanapotaka kuomba zabuni mbalimbali.

Hapa ni kazi kwa kazi.Tafuta mbinu ya kupata kazi!
 
We mtoa mada ni mchonganishi.
Naendelea kutafakari kwa nini umeamua kuchonganisha watu na serikali yao pendwa.

Huwezi ukabadilisha jina kirahisi. Mchakato wa kubadili jina huchukua miezi si chini ya mitatu na kuendelea maana lazima jina hilo litolewe kwenye government gazette kitu ambacho si kirahisi kama unavyofikiria.

Mods, ningewaomba mwondoe uzi huu maana hauna logic yoyote zaidi ya uchonganishi usio na maana.
 
Huyu mtu anacho sema Si uongo. Wanajiita John Stephen,Andrew Michael etc. wanafanikisha hata ktk ajira ndio wame acha kabisa majina ya Masawe, Shayo, Mushi.
Why ?
Wanadhani Watu wamesahau walivyokuwa wanaingizana kazini kikabila . Sehemu zote muhimu walijaa wao kiupendeleo una kuta ofisi ina Ndugu 10 wa familia moja. Mna fahamu hali ilivyokuwa TRA hivi kweli wao ndio wanajua tax collection kuliko wote? CRDB, Bandari, OR UTUMISHI, Hazina n.k walijaa Kilimanjaro sehemu nyeti zote.

Sasa huko ktk Biashara tender zote asilimia kubwa ilikuwa wao why hakuna wengine wanaojua Biashara mbona sasa the ground has been leveled wanakimbia Kariakoo lakini wakinga wapo. Ni hivi Watu hao wengi ni wapigaji watoa rushwa, wakwepa kodi, wanajua kuharibu Biashara za wengine kwa tabia zao za ukabila na ukosefu wa maadili. Sasa hivi tender zinakuwa processed kwa haki sio upendeleo.

Mlizoea dezo eti nyie ndio mnajua kutafuta pesa wengine hawa jui sababu ya ujanja ujanja . Hebu pitieni majina ya watumishi wasio na vyeti walioondolewa Serikalini nusu yao ni Watu wa huko Kilimanjaro. Mmestukiwa Ndugu zangu.

Angalieni nyuma mlipokosea mjisahihishe. Kuacha majina ya ukoo Si dawa ya mnalodhani ni tatizo. Hali mliyonayo ndio wenzenu walikuwa nayo. Sasa hakuna upendeleo. Kwa hili JPM amelikomesha kama kuna waliobaki ni wachache wenye upendeleo .

Kazana kazana kuandika na wewe utakuwa tajiri
 
Awamu hii ni zamu ya akina Mayanga Construction, Shija Civil Engineering na Masanja (T) Ltd. Acha wale nchi kwa hisani ya Sizonje.
 
Lecturer wangu mmoja aliwahi kusisitiza sana kutotumia majina yetu ktk biashara kutokana na adhari kama hizi, ukianzisha biashara/ kampuni yako kwa kutumia jina la familia inahasara zaidi kuliko faida.
 
Yaani kwa uongo huu ni sawaa kupanda mlima kinyume yume.

fact! 1:Kampuni imesajiliwa tayari sasa unabadili vipi?
2:Kuna baadhi ya document mfano bank, Id na nk nazo unabadili?
3:Huu ubaguzi umeanza lini km umefuata sheria zote na kazi yako nzuri?
Process ya kubadilisha jina la kampuni iliyokwishasajiliwa ni fupi sana. Unahitaji tu barua na company board resolution. Kwa kawaida haichukui zaidi ya wiki.
 
