Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
BASI KAONGOZE NA WEWE, tulio nje nje box (white house) mengi hatujui ila kukosoa tu ndo tunachokijua.
Kaa ukijua uongozi ni dhamana na vita ni mapambano.
Cku ukijua ikulu si mahali pa kitoto nadhani utajihidhuru mapema sana kama ndo wewe,
JPM hafurahishwi na hili, hii ni vita kali sana baada ya kutangaza vita ya kiuchumi ndgu, tutachekwavibay sana endapo atalegeza katikati ya uwanja wa medani.

kiusalama kuna vitu vingi hatuvijui.Rais pambana hadi mwisho, mambo mengine ni nyeiti kuyasema hadharani hasa ya kiusalama wa nchi iliyo vitani
Ni kweli mambo mengine ni ñyeti sana utaanzaje kuyasema wakati wewe ndio muuaji na mtekaji namba moja??
 
BASI KAONGOZE NA WEWE, tulio nje nje box (white house) mengi hatujui ila kukosoa tu ndo tunachokijua.
Kaa ukijua uongozi ni dhamana na vita ni mapambano.
Cku ukijua ikulu si mahali pa kitoto nadhani utajihidhuru mapema sana kama ndo wewe,
JPM hafurahishwi na hili, hii ni vita kali sana baada ya kutangaza vita ya kiuchumi ndgu, tutachekwavibay sana endapo atalegeza katikati ya uwanja wa medani.

kiusalama kuna vitu vingi hatuvijui.Rais pambana hadi mwisho, mambo mengine ni nyeiti kuyasema hadharani hasa ya kiusalama wa nchi iliyo vitani
Muda wangu wa kuongoza upo jikoni,
Well said kiusalama mambo mengi hatujui,unadhani Tanzania pekee ipo kwenye tishio la namna hii na je unadhani ndio nchi ya kwanza kuwa na matishio ya namna hii kama jibu lako ni hapana kwamba zimewahi kuwako nchi zilizotishiwa lakini hatukuona hatua au matukio kama haya yakitokea kudhibiti hali hii kama ndio je hamuoni njia nyingine ya kudhibiti hali ya mambo na kujifunza kwa hao wengine namna ya kudhibiti bila kuchafua sura ya nchi katika jumuiya zingine za kimataifa na kuwatia hofu wananchi walio katika utandawazi kujua kwamba wao hawako salama wala nchi yao haiko salama?

Kwa maelezo yako ya hapo juu unakubali kwamba matukio haya yote yanaendeshwa na serikali kwaajili ya kudhibiti hali ya mambo au tishio la usalama kwa rais!

Je kwa nini sasa? Kwa sababu ya kujifungia chumbani nakutotaka kwenda sebuleni kutazama hali huko ikoje!,ni kwa sababu ya kutokuwa na uhakika kwamba ingetokea siku angekuwa rais (hakujiandaa).....

Kwanini sasa? Wenzake walliwezaje kudhibiti kimya kimya kuliko yeye?

Pesa hana, uwezo hana au tatizo liko wapi?

Uongozi ni chain lakini chain ambayo haina cracks, chain ambayo kila mtu anaumuhimu wake.

Katika mnyororo wa baiskeli kila kipande kinatoa support yake ili kuendesha gurudumu la baiskeli vivyo hivyo katika leadership.

Kipande kimoja kikikatika chain handler itazunguka free bila ugumu wowote na kuleta effect katika gurudumu.

Kikikatika hukiachi unakibadilisha,

Ukihang na watu wa wabaya nawe utakuwa mbaya rafiki.....

Ukiendelea kuzungusha mnyororo uliokatika katika baiskeli utaanguka tu balance itatoka wapi.

NATAKA KUSEMA kuna watu rais anawakumbatia hawana tactics plan za namna ya kudhibiti mambo kulingana na hali ya sasa ilivo (kitekinolojia, utandawazi )

Sio muda wa ujanja ujanja au kutumia nguvu nyingi rather than AKILI KUBWA.

Tatizo siku zote linaanzia kwako wewe mwenyewe huwezi rogwa bila sababu.

Ikitokea ujue hauna kinga hiyo ndio sababu yenyewe au kutokana na wivu basi ujue wewe ndio sababu kwani nyota yako chafu inagiza. ....

SABABU NI YEYE KATIKA KUSOLVE MAMBO KATIKA NJIA NZURI NA ILIYO SAHIHI YENYEWE ITALETA MATOKEO HARAKA BILA KUACHA CHEMBECHEMBE ZA MAKOSA,MADHARA NA MASHAKA MIONGONI MWA WENGINE.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Eventually hata ccm wenye akili za kubabia (read slow learners) wameanza kujiuliza hili swali.
 
Nadhani extreme left kiasi kumiliki baskeli hadi ujadiliwe na kamati ya chama.
 
Matajiri wataishi kama mashetani, maneono huumba,
Wanasiasa watu waajabu sana.

Ukitekeleza Sera nzuri za uchumi, biashara uwekezaji lazima utazalisha "matajiri"
Wakitokea matajiri unasema ni wezi.

Ukiboresha mfumo wa elimu watatokea watu wadadisi wabishi wajenga hoja na wanaoojii kila kitu. Alafu utasema siyo wazalendo.

Ukiboresha siasa yademokrasia utazalisha wapinzani. Alafu unaanza Kuwaita "wahaini"
Roho wa kimaskini na hofu kamtawala bwana Jiwe
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
Majibu ya kizombie!
 
Muda wangu wa kuongoza upo jikoni,
Well said kiusalama mambo mengi hatujui,unadhani Tanzania pekee ipo kwenye tishio la namna hii na je unadhani ndio nchi ya kwanza kuwa na matishio ya namna hii kama jibu lako ni hapana kwamba zimewahi kuwako nchi zilizotishiwa lakini hatukuona hatua au matukio kama haya yakitokea kudhibiti hali hii kama ndio je hamuoni njia nyingine ya kudhibiti hali ya mambo na kujifunza kwa hao wengine namna ya kudhibiti bila kuchafua sura ya nchi katika jumuiya zingine za kimataifa na kuwatia hofu wananchi walio katika utandawazi kujua kwamba wao hawako salama wala nchi yao haiko salama?

Kwa maelezo yako ya hapo juu unakubali kwamba matukio haya yote yanaendeshwa na serikali kwaajili ya kudhibiti hali ya mambo au tishio la usalama kwa rais!

Je kwa nini sasa? Kwa sababu ya kujifungia chumbani nakutotaka kwenda sebuleni kutazama hali huko ikoje!,ni kwa sababu ya kutokuwa na uhakika kwamba ingetokea siku angekuwa rais (hakujiandaa).....

Kwanini sasa? Wenzake walliwezaje kudhibiti kimya kimya kuliko yeye?

Pesa hana, uwezo hana au tatizo liko wapi?

Uongozi ni chain lakini chain ambayo haina cracks, chain ambayo kila mtu anaumuhimu wake.

Katika mnyororo wa baiskeli kila kipande kinatoa support yake ili kuendesha gurudumu la baiskeli vivyo hivyo katika leadership.

Kipande kimoja kikikatika chain handler itazunguka free bila ugumu wowote na kuleta effect katika gurudumu.

Kikikatika hukiachi unakibadilisha,

Ukihang na watu wa wabaya nawe utakuwa mbaya rafiki.....

Ukiendelea kuzungusha mnyororo uliokatika katika baiskeli utaanguka tu balance itatoka wapi.

NATAKA KUSEMA kuna watu rais anawakumbatia hawana tactics plan za namna ya kudhibiti mambo kulingana na hali ya sasa ilivo (kitekinolojia, utandawazi )

Sio muda wa ujanja ujanja au kutumia nguvu nyingi rather than AKILI KUBWA.

Tatizo siku zote linaanzia kwako wewe mwenyewe huwezi rogwa bila sababu.

Ikitokea ujue hauna kinga hiyo ndio sababu yenyewe au kutokana na wivu basi ujue wewe ndio sababu kwani nyota yako chafu inagiza. ....

SABABU NI YEYE KATIKA KUSOLVE MAMBO KATIKA NJIA NZURI NA ILIYO SAHIHI YENYEWE ITALETA MATOKEO HARAKA BILA KUACHA CHEMBECHEMBE ZA MAKOSA,MADHARA NA MASHAKA MIONGONI MWA WENGINE.

ASANTE MKUU, kumbuka uzoefu wa haya mambo hutokana na chngamoto nyingi na ndipo ukomavu wa kung'amua mambo.

Sisi bado wachanga sana kiinteligence sababu ya kukosa changamoto ngumu kama hiz, bado tunajifunza, hope vyombo vyetu vinajifunza kupitia haya.
Uchumi ni vitakali duniani na inahitaji ukomavu sana kiinteligence,sasa ndo kama hivi inavotokea na hata RAIS hawezi kukurupka kizembe kuyasemea hadharani.
MIMI sitakikuamini moja kwa moja eti RAIS anampango rukuki wa kuiangamiza nchi hii hata kidogo na tuache lawama za kumkatisha tamaa juu vitendo huvi kumnyoshea vidole kila mara, anaumiza kichwa pia na yeye nini afanye kudhibiti haya matukio.
 
Jitu badala ya kwenda huko ulimwenguni kusaka fursa, limejifungua ikulu na kina Bashite kuratibu UTEKAJI, MATESO ya wa watu wasio na HATIA
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
Mleteni Mo Kwanza, hayo mengine ni kelele tu na tumeyazoea siku hizi.
 
Jitu badala ya kwenda huko ulimwenguni kusaka fursa, limejifungua ikulu na kina Bashite kuratibu UTEKAJI, MATESO ya wa watu wasio na HATIA

WEWE mnafiki kweli, JK alisafirienzi zake mkamkosoa vikali eti anaitwa kusaini kisirisiri, leo hii asiye safiri kwa manufaa ya uzazi wa kiuno chako amekuwa mratibu utekaji. duh TANZANIA hatuna la maana kabisa kiakili, ANGALIA wanavyomkosoa wakenya Uhuru KENYATTA misafari yake ughaibuni na madhara ya safari zake kwa taifa. Taifa linanuka madeni kibao sababu ya TAMAA ya kuona vya wenzao huko ingali nchi yake haina uwezo wa kufanya yote hayo anayoyaona UGHAIBUNI,

SAFARI ZA NJE KWA VIONGOZI WAKIAFRIKA NI CHANZO CHA MADENI MAKUBWA SABABU YA TAMAA KUPENDEZESHWA KWAO.
 
Hakika anakazi ngumu ila tatizo lake kubwa yupo idle, mkoloni mno (ni kama hashauriki hasikii kitu )

Hakuna suala la nchi changa...
Unapotaka kujenga uchumi lazima kipaumbele uweke katika namna ya kuulinda uchumi aidha kijeshi, kiintellijinsia au kisera.

HEBU SOMA NA ELEWA KIPANDE HIKI KUHUSU KUJITEGEMEA NA KAFANYA JITIHADA KWA USHUPAVU.

Siasa yetu iwekwe juu ya msingi gani?
Inatakiwa iwekwe juu ya msingi wa nguvu zetu wenyewe, na hiyo ina maana ya kujitegemea wenyewe. Hatuko peke yetu; nchi zote na watu wote wa dunia nzima wanaopinga ubeberu ni marafiki zetu. Hata hivyo, tunatilia mkazo wa kujitegemea wenyewe. Kwa kuzitegemea nguvu tunazozikusanya sisi wenyewe, tunaweza kuwashinda wapinga maendeleo wote wa kitanzaniana wa kigeni.

Sisi tunatetea kuzitegemea wenyewe. Tunatumainia kupata msaada wa nchi za nje lakini hatuwezi kuutegemea msaada huo; tunategemea juhudi zetu wenyewe, nguvu za busara za jeshi lote na watu wote.

Kupata ushindi wa nchi nzima ni hatua ya kwanza tu katika mwendo mrefu wa li elfu kumi. .......Mapinduzi Tanzania ni makubwa, lakini njia ya baada ya Mapinduzi itakuwa ndefu zaidi. Jambo hili lazima sasa liwekwe wazi katika chama. Makomredi lazima wasidiwe kuendelea kuwa wanyenyekevu, wenye hadhari na kujiepusha na majivuno na papara katika mtindo wao wa kufanya kazi. Makomredi lazima wasaidiwe kuendelea na mtindo wa kufanya jitihada kwa ushupavu sio mabavu.

Lazima tuyaondoshe kwa ukamilifu miongoni mwa makada wetu mawazo yote ya *kupata ushindi kwa urahisi kwa kutegemea bahati nzuri, bila ya mapigano magumu na makali, bila kutoa jasho na damu wala kuichafua sura ya nchi.

