Anayeshupaza shingo yake mwisho wake? Je, inawahusu watawala wa sasa hapa Tanzania?

Anayeshupaza shingo yake mwisho wake? Je, inawahusu watawala wa sasa hapa Tanzania?

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Kelele zilikuwa nyingi kumkomesha Polepole kuropoka ropoka kupitia shule yake. Akashupaza shingo yake na kutoa shule kubwa Zaidi yenye vijembe kibao ndani yake.

Mwishowe tuliona kabisa wakaja TCRA wakakata shingo yake! Mbaya Zaidi amepelekwa na kwenye LiCHAMA lake pengine na bungeni anaweza akakatwa na akizubaa akaendelea kushupaza shingo Zaidi anaweza akang'olewa uancahama wa CCM kama alivyomfanyia Membe kwa maneno yake mwenyewe na pengine maandishi yake.

Swali linakuja, je watawala hawa walivyoshupalia kesi isiyo ya mashiko ya Mbowe nao watakatika shingo zao "kaaaaaaa"- kwa Mungu mwenyewe kuwapindua toka madarakani?

Je, mfungo na maombi ya Gwajima yaliyomalizika hivi karibuni ya kuuondoa utawala wa Amaleki nao unahusiana na kushupaza shingo? Mambo ni mengi muda ni mchache, tunaendelea kuangalaia movies!
 
Utawala unaofitini watu wake, Utawala uliojiweka Madarakani Kinyume na Matakwa ya Walio wengi, Utawala uliobaka demokrasia, Utawala ulionuka damu toka mwanzo, na Utawala ulioasisi utumiaji wa Kiganja cha chuma na Viroba/sandarusi ...Ni fact Hauna uchungu na watu wake na ni swala la muda tu kwa maana Mungu anawapenda sana Watu wake.
 
Ni suala la muda tu!
 
Back
Top Bottom