Ni lazima Watanzania wamkane shetani na nguvu zake zote, ushawishi wake wote na maovu yake yote. Hapo ndipo ndoto zao za matumaini zitafufuka tena. Ni lazima wapiga kura wafanye uamuzi sahihi ktk sanduku la kura ifikapo tarehe 28-10-2020.
Kwa maana jamaa anaonyesha wazi kabisa, kama akipata tena fursa kwa kuongoza tena kwa awamu ya pili bado anatamani kununua madege, meli na kuwekeza zaidi ktk miradi mikubwa huku maendeleo ya watu hayapo akilini mwake. Hakika vijana, wazazi wenu waliopo ktk ajira za utumishi wa umma, na babu na bibi zenu wastaafu ni makundi yasiyogusa vipaumbele vyake kabisa.
Ni lazima wananchi wachague kile kilichokuwa bora kwao. Hii ni kwa ajili ya mustakabali wa Tanzania iliyokuwa bora kwao.