Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ninaamini kabisa huyu Magufuli alikuwa pandikizi wa nchi jirani aliyepewa mission ya kuiharibu Tanzania. Na inasemwa alijaza sana watu wake wa Burundi na Rwanda kwenye system huko!
Kagame pro huyo na ndio maana kagame alianza chokochoko za kufungiana mipaka na Uganda kitu ambacho kwa sasa hakitakuwepo tena
 
Ili Prof Assad na wengine wote wanaotaka kuichafua oil chafu wanatakiwa wafanye kinyume na Magufuli kama
"NAAAM....!

Miradi yake mingine inaleta foleni na mingine hasara? Ni rahisi tu, kwa nini tuendelee na Ma-foleni na Ma-hasara? ...Nashauri Vunjeni Madaraja na Flyovers zote, Ng'oeni reli zote especilly SGR, uzeni Ndege zote na vivuko vyote nchini, Uza Meli zote Mpya zilizozinduliwa, kule Ziwa nyasa, simamisheni Ujenzi wa Bwawa la umeme, Gaweni Migodi yote, Binafsisheni Milima, Maziwa na Mbuga.

Bomoa Bandari zote zilizoboreshwa ikiwemo Mtwara, Tanga na Dar, Jengeni moja ya Wachina kwa mkataba wa miaka 100...rudisheni Ada shuleni tukuze uchumi, Wapeni Matajiri Exemptions za kodi, Ruhusuni Makinikia kwenda nje, Vunjeni Masoko mapya ya Madini mikoani, ...Charaza Bakora Machinga mjini, Mwaga wali wa Mama Ntilie.

Vunja vyama vya wakulima na utaratibu wa stakabadhi ghalani, Ruhusuni Uhuru wa Mashoga, Mateja kwa wingi mtaani, madawa ya kulevya n.k....pia Msisahau kuifunga ile Mahakama ya Mafisadi,....kwa uchache tu Hakika hapo sasa pengine Tanzania itakuwa kama ULAYA, Tanzania ya Asali na Maziwa!.

Vunjeni makao makuu Dodoma mrudishe serikali Dar.

Hapo sasa mtakuwa mmemkomoa Magufuli na watoto wake watashinda njaa ili anyooke kabisa.



Nawasilisha
Unateseka sana mkuu. Mbona vingi ulivyoorodhesha muasisi ni JK? Vingine ni sera ya nchi tangu kuanzishwa kwake?
 
Nchi hii haikuwai na haitakuja kupata kiongozi mshenzi na fedhuli Kama Magufuli. Kati ya sehemu ambayo nitawalaumu milele CCM na TISS yao ni hapa , iweje walazimishe watanzania tuongozwe na mtu mshenzi Kama yule??
Kama kuna kipindi cha uongozi TISS walineemeka, ni utawala wa pombe. Wakuu wa wilaya karibu wote, wakurugenzi, wakuu wa mikoa mpaka wakuu wa idara za serikali na vyombo vya usalama ndo walichukua hao.
Zamani tuliambiwa wabeba makopo na vichaa ndo walikuwa TISS kipindi cha mchonga, zamu hii walikuwa watana shati tu.
 
Ukweli hakuwa mstaarabu kuanzi kwao Unawezajd kupasua kwa shoka jeneza alilo nunua dada yako kisa tu mwanamke
Wana Chato wanalijuwa hili
Alikuwa kiumbe hatari sana!!
Elezea vizuri tukio Hilo,weka nyama za kutosha,weka limao,tangawizi,vitunguu na nyanya.
 
Hoja dhaifu sana !
Mwenzako kaleta hoja kwa upana zaidi hata Kama ni dhaifu,
Hebu nawewe Sasa tuletee hoja zako zenye mashiko zilizojazwa nyama Kama alivyofanya mwenzako, otherwise wewe ndo utakuwa dhaifu wa Ubongo.
 
Ndio naiona hekima ya kukatazana kumsema marehemu,kwa sababu kinachoendelea ni sawa na kusikiliza kesi upande mmoja tu na kisha kutoa hukumu.
Yeye alipovamia maduka yetu ya kubadilishia fedha mbona hakutupa nafasi ya kusikiliza pande zote!!??
Katupora hela zetu na kusababisha turudi nyuma miaka kadhaa.
 
Yeye alipovamia maduka yetu ya kubadilishia fedha mbona hakutupa nafasi ya kusikiliza pande zote!!??
Katupora hela zetu na kusababisha turudi nyuma miaka kadhaa.
Mimi sizungumzii hayo mkuu jaribu kunielewa,sipo hapa kumtetea marehemu au kuzuia watu kumzungumzia tu marehemu bali nachosema ni kutoa tuhuma kwa mtu ambaye amefariki hivyo hatuwezi kusikiliza upande wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom