Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Huwezi kujua utendaji wa sehemu vizuri mpaka Tatizo litokee. Pamoja na idara, polisi, jeshi, serikali ya mkoa utendaji wa hii ajali unaonyesha ni jinsi gani tumekazania mifumo kisiasa zaidi na kusahau matatizo ni watu na maisha ya Watanzania. Inaelekea wakati wabunge wakilalamika kwenye chombo kibovu walikuwa wanasikilizwa kisiasa. Lakini hata kwenye mambo mengine yanashangaza jamaa waliotoa makontena ya msaada walisema hawatatoa mpaka wapate barua ya kutokuwa na kodi mkuu wa mkoa akatuma huko Washington state wakampa vitu serikali hiyo hiyo inapiga vitu mnada. Tatizo ni mifumo kama kweli mkuu wa mkoa alikuwa hajui utaratibu wa serikali je mtu wa kawaida atajuaje. Lakini pamoja na yote haya watoto bado wanakaa chini wengi tu. Sasa tunatatizo gani yaani hata ukiangalia vizuri vitu vinavyo sifiwa havifanywi na serikali ni miradi ambayo inafanywa na private companies kama reli, barabara na hata majengo hivi sio vitu vinavyofanywa na serikali ni contracts. Ni vigumu kuona vitu ambavyo serikali yenyewe inafanya vizuri. Ni wakati wakuangalia mifumo yetu vilevile jamani Technology ya sasa watoto hawatakiwa kukaa chini, watu kufa au migogoro ya ardhi wakati kuna GPS🤔. Kuna watu wanakazania mazoea na utaratibu ambao haufanyi kazi.
Baada ya chama chetu tulichokiamini Sana kugeuka na kuwa chama cha wachumia tumbo sasa hakiwezi kuzalisha tena state individuals or states man wa kuweza kufanya hivyo ambavyo havionekani kwa macho. Kinazalisha politicians, wanasiasa uchwara, wachumia tumbo ambao kila saa wanafikiria uchaguzi,mwisho wa siku wanaishia kufanya vitu vinavyoonekana ili kujustfy uwepo wao, Kwa kifupi ccm ni janga la nchi yetu kwa sasa kuliko umaskini,ujinga na ukimwi
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Kama hujui uendako huwezi kupotea
 
Yamanifika shingoni mwenzenu nimeshindwa kuvumilia. Hivi tunalipeleka wapi taifa letu. Sasa vijana wengi ambao nilitegemea wawe nguvukazi ya taifa wakifanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Sasa wanaamka asubuhi na mapema kuwahi kwenye mitandao na mashine za kubet- Kucheza kamali. Jamani tunatengeneza kizazi kijacho cha wacheza kamali watakaotegemea bahati na sio bidii na weledi wao kuzaalisha (they wont be productive)Kamali imekatazwa na vitabu vyote vya dini. Mh. Raisi hili hujaliona?????. Hata kama wanalipa kodi, huwezi halaliisha haramu kwa sababu ya pesa. Hivi huyu Mungu tunayemuomba atatusikiliza kweli huku tunaenda kinyume na makatazo yake. NCHI HII TUTAIFANYA KUWA YA MATAPELI WATUPU TUSIPOJIREKEBISHA. Eee mungu tusaidie
 
kwakweli mm suala la mamichezo hayo nahis kama sodoma na gomora...yan nahis umombasa mombasa hv... kwakweli nakereka!unayakuta yameshika makaratasi ova yanacheki matokeo ya form 6!..majanaume na siku hizi na wamama nao arghhh
 
Mkishapata vihela mnaanza kuwaponda wenzenu eti hawafanyi kazi wanashinda kwenye mitandao.

Kila mmoja ataokota ridhiki yake pale anapoona ipo.

Acheni hizo.
 
Ikifika J.pili una wakuta kanisani eti na wao wanakwenda kufanya Ibada ....

Maisha bila unafiki ni sawa na gari lisilo na mafuta wallahi...

lakini serikali ya nchi hii imeshajitabanaisha kwamba haina dini".. kwa hiyo tusitarajie kuwa wataiona kamari ni kitendo cha dhambi"... kwa sababu wapo nje ya imani ya hizo dini
 
Binafsi hadi 2025 naiona tanzania yenye madini, milima, mito na mabonde ikiitwa nchi yenye uchumi wa kati kinadharia lakini ki uhalisia hakuna uhalisia unaohubiriwa.
 
Naiona "downfall" ya kutisha kiuchumi kwenye nchi yangu ya Tanzania.......
 
Binafsi hadi 2025 naiona tanzania yenye madini, milima, mito na mabonde ikiitwa nchi yenye uchumi wa kati kinadharia lakini ki uhalisia hakuna uhalisia unaohubiriwa.
kutekana kutakuwa nje nje mara 5 ya hivi sasa ... kuhusu uchumi tujiandae kuporomoka kwa shilingi Yetu mkate wa 1k utakuwa unauzwa 5ks
 
Naiona nchi yenye miundo Mbinu mizuri sana from Ocean zone to lake zone lakini uchumi ukiwa dhoofu ilhali. Wachina watajazana kila mahali mana watakua wanajitahidi kuvaa mashati ya rangi ya majani kudumisha umoja wa nchi za kijamaa kama China ambayo kiuhalisia ni nchi ya kibepari na ya kinyonyaji kwa sasa. Ujamaa umebaki kama neno tu na tamaduni za kichina laikini ujamaa haupo.
Ujamaa wa kweli uko nchi za Ulaya ya Kaskazini.
 
"Ila tuwe wakweli Magufuli kaua uchumi"

2025 ingawa mimi naamini hatokuwepo kama Rais

Akiwepo vijana hasa wasomi watakuwa hoi bini taabani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom