Anayeshtakiwa kumuua Mkewe adai haogopi Kunyongwa

"Ninataka kesi hii iwe fundisho kwa watu wengi, kwa sababu tulifanya uzembe mkubwa sana sisi wanandoa na jamii pia ilifanya uzembe hadi mauaji yakatokea, alidai Luwonga.
Kwani wangetengana ingekuwaje? Haya ni matokeo ya kung'ang'ana na ndoa wakati dau limeshakwenda mrama.

Piga talaka uende na shughuli zako na yeye aende na zake. Jina lake linaonyesha ni muislamu au ameritadi kumfuata mwanamke?

Samahani lakini huyo mwanaume kukaa mpaka akavutwa hayo madude au kupigwa mbele ya mama na yeye bado amebaki anachekelea tu bila kuchukua hatua, mbona naona haina muelekeo?
 
Apimwe afya ya akili kwanza
 
daah si angekubali tu waachane wauze nyumba kila mtu afe kivyake...!!
 
Ndoa ya shangazi yako uliivunjaje? I mean ulisimama Kama nani katika hiyo issue?[emoji848]
Nilikua km mwana familia, na nilijitokezaa kuupasua ukweli, na kuondoa unafikii ulio kuwa unaendelea kulindwaa.

Couz huyo shangazi nilimchokonoaa ndo akaniambia ukweli wote, miaka 11 migogoro haiishi. Ila wanaishi Pa1, kumbe kila mtu analala kwake, kila mtu na mipango yake, ila huku nje wana pretend wako sawa, hiyo ni ndoa au uchuro? Shangazi akitaka kuachika, baba, bibi na ndugu zake wengne wana muambia avumilie tyuuh, jamii itamuonajee? Itamchukuliajee?. Huku mtu anateketea ndani kwa ndani.

Nkamuambia shangazi lianzishee afu mie nalimalizaa.na niliwachambaa sio wazazi wala ndugu zake wengine hawanisahau kamwee
 
Kuna umuhimu wa sheria za ndoa, hasa kipengele cha kutalikiana kibadilishwe. Wanawake wengi wameuliwa sababu ya ndoa.

Ndoa za siku hizi nazo pasua kichwa. Fikiria hawa wanandoa ni vijana. Walikuwa na maisha yao tayari wanajimudu. Sijui mdudu gani aliwaingia.
 
Ila namsifu jamaa kwa alichoeleza mbele ya mahakama. Naomi alikuwa msumbufu sana hata majirani zake Kigamboni wanakili hilo wazo baada ya hilo sekeseke kutokea 2019.
Sasa si umeona kumbe hadi majirani wanafahamu kila kitu.

Jamaa amekuwa honestly ameamua kuipatia uhuru nafsi yake kwa kusema ukweli ambao ulikuwa kwenye kifua chake.

Na mahakama inatambua kuua bila kukusudia ni bahati mbaya hivyo sidhani kama kutakuwa na kifungo kikubwa.
 
Na wanaume wakienda kushitaki wasikilizwe pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…