Kweli hizi ni stori za kijiweni kama alivyosema yaani zamani tunaita wazurulaji, katika tender application unaingia kwa jina la kampuni au biashara na kama ukibadirisha inamaana unaanza upya kuanzia tin namba. Hii ni proses ndefu na tenda ni mwaka 1 na kumbukumbu zako ndiyo zinakusaidia kupata tena sasa jamaa wa kijiwe katupa jiwe.
Wewe sasa ni mwongo!
Kama kampuni yako ilikwishasajiliwa, jkitaka kubadilisha jina, unapeleka barua na board resoluyion BRELA. Utapewa certificate mpya yenye registration namba ile ile. Na mambo mengine kama TIN inabakia ile ile. Ni process fupi sana.
 
We mleta mada, unaona hayo mazee kukutana kikaoni kabila moja kujadili maslahi kikabila ni normal hiyo? Bora hata wangejadili maendeleo ya wanakotoka.
Sishangai sana maana hata jamaa wakikaa group kupiga bia utakuta wote kabila moja.
 
Lipo tatizo kwa wachache wenye dhana zao potovu, ni vyema kuepuka majina ya kikabila katika biashara.
 
Siku za karibuni nilikuwa Dar kwenye msiba wa ndugu yangu. Kwenye msiba walikuwepo baadhi ya wazee wastaafu waliokuwa nafasi za juu serikalini, na mmoja alikuwa afisa wa ngazi ya juu UNESCO. Wote, hakuna miongoni mwao aliyekuwa anatoka mikoa ya Kaskazini. Katika mazungumzo yao, namnukuu mmojawapo:

'Sijui, lakini kipindi hiki, japo haisemwi, ila inaonekana kuna jitihada kubwa sana zinafanywa, za kuhakikisha nafasi nyingi za juu, wanawekwa Kanda ya Ziwa, sijui kama wote wanaona hivyo'.

Oh yes, that is very obvious.

Waliendelea na mengi. Kwa hiyo kwa sasa fikra za upendeleo wa kikanda/kikabila, kwa wengi, wanaona zipo wazi kuliko utawala wowote uliopita. Huenda huko nyuma haya mambo yalikuwepo lakini hayakuwa wazi kiasi hiki.

Kama watawala wana nia ya kulijenga Taifa, wasipuuze haya yanayosemwa na watu maana watu wanatoa na uthibitisho wa kitakwimu. Fikra hizi zikiendelea kujengeka kwa watu, kuziondoa kutakuwa na gharama.

Ubaguzi ni tabia. Anayebagua watu kwa misingi yoyote ile, wakati wote ubaguzi wake hauishii kwenye jambo moja.

Anayewabagua watu kwa itikadi zao, hataishia hapo tu bali atawabagua watu kwa makabila yao, kwa dini zao, kwa madhehebu yao, kwa lugha zao, kwa maeneo watokayo, kwa rangi zao, n.k.

Tupige vita ubaguzi kwaajili ya ustawi wa nchi yetu. Mbaguzi ni adui wa Taifa.
 
mbona hili linajulikana cku nyingi. hao wanaolalamika ni wale waliochelewa. kwa mfano baada ya mkulu kuwaruhusu wamachinga wengi wa wachagga wenye maduka walitengeneza machinga wao wenyewe wakawapa mizigo na kusubir hela jion. ucpambane na mtu mwenye nia mbaya na wewe cheza na akili yake tu
 
Kinachofanyika ni kwa watoto kutochua jina la tatu la ukoo bali wanachukua jina la pili au la ubatizo la baba. Hii ipo ktk baadhi ya familia Mzee akisoma gemu anafanyahivyo hasa hao wachaga utakuta eg mtoto wa Tarimo anajulikana ni tarimo lakini ktk official document tarimo haionekani. Shida sus ya mchaga haijifichi hajalishi ni wa marangu, kibosho umbu au rombo.
Hii ni mipango ya familia zaidi
 
Kama haya ni ya kweli ambayo wanafanyiwa kabila hili basi nchi yetu tayari imegeuka. Ingawa tunaweza kusema ni ya kweli au siyo ya kweli, vipo vihashiria vinavyosema ni ya kweli.

