Anayetengeneza pesa analipwaje?

teledam

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2017
Posts
927
Reaction score
1,239
Habari zenu wadau,naamini wengi wetu tupo poa sana licha ya tishio/janga lilipo mbele yetu. Nina imani kubwa kwamba pamoja na jitihada zetu kujikinga Mwenyezi atatuepusha na hili.

Nisiwachoshe waungwana, Nafikiri tupo wengi ambao hatufahamu mchakato mzima ni jinsi gani kampuni ama taasisi zinazopatiwa zabuni ya kutengeneza fedha zinavyolipwa lakini pia miongoni mwetu wapo wanaofahamu hiyo michakato.

Kila ninapowaza fedha huwa najiuliza ikiwa je mzabuni analipwaje? Kwa mfano ikiwa serikali imeagiza kutengenezewa tsh billioni mbili mzabuni atalipwa kiwango gani? Yaani sawa na kuuliza atalipwa sawa na kiwango alichotengeneza ama zaidi au ikiwa ni chini ya hapo ni kwa muda gani atalipwa na kwanini,nafikiria kwamba labda anaweza kulipwa kulingana na mkataba baina ya pande hizi mbili lakini pia nawaza kwamba pengine kuna 'international standards ' sijui, najaribu tu kuwaza.

Karibuni wajuzi wa mambo tuelemishane.

Natanguliza shukran.

Rai:
I.Tafadhali kama uelewa wako ni kama wangu usibandike mizaha, ni bora kuuliza swali ili wenye ufahamu wajibu kwa faida ya wengi

II. Uzi huu umelenga kutafuta elimu kutoka kwa wadau mbalimbali wenye ufahamu jinsi gani fedha zinatengenezwa na si vinginevyo. Aidha mtoa mada anaheshimu kanuni zote zinazolinda na kusimamia fedha katika taifa letu
 
Dhana ya pesa ipo zaidi kisheria yaani kampuni haitengenezi pesa "pesa kwa maana ya thamani ya pesa" kampuni zinapewa tenda ya kuchapisha noti kadhaa labda noti laki moja.

Baada ya kichapisha noti kwa makubaliano walioingia na serikali basi serikali kwa kutumia sheria huipa nguvu noti iyo kuwa fedha halali. Na malipo ya kuchapisha noti ni kama vile mtu aliyepewa tenda ya kuchapisha vipeperushi vya ukimwi au corona.
 
Japo sielewi sana, ila nadhani analipwa kama mtengeneza tiketi. Mfano Kuna mabasi root tofauti kampuni moja na tiketi zinafanana lakini mchapishaji alilipwa bei ile ile hata kama tiketi zitatofautiana bei.
Haya hamishia mfano huu kwenye kutengeneza hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
πŸ˜†πŸ˜†eti kama vipeperushi vya ukimwi,kuna raia wanachekesha sana humu

Nyongeza,ina maana mkandarasi anamaliza kila kitu chkulia mfano note ina namba na alama mbali mbali zilizofichwa ambazo mzabuni anaweza shawishika kutengeneza zaidi ikiwa atamaliza kila kitu mwenyewe?

Tuseme mimi nimepewa zabuni ya kutengeneza pound au dinnar si nitashawishika kutengeneza nyingi zaidi kwa faida zaidi ama hili limekaaje?
 
Kama huna hakika kuwa mpole kama mimi kaka😎
 
Kama hajaelewa na hapa ndo basi tena
Haya ndio masihara yenyewe sasa naomba tuwe serious jamani, siyo lazima tuandike wenye uelewa kama mimi tusubiri hoja za kujenga. Tujiheshimu kwenye kutafuta elimu zaidi
 
Haya ndo masihara yenyewe sasa naomba tuwe serious jamani,siyo lazima tuandike wenye uelewa kama mimi tusubiri hoja za kujenga. Tujiheshimu kwenye kutafuta elimu zaidi
Mkuu sio masihara majibu yapo hapo juu yanajiyosheleza unataka kujaza comment kwenye post yako tuuuuu au unataka kuelewa,?
Kama hunaelewa uliza swali
 
Mkuu sio masihara majibu yapo hapo juu yanajiyosheleza unataka kujaza comment kwenye post yako tuuuuu au unataka kuelewa,?
Kama hunaelewa uliza swali
So mzabuni anamaliza kila kitu ama kuna kitu central bank inakuja malizia kwenye noti?
 
