Anayejua Wasifu wa Ramadhan Kingai (ACP) atusaidie

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
RPC Kinondoni leo ni shahidi aliyesimama Mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi ya Mbowe na wenzake ya Ugaidi.

Katika kufuatilia cross examination kiongozi huyu wa Jeshi la Polisi amejichanganya sana na hivyo kushindwa kusimama kwa nafasi ya afisa mkubwa kwenye Jeshi na mchunguzi.

Yawezekana tatizo ni elimu au tatizo ni aina ya kesi ndiyo sababu ya yeye kubanwa mahakamani hadi wakati mwingine kupata gaidance ya Mahakama.

Ili tumfahamu vizuri kama ambavyo nchi nyingine ufanya, tunaomba tupate CV yake kuona kama kwenye criminal investigation huyu anaelewa au Basi kawekwa tu.

Lakini pia kesi hii ameanza kuichunguza akiwa Arusha wakati mazingira ya kesi yapo Kilimanjaro na Dar es Salaam, je huyu ndiye alionekana nafuu Kati ya ma RCO nchi nzima au kwanini yeye na si RCO Kilimanjaro Wala Dar?
 
Wanaosema TP ni taasisi #1 inayotakiwa kufumuliwa kuanzia juu mpaka chini na kuundwa upya wana hoja nzito sana. Hamna kitu mle zaidi ya kujificha kwenye matumizi ya nguvu yaliyoptiliza ku-cover udhaifu mkubwa unaoliandama.
 
Polisi ajirieni watu kwa elimu na kuwapandisha vyeo kwa elimu elimu na weledi sio Udini tu ona sasa aibu hii mtu ana mivyeo kibao hata Hati ya mashtaka hakusoma inaasema nini msisikilize wanasiasa
RPC Kingai (ACP) hana shida. Tatizo ni mfumo wa kihuni anaoutumikia hata malaika angechemka tu! Katiba bora itaondoa matatizo kama haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…