Wapo watu fulani wakubwa tu wenye makampuni yao ambao walikuwa wamekaa kama kamati fulani kujadili namna ya kukabiliana na kile walichokiita changamoto wanazokabiliana nazo katika biashara. Watu hawa ni wa kabila moja maarufu sana Tanzania linalotoka kanda ya kaskazini. Kiukweli ni maneno ambayo nimeyasikia wakiyaongea tena wanayapa mkazo kwelikweli na mbinu ili kujikwamua.

Jamaa mmoja akasema yeye ni mtu anayeomba tenda mbalimbali za kusambaza vifaa kwenye taasisi za serikali ila amekuwa akipata changamoto ya kunyimwa tenda lakini akakiri wazi kuwa kabla ya utawala wa awamu ya tano mambo hayakuwa hivi! Huyo akadiriki kusema kuwa aliamua kuanza mchakato wa kubadili jina lake la ukoo kwenye documents anazoombea tenda ili tu asikatwe kwa kigezo hicho. Anakiri wazi kuwa walau hilo limeanza kumpa uhai. Naomba ninukuu baadhi ya maneno aliyosema "Siwezi kutumia tena jina la TARIMO kwenye kuomba zabuni. Limekuwa likiwa kikwazo kwangu! Hata wanangu wote nimewaambia wabadili jina lao la ukoo kwenye mambo yao ya shule! Wasitumie kabisaa jina hilo" Mzee huyo kweli akawa anasisitiza hivyo.

Katika maongezi yao kumbe kuna mama mmoja mfanya biashara ambaye alishauriwa asiweke jina lake la asili kwenye makabrasha yake ya kuomba tenda ya mabilioni ya fedha kwenye moja ya mashirika ya serikali. Nadhani aliyemshauri ni mmoja kati ya wazee waliokuwa wakijadiliana katika mjadala huu. Mara lile jina lake likaanza kujadiliwa. Nadhani hili jina linaweza kuwa linatokea Maeneo ya Wilaya ya Moshi. Lakini katika mjadala wao wakagundua kuwa jina hili halifahamiki sana kama jina la kikabila. Mara nikaona mzee mmoja akinyanyua simu na kumpigia yule mama na katika maongezi yake akamuambia "Kwenye documents usiweke jina la ukoo la mume wako! Hilo linajulikana, tumia jina la upande wa baba yako ambalo linaonekana siyo maarufu kulitambua" Kwakweli nimeacha mjadala ukiwa hot sana na inaonekana hili kabila limeanza kukutana na adha kubwakubwa za hapa na pale katika miangaiko yao ya kutafuta riziki.

Pamoja na hayo nalisifu kwa kung'amua hilo na kuanza kutafuta mbinu za kukabiliana na hili jambo.

Hayo ndiyo niliyokutana nayo kijiweni moja ya maficho maalum ya wazee maalum ambapo nilibahatika kuingia hapo baada ya kuwa nimempeleka boss fulani kumkutanisha na mtu ila huu mjadala umechukua muda mrefu nawanajadili kwa umakini na wanaweka uthibitisho! Wengine wanasema kuwa wanapigiwa simu kutoka huko juu na watu wanaowapenda na wamekuwa wakiwapa huo ushauri wa kuondoa kabisa majina ya koo zao au kuyaandika kwa herufi moja tu pale wanapotaka kuomba zabuni mbalimbali.

Hapa ni kazi kwa kazi.Tafuta mbinu ya kupata kazi!

Hao watu ni waisrael bwana!! Wana kitu inaitwa "intellectual versatility". Achana na hii kitu kabisa!! Ukibana huku wanachomolea kungine na maisha yanaenda. Wameshindwa kuwazuia wasiende kwao mwisho wa mwaka, cha kushangaza huko Moshi kukaelemewa ujio wao! Eti mnawabana wasifanikiwe, kweli??!! Huwezi kusaidia maskini kwa kuwabana hao watu wa kaskazini, walianza zamani. Hawatakagi ujinga kabisa, ni wakati wa wengine kuiga huu utamaduni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom