Labda kwa taarifa mimi ni Simba ila miaka ya karibuni bado simba lakini sio wale mpaka kupiga kelele. Mimi nimeongelea team za Tanzania sijaongelea team moja, wanaweza kusajili hata team mpya mpaka kocha sawa tu ila nimesema hali hii utaikuta Tanzania tu hakuna sehemu nyingine. Hao kina Liverpool tu majeruhi kibao lakini unaona wamekomaa kuna mtu katoa sababu ya corona ndio maana wameambiwa na CAF waongeze. Sasa tufanye ni kweli, team imesafiri na wachezaji 25 kufika kule wa tano corona team haiwezi kucheza? sababu hazina mashiko ila tunaweza kusajili tu wala sio issue, point yangu inabaki haya mambo yako kwetu tu.