Anayestahili kulaumiwa kosa la watoto wadogo wa shule kubebwa mshikaki kwenye bodaboda

Anayestahili kulaumiwa kosa la watoto wadogo wa shule kubebwa mshikaki kwenye bodaboda

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Pamoja na kwamba Sensa haifanyiki siku hizi!
Wacha nijikite kwenye mada tajwa!

Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watoto wadogo wa shule kubebwa zaidi ya mmoja kwenye pikipiki moja (mshikaki).
Kitendo hiki kinahatarisha Sana usalama wa Watoto hao lakini Je; Anaestahili kulaumiwa hapo ni Nani?

JE, NI DREVA BODABODA?
Ukitizama juu kwa juu lawama unaweza kumpatia dreva bodaboda, lakini ukitafakali utagundua dreva yule Ni mwajiliwa wa wazazi wa Watoto!

wazazi watatu wanaunganisha nguvu kuchangia malipo ya bodaboda kwa mwezi!
mfano! Kama malipo ya bodaboda yalihitaji 120000/= kwa mwezi, Basi wazazi watatu wanapoungana watalipa elfu 40000/= tu ili maisha mengine yaendelee!
Ikumbukwe mbali na nauli, watoto wanahitaji bukubuku kila siku za kula shuleni.
JE, NI WAZAZI?
Hakuna mzazi anaependa mwanae apate tabu!
Kutokana na changamoto za ugumu wa maisha wazazi wanaamua ku-risk maisha ya watoto kuwapandisha bodaboda ya mshikaki ingawa kiuhalisia wengi hawapendi wanao wapate tabu namla Ile lakini Hakuna namna!
JE, NI JESHI LA POLISI?
Ifahamike hata polisi ni wazazi, Wanaouwezo wa kufukuzia bodaboda zote zinazobeba mshikaki ili wazikamate lakini kwa usalama wa Watoto, hawafanyi hivyo kwasababu watahatarisha zaidi maisha ya watoto!

"Kuna mpango wa jeshi la polisi kuanza kupiga picha bodaboda wanaobeba Watoto wa shule mshikaki ili baadae wawafatilie taratibu maskani mwao sambamba na kukamata na wazazi waliobariki uvunjaji wa sheria ili kukomesha Hali hii"
Lakini Je? kipi Bora watoto watembee kwa mguu umbali mlefu wagongwe kwa kuvuka barabara? au wasiende kabisa shule?

MAONI YANGU!
Serikali iendane na kasi la ongezeko la watu, Miji imepanuka kwahiyo serikali ijenge shule ya msingi kila kitongoji kadri miji inavyopanuka ili kuepusha watoto kuvuka umbali mrefu kwenda shule!

Serikali ifikilie kufungua shule za awali daraja la Kati mtaani! Vinginevyo serikali watoe vibari vya shule za awali/daycare center zilizopo mtaani kufundisha watoto Hadi darasa la tatu ( kuanzia la kwanza Hadi la tatu) kwa kuzingatia mitaala ya shule za msingi!

Ili watoto hao wapokelewe shule za msingi kuanzia darasa la nne wakiwa angalau wamekomaa kiasi Cha kufika wenyewe shule!

Hii itapunguza Sana kero kwa wazazi kupandisha watoto wadogo bodaboda za kuchangia!
Kwa umri wa darasa la nne mtoto ataweza kwenda mwenyewe shule hata kama ni kwa mguu na kuweza kuvuka barabara salama!
Haya ni maoni yangu!

Je, wewe una maoni gani ili kupunguza hatari kwa watoto wadogo wanaobebwa mshikaki? KARIBU
 
Kama ulivyotamka hapo awali kwenye mada yako kuwa sababu ni umaskini.
Na mimi nakazia hapa sababu ni umaskini,mzazi tajiri hawezi kukubali mwanae kupanda bodaboda kwenda shule hata kama atapanda peke yake.
Umaskini haujawahi kumuacha mtu salama.
Hakuna kitu kilichofanywa kimaskini kikawa salama,maana hata nyumba zilizojengwa kimaskini pia ni hatari muda wowote inadondoka na watu wakiwa wanaishi humo na huwezi kuwaambia wahame wakalale nje itabidi waendelee kuishi kwa vile hawana njia mbadala.
 
wazazi ndio wa kulaumiwa kama wanaona 80k ina thamani kuliko maisha ya watoto wao basi sawa tu.....
pia wao ndio wameichagua ccm lawama zote kwao tu.........
 
Kama ulivyotamka hapo awali kwenye mada yako kuwa sababu ni umaskini.
Na mimi nakazia hapa sababu ni umaskini,mzazi tajiri hawezi kukubali mwanae kupanda bodaboda kwenda shule hata kama atapanda peke yake.
Umaskini haujawahi kumuacha mtu salama.
Hakuna kitu kilichofanywa kimaskini kikawa salama,maana hata nyumba zilizojengwa kimaskini pia ni hatari muda wowote inadondoka na watu wakiwa wanaishi humo na huwezi kuwaambia wahame wakalale nje itabidi waendelee kuishi kwa vile hawana njia mbadala.
kweli kabisa
 
Siku hizi bodaboda hawavai kofia ngumu Tena. Hawalipi Kodi aina yoyote. Kisa eti kampeni na serekali imelala usingishi wa pono
 
Siku hizi bodaboda hawavai kofia ngumu Tena. Hawalipi Kodi aina yoyote. Kisa eti kampeni na serekali imelala usingishi wa pono
tujadili la watoto kwanza kubebwa kwenye bodaboda
 
Back
Top Bottom