Umesema kweli kuwa kinachoendelea TZ ni Mungu anajua. Naamini ulimaanisha Mungu wa Mbinguni ambaye anaona kinachotokea na kitakachotokea. Pia naamini unamwamini huyo Mungu na sio miungu. Kama ni hivyo Mungu akubariki Sana na akufunulie uone nchi yetu ilielekea kwenye neema kwa speed kubwa ambayo haijawahi kutokea toka Uhuru December 1961.
Kwa nini hiyo neema ije na chuki na visasi?
Hivi barabara au reli haiwezi kujengwa mpaka watu watumie nguvu kubwa kuwanyamazisha wengine ili hali wanaovunja SHERIA na katiba wanaonekana wazi kabisa.
Umefuatilia wanayofanya baadhi au karibu maDC wote na wakurugenzi hasa maeneo yenye wapinzani wengi.
Nikuulize swali hivi Arumeru,Hai ,Monduli ni maskini kuliko wilaya ya Mafia ,Kilosa na Wilaya karibu zote za Mikoa ya Dodoma na Singida? Sasa jiulize yanayoendelea huko ni kusaka maendeleo na kama ni kusaka maendeleo kwa nini yasifanyike kwenye wilaya na mikoa maskini sana. Kwa nini yafanyike Hai ambapo maendeleo yapo juu?
Maendeleo ya vitu hayamsaidii MTU wa kawaida kamwe ndio maana tuliwaondoa wakoloni waliokua na Uwezo wa kuifanya Afrika iwe zaidi ya ulaya mana tulihitaji maendeleo ya wananchi kwanza. Wananchi wapate ajira zinazoweza kuwapa heshima na sio utumwa, wananchi waweze kuanzisha mashirika na biashara zao kubwa kama wahindi na sio kuwa omba omba kwa watawala, wananchi waweze kulima na kupata masoko yao.
Hatukutafuta Uhuru ili kujenga mfumo wa kikoloni zaidi unaojenga chuki mana itafikia mahali watu hawatasalimiana kwa sababu ya kutendewa ukatili na ndugu zao ambayo wanalipwa mamishahara makubwa kwa kodi wanazokamuliwa wanyonge.
Vyeo vya uteuzi vimekua ni jehanamu kwa mataifa ya Afrika .
Wanateuana kwa maelfu kama rushwa kwani wenye mavyeo ya kuteuliwa wanalipwa mamilioni tofauti na watu wenye Taaluma zao.
MTU anateuliwa hana Cheti na analipwa mshahara Mara kumi ya MTU mwenye taaluma. Kwa hiyo kumfukuza mwalimu mmoja anayelipwa laki NNE na kumwacha Mteule mmoja asiye na cheti anayelipwa Mara kumi na tano zaidi ya mwalimu ni dhambi kubwa na unyonyaji mbaya kuwahi kutokea duniani.
Tulete maendeleo endelevu sio maendeleo yanayowaacha wanyonge wakiwa maskini zaidi huku watawala wakizidi kuwa mabepari kwa mamishahara makubwa na maslahi manono na wengine wakikwepa mpaka kodi.
Wakati wa A 1 nchi ilikua gizani na redio moja ikitangaza propaganda kila siku Watu wakajiona wameendela sana kumbe nchi iko nyuma sana baada ya vyombo vya habari kuwa huru A 2 ndipo watu walipobaini kuwa wananchi wa chini ni maskini sana. Ndio maana mpaka Leo familia zenye unafuu ni za watawala tangu awamu ya kwanza. Wakoloni ambayo walisoma enzi za mkoloni ndio waliogeuka na kutuwekea SHERIA zile zile za mkoloni na mpaka Leo zinaendelea kutumika kuwafanya watawala kuwa kama wamiliki wa nchi huku wananchi wakiwa kama watumwa wao.