Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Umesema kweli kuwa kinachoendelea TZ ni Mungu anajua. Naamini ulimaanisha Mungu wa Mbinguni ambaye anaona kinachotokea na kitakachotokea. Pia naamini unamwamini huyo Mungu na sio miungu. Kama ni hivyo Mungu akubariki Sana na akufunulie uone nchi yetu ilielekea kwenye neema kwa speed kubwa ambayo haijawahi kutokea toka Uhuru December 1961.
 
MASIKITIKO NA MAAFA MAKUBWA YATATOKEA JUU YAKO MLETA MADA WALAHI!
Ungetabiri hivyo sio kuja hapa na kuleta uwongo wako juu ya nchi yetu Tanzania!
NEEMA NA BARAKA JUU YA TANZANIA MILELE YOTE walahi!
 
Uzandiki wa wazi unafanyika dhidi ya wote wasiomsifia rais, vyombo vya habari vyote vinavyodhalilisha wapinzani vinafumbiwa macho, lakini vikionyesha udhaifu wowote wa serekali kinafungiwa kwa kisingizio cha uchochezi.
 
Umesema kweli kuwa kinachoendelea TZ ni Mungu anajua. Naamini ulimaanisha Mungu wa Mbinguni ambaye anaona kinachotokea na kitakachotokea. Pia naamini unamwamini huyo Mungu na sio miungu. Kama ni hivyo Mungu akubariki Sana na akufunulie uone nchi yetu ilielekea kwenye neema kwa speed kubwa ambayo haijawahi kutokea toka Uhuru December 1961.
Speed ya KUPIGA RISASI WAKOSOAJI?? SPEED YA KUZIMA UHURU WA KUJIELEZA? SPEED YA KUPOTEZA FEDHA TRION 1;6 ? SPEED YA KUPANDIKIZA CHUKI YA UKANDA? UKABILA? UPENDELEO? KUVURUGA MISINGI YA AMANI KWA KUJIFICHA NYUMA YA MWAVULI WA MAENDELEO? NIMEAMINI UZAZI WA MPANGO UNGEZINGATIWA TUSINGEKUWA NA RUBBISH POST KAMA HIZO.BY the way MKUU Hongera kwa Kuchagua UJINGA.
 
Kwa nini hiyo neema ije na chuki na visasi?
Hivi barabara au reli haiwezi kujengwa mpaka watu watumie nguvu kubwa kuwanyamazisha wengine ili hali wanaovunja SHERIA na katiba wanaonekana wazi kabisa.
Umefuatilia wanayofanya baadhi au karibu maDC wote na wakurugenzi hasa maeneo yenye wapinzani wengi.

Nikuulize swali hivi Arumeru,Hai ,Monduli ni maskini kuliko wilaya ya Mafia ,Kilosa na Wilaya karibu zote za Mikoa ya Dodoma na Singida? Sasa jiulize yanayoendelea huko ni kusaka maendeleo na kama ni kusaka maendeleo kwa nini yasifanyike kwenye wilaya na mikoa maskini sana. Kwa nini yafanyike Hai ambapo maendeleo yapo juu?
Maendeleo ya vitu hayamsaidii MTU wa kawaida kamwe ndio maana tuliwaondoa wakoloni waliokua na Uwezo wa kuifanya Afrika iwe zaidi ya ulaya mana tulihitaji maendeleo ya wananchi kwanza. Wananchi wapate ajira zinazoweza kuwapa heshima na sio utumwa, wananchi waweze kuanzisha mashirika na biashara zao kubwa kama wahindi na sio kuwa omba omba kwa watawala, wananchi waweze kulima na kupata masoko yao.
Hatukutafuta Uhuru ili kujenga mfumo wa kikoloni zaidi unaojenga chuki mana itafikia mahali watu hawatasalimiana kwa sababu ya kutendewa ukatili na ndugu zao ambayo wanalipwa mamishahara makubwa kwa kodi wanazokamuliwa wanyonge.

Vyeo vya uteuzi vimekua ni jehanamu kwa mataifa ya Afrika .
Wanateuana kwa maelfu kama rushwa kwani wenye mavyeo ya kuteuliwa wanalipwa mamilioni tofauti na watu wenye Taaluma zao.

MTU anateuliwa hana Cheti na analipwa mshahara Mara kumi ya MTU mwenye taaluma. Kwa hiyo kumfukuza mwalimu mmoja anayelipwa laki NNE na kumwacha Mteule mmoja asiye na cheti anayelipwa Mara kumi na tano zaidi ya mwalimu ni dhambi kubwa na unyonyaji mbaya kuwahi kutokea duniani.

Tulete maendeleo endelevu sio maendeleo yanayowaacha wanyonge wakiwa maskini zaidi huku watawala wakizidi kuwa mabepari kwa mamishahara makubwa na maslahi manono na wengine wakikwepa mpaka kodi.

Wakati wa A 1 nchi ilikua gizani na redio moja ikitangaza propaganda kila siku Watu wakajiona wameendela sana kumbe nchi iko nyuma sana baada ya vyombo vya habari kuwa huru A 2 ndipo watu walipobaini kuwa wananchi wa chini ni maskini sana. Ndio maana mpaka Leo familia zenye unafuu ni za watawala tangu awamu ya kwanza. Wakoloni ambayo walisoma enzi za mkoloni ndio waliogeuka na kutuwekea SHERIA zile zile za mkoloni na mpaka Leo zinaendelea kutumika kuwafanya watawala kuwa kama wamiliki wa nchi huku wananchi wakiwa kama watumwa wao.
Umeeleza vizuri sana ila tatizo ni hilo boya la kichaa jiwe liko kazini anatafuta riziki, ili aweze kupata mlo ni lazima kwanza apost chochote cha kusifia kichaajiwe
 
MASIKITIKO NA MAAFA MAKUBWA YATATOKEA JUU YAKO MLETA MADA WALAHI!
Ungetabiri hivyo sio kuja hapa na kuleta uwongo wako juu ya nchi yetu Tanzania!
NEEMA NA BARAKA JUU YA TANZANIA MILELE YOTE walahi!
Sawa
 
Ignorance: The reason for all this, we spend our time fond of unnecessary life realms aside from what constitute our lives in the better ways, then let us perish 😕😕
 
kinachoendelea nchini Mungu tu ndo anajua wapi Tanzania inaelekea kama ni ktk maziwa na asali au ktk GIZA NENE NA MATESO.
Kuna magazeti kadhaa yamefungiwa kama mawio, mwanahalisi na serikali kwa uchocheziok uchochez haufai
BUT KUNA MAGAZETI KAMATANZANITE, JAMHURI NK YANAANDIKA MAKALA AMBAZO ZIPO ZA UCHOCHEZ KWA JAMII LAKINI SERIKALI INAYANGALIA TU.
Kuna watu baadhi wanachezea amani yetu lazima tuwakemee bila kujali itikadi ya vyama, dini wala kabila.
Naona kama vile Tanzania inatoka kwenye reli na kwenda chaka.
God please bless our country Tanzania
Kichwa cha habari kizito Hakuna hoja ya msingi
 
Nasikia Mwandiga pamoja na ufundi wao wote, hawana uwezo wa kumuingiza mtu IKULU😯😯
Hawajataka tu!Soon utasikia na siunaona Zitto hata watu wasiojulikana wanamwogopa ,unaona ana kesi za ajabuajabu.Uliza Kigoma one ndio utaijua mwandiga wewe!Urais wa wapi!unajuaje hawamwongozi aliyepo?mpaka anaona u_ichaa ni sifa taratibu tutafika tu
 
Speed ya KUPIGA RISASI WAKOSOAJI?? SPEED YA KUZIMA UHURU WA KUJIELEZA? SPEED YA KUPOTEZA FEDHA TRION 1;6 ? SPEED YA KUPANDIKIZA CHUKI YA UKANDA? UKABILA? UPENDELEO? KUVURUGA MISINGI YA AMANI KWA KUJIFICHA NYUMA YA MWAVULI WA MAENDELEO? NIMEAMINI UZAZI WA MPANGO UNGEZINGATIWA TUSINGEKUWA NA RUBBISH POST KAMA HIZO.BY the way MKUU Hongera kwa Kuchagua UJINGA.

Kwa vile unamwamini Mungu pia hayo unayoandika huyo Mungu ndiye aliyekuongoza. Ila ni wazi kuwa Mungu wako sio wa Mbinguni ni mwingine ambaye anakuruhusu utunge uongo umbambike mtu na kisha umtuhumu kwa uongo uliombambikia. Usijali kuna siku utaangaziwa mwanga utamtambua Mingu wa kweli na ninaamini utajuta sana kwa hizi post zako.
 
A.alleikhum mabibi na mabwana,nisiwachoshe sana na utangulizi,kama title inavyojieleza
Nimekua nikisikia kauli za kukombolewa/kutetewa/kusaidiwa kwa mwananchi mnyonge toka mwishoni mwa mwaka 2015, nguvu inayotumika kumuanisha mnyonge anayetetewa/kusaidiwa na utawala ni kubwa kuliko uhalisia,yani hata mnyonge hajui kama anatetewa/kupatiwa unafuu wa maisha,huyu Mnyonge ni yupi?

Naona gharama za maisha zinapaa,bidhaa muhimu zikipanda bei,vifaa vya ujenzi havishikiki,wakulima wanalia na pembejeo na masoko ya mazao yao,gharama za matibabu na upatikanaji wa dawa muhimu,watumishi wanyonge mfano walimu,askari na kada zingine maisha yao sio siri,wengi wanasema wanamkumbuka Mkwere...haya na mengine mengi yananifikirisha kutaka kumfahamu huyu mnyonge...

Au kama yumo humu JF ajitokeze tumjue..
 
Huwezi elewa chochote kinachoendelea nchi hii, kutwa kucha umepakatwa, nchi ni kubwa Sana, na kunahatua njema zinatendeka, wewe endelea kupaka wanja mjini
 
Huwezi elewa chochote kinachoendelea nchi hii, kutwa kucha umepakatwa, nchi ni kubwa Sana, na kunahatua njema zinatendeka, wewe endelea kupaka wanja mjini
Kwa faida ya wanajukwaa,wewe unayeelewa tiririka basi..
 
Na mimi nina mda namtafuta. Au sijui ni mistari tu ya wazee kuonekana wema ili wabaki kwenye viti

Ila yawezekana ni wale(sisi) jamaa ambao hatujambui hoja. Hatupendi kusoma( elimu ya darasani, vitabu, majarida, na taarifa mbali mbali.)

Tutakua ni wale ambao hatuko makini kufuatilia uhalisia wa hali ya maisha na nchi.

Itakua ni wale ambao tukipewa maneno matamu. Tuna wapitisha.

Bahati mbaya ukishakua mnyonge na ukajikubali badala ya kutafuta njia ya kutoka kwenye huo unyonge utabaki tu kuwa mnyonge.

Kwa upeo wangu wakijinga huyu ndiye mnyonge.

Ila kuna wale wanaopewa hadi allowance ya vyakula vya familia zao na bei ua mtaani ni mpaka wasome taarifa za uchumi. Wao sijui nao ni "wanyonge"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom