Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Atoke kitini kwa hiari yake!
Ama la sivyo atakiona cha mtema kuni!! Tutamshtaki kwa kocha mchezaji "kuruona"
 
Mkuu umeandika kitu cha Maana Sana achana na wanao kukejeri
Na sio hapo tuu, Huu mfumo uliopo Wala haufai. Mfumo unampa mamlaka makumbwa Sana na haya ndio Matokeo yake

I'm on that good kush and alcohol
 
2.jpg


sio mimi ni KP
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Jf Great Thinker

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother/sister kwani si ni Rais ambaye ameshushwa na Mungu au? Rais wa wanyonge leo mnasema hammtaki?
 
Hilo hata sio la kushangaa ndio utajua akili za watazania vizuri,pamoja na madudu yote haya ila nakuambia huyu jamaa uchaguzi wa mwaka huu atapita kwa zaidi ya asilimia 80
Sio atashinda, Ila wataiba kura.ccm Mara ya mwisho kushinda uchaguzi ilikuwa 2005. Kuanzia hapo ni mwendo wa kuiba kura tu
 
Muda mwingine unaweza kuonyesha uwerevu lakini kupitia uwerevu wako ujinga wako pia ukaonekana, hivi Dkt Magufuli tangu aingie madarakani alikua anaenda na bajeti aliyoiandaa au aloandaa Kikwete? Tabia za namna hii haitusaidii sisi kama watanzania, hata kama aumpendi jitahidi kupima kwa haki, nafikiri unafuatilia bunge la bajeti na kilichomo unakiona hapo ndo tuanzie, nchi haiendeshwi wewe unavyotaka bali Rais anavyoona inafaa muda wa kupima anafanikiwa au la bado aujafika kupitia bajeti hii tutaweza kupima ni kwa kiasi gani Rais anafanikiwa lakini hii tabia ya kumkatisha tamaa Rais haifai ni tabia za watu wenye husuda na zaidi wamejaliwa wanawake kuwa nazo nchi ikiyumba sio yeye Rais atakayeteseka bali ni sisi wananchi, ni jukumu letu kukosoa pale palikosewa na kuonyesha njia sahihi ya kupita lakini kukosoa tu bila kuonyesha nini kilitakiwa kifanyike hiyo ni tabia ya kike
Kwa huyu jiwe tumepata hasara kubwa sana Kama taifa . tunaelekea shimoni
 
Hata kwenye hili janga la Corona, kuna watu wanaona kama tumepotea...

Mkuu TumainiEl, hatukuchagua malaika, tumemchagua binadamu, hivyo can make mistakes kama human beings wengine wote ndio maana tumemuwekea wasaidizi wa kumsaidia ikiwemo kumshauri, hawa wasaidizi ndio hawamsaidii ipasavyo!.

Nasisitiza hata kwenye janga hili la Corona, rais Magufuli asaidiwe sana na wasaidizi wake. Kila rais atakachoongea kama kina utata wasaidizi wake wajitokeze kuutatua utata wake.

Mfano vurus ana life span, baada ya muda fulani kama hajapata medium ya kuingia na kufanya mutation hawezi ku survive,
Rais Magufuli kasema kuna uwezekano barakoa zimetiwa virusi, wataalamu wajitokeze kufafanua.

Rais Magufuli ameponda Fumigation ya Makonda,
Hili lifafanuliwe.

Rais Magufuli ameshauri wananchi wajifukize, lifafanuliwe,

Rais Magufuli ameruhusu wananchi watumie barakoa za kujishonea, wataalamu walipaswa kujitokeza kesho yake kutoa muongozo hizo barakoa ziwekewe linings gani ndani ili zikidhi viwango etc.

Wasaidizi wa rais, hata kwenye hili la Corona, msaidieni rais Magufuli, msimuachie pekee yake.
P
Kalala mbele mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom