Anayesumbuliwa Na vidonda vya tumbo tafuta majani yanaitwa mashona nguo

Anayesumbuliwa Na vidonda vya tumbo tafuta majani yanaitwa mashona nguo

Miss_Mariaah

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
2,176
Reaction score
4,979
Habari za Leo wakuu,

Haijalishi vidonda vyako vimefika hatua gani au umekuwa ukisumbuliwa kwa muda gani, unaweza kutumia tiba ya asili kwa majani ya mashona nguo. Haya ni yale majani ambayo huwa yanatoa vimiba vidogo vya rangi nyeusi vyembamba, ambavyo huweza kunasa nguo unapopita karibu nayo.

Jinsi ya Kutumia:

1. Chukua majani kiasi cha ukubwa wa kiganja cha mkono.

2. Weka kwenye maji kiasi cha glasi moja.

3. Chemsha kwa muda mfupi hadi rangi ya maji ibadilike na kuwa ya machungwa (orange).

4. Epua na chuja kisha kunywa.

Ratiba ya Matumizi:

• Kunywa kila asubuhi ukiamka kabla ya kula chochote.

• Rudia jioni kabla ya mlo wa usiku.

Mimi mwenyewe nimetumia ndani ya siku mbili na nilipata nafuu ya ajabu.

Kila la heri!
Sharing is caring
 

Attachments

  • IMG_20241209_102710.jpg
    IMG_20241209_102710.jpg
    473 KB · Views: 11
  • IMG_20241209_102710.jpg
    IMG_20241209_102710.jpg
    473 KB · Views: 13
Back
Top Bottom