Inataka tufanye uenezi habari kwa mfululizo miongoni mwa umma juu ya ukweli wa maendeleo ya dunia na mustakabali mzuri ulio mbele ili wajenge imani ya ushindi wa haki. Kwa wakati huo huo, lazima tuwaambie umma na tuwaambie makomredi wetu kwamba patakuwepo mazonge mengi kwenye njia yetu. Bado vipo vingi ni shida nyingi kwenye njia ya Mapinduzi. Mkutano mkuu wa chama lazima ufikirie kuwa kutakuwa na shida nyingi, kwani tunaona bora kufikiria shida nyingi zaidi kuliko kidogo.
Baadhi ya makomredi hawapendelei kufikiria sana shida. Lakini shida ni mambo yaliopo; lazima tuzitambue shida nyingi kama zilizopo sasa na tusifuate "siasa ya kutotambua".Lazima tuzitambue shida, tuzichambue na tupambane nazo. Hakuna njia zilizonyooka katika dunia; lazima tujitayarishe kufuata njia amabayo ina mizunguko na mapindo na tusijaribu kupata vitu kwa urahisi. Isiwazwe kwamba mnamo asubuhi moja nzuri wapinga maendeleo na vijibwa vyao vyote watapiga magoti kwa hiari yao. Kwa ufupi, mustakabali ni mzuri, na njia ina mazonge mengi. Bado ziko shida nyingi mbele yetu na tusizipuuze. Kwa kuungana na umma mzima katika juhudi ya pamoja, hakika tunaweza kuzishinda shida zote na kupata ushindi wa haki.

*Mtu yeyote anayeona upande mzuri tu lakini haoni upande wa shida basi mtu huyo hawezi kupigana vyema katika kutimiliza kazi za chama na nchi.*

Utajiri wa jamii unaletwa na wafanyakazi, wakulima na wataalamu wafanyao kazi. Ikiwa watachukua maisha yao katika mikono yao wenyewe, wakafuata msimamo wa kimarx-lenin na kuchukulia bidii katika kuyatanzua matatizo badala ya kuyakwepa na kutimia nguvu, hapa to hapatokuwa na shida yoyote katika dunia ambayo hawataweza kuishinda.

Makomredi katika chama chote lazima wazizingatie vyema shida zote na kujiweka tayari kuzishinda kwa moyo usiovunjika na kwa njia ya mpango. Nguvu za kipinga maendeleo zina shida zao na sisi tuna zetu. .Lakini shida za nguvu za kipinga maendeleo haziwezi kushindwa kwa sababu hizo ni nguvu zinazokaribia kifo na hazina mwisho mwema. Shida zetu zinaweza kushindwa kwa sababu sisi ni nguvu mpya ambazo zinachomoza na zina mustakabali mzuri.

Katika nyakati za shida, sisi makomredi tusisahau mafanikio yetu, lazima tuuone mustakabali mzuri ulliombele yetu na tupige moyo konde.

Mambo mapya siku zote lazima yakutane na shida na vipingamizi wakati yanapokua. Ni ndoto tu kuwaza kwamba jihadi ya usoshalisti itafanikiwa kwa urahisi katika hali shwari, pasipo na shida na vipingamizi au bila ya kutumia jitihada kubwa.

Katika nyakati fulani za mapigano ya kimapinduzi, shida zinakuwa zimezidi hali nzuri na kuwa ndio upande wa nguvu wa hitilafu, na hali nzuri kuwa ndio upande dhaifu. Lakini wana -mapinduzi kwa jitihada zao wanaweza kuzishinda shida hizo hatua baada ya hatua na kuleta hali mpya ya mwafaka bila kutumia nguvu na mabavu; kwa hivyo hali ya shida inaondoka kuipisha ile ya mwafaka.

Nini maana ya kazi? Hapa kazi tu? Kazi ni mapigano. Popote pale penye shida na matatizo, inatuwajibikia kwenda kuyatanzua kwa njia iliyosalama isiyoumiza wengine yenye kutenda haki na usawa miongoni mwa umma. Tunakwenda kufanywa kazi na kupigana ili tuzishinde shida hizo. Komredi mzuri ni yule mwenye hamu kubwa ya kwenda pale penye shida kubwa zaidi.

Wa salaam,
Joselela.

Back
Top Bottom