So mzabuni anamaliza kila kitu ama kuna kitu central bank inakuja malizia kwenye noti?
Yes.
Mchapaji anachapa.....BOT anaihalalisha kuwa pesa
Chukulia mfano kampuni ya kutengeneza vocha inatengeneza lakini haitumiki hadi kampuni ya simu iidhinishe ile vocha
 
Yes.
Mchapaji anachapa.....BOT anaihalalisha kuwa pesa
Chukulia mfano kampuni ya kutengeneza vocha inatengeneza lkn haitumiki hadi kampuni ya simu iidhinishe ile vocha
Ni kweli kabisa usemayo,Na kwenye kutengeneza Pesa kuna kampuni ni zaidi ya moja lazima zihusike katika kutengeneza pesa,mfano Mzabuni wa kwanza anatoa material ya hela ,kuna mtu kazi yake ni kutengeneza Rangi itakiwayo kwenye noti,anakuja mwingine hapo ambaye anakuwa mtu wa mwisho yeye ndio anazichapisha ila zinatoka kwa mfumo wa namba.

Malipo kwa mtengenezaji yanafanyika ivyo mfano Serikali inasema katika kila noti moja ya elfu kumi elfu tatu ni malipo ya mtengenezaji kwa hapo mtengenezaji anachukua elfu 3000 yake anazidisha kwa namba zitakazoishia
 
Yes.
Mchapaji anachapa.....BOT anaihalalisha kuwa pesa
Chukulia mfano kampuni ya kutengeneza vocha inatengeneza lkn haitumiki hadi kampuni ya simu iidhinishe ile vocha
umesomeka mkali, ila una majunguu
 
I find this helpful
 
Nyongeza vipi kuhusu pesa za kigeni? Au hutumika tu kununua bidhaa nje?
 
Sio kuchekesha mkuu ni namna tuu ya kufikisha ujumbe.

Sasa kwenye mchakato wa kutengeneza ni mrefu kidogo ili kutoruhusu mtu au kampuni kuiba noti. Kampuni haimalizi mchakato wote kuna alama na namba za noti ambazo huwekwa na B. O. T pindi wakiongeza fedha kwenye mzunguko au fedha inapochakaa basi namba yake hupewa noti mpya.

Sasa hapa kwenye namba ndipo hizi kampuni za kuchapisha noti hazihusiki bali bot wanaweka namba zao wenyewe kabla ya kuzipeleka kwenye mzunguko.
 
KUHUSU MALIPO YA KUTENGENEZA PESA.

Kama walivyoeleza baadhi ya wadau waliotangulia, huwa ni makubaliano ya mamlaka husika na kitengo/kampuni inayotengeneza pesa. Taarifa sahihi na mahsusi ni ngumu kuzipata, na ni kwasababu za kiusalama; Hivyo ni ngumu kusikia benki kuu, serikali au kampuni zinazotengeneza pesa zinaongelea kwa uwazi jambo hili. Lakini zipo nchi ambazo taarifa zake zipo hadharani mfano kwa nchi ya Marekani;

Noti ya $1 na $2 inawagharimu 4.9 cents kuitengeneza, wakati $5 inagharimu 10.9 cents, $10 inagharimu 10.3 cents, $20 na $50 inagharimu 10.5 cents, na $100 inagharimu 12.3 cents. Kwa lugha rahisi, kadiri pesa inavyokuwa na thamani kubwa zaidi na gharama ya kuitengeneza inaongezeka.

SAWA, KWA HIYO - NANI HASA ANATENGENEZA PESA?

Kuna baadhi ya nchi zinatengeneza pesa zao ndani ya mipaka yake, aidha kwa kitengo kinachosimamiwa na serikali au kwa kutoa kandarasi kwa kampuni za ndani ya nchi. Mfano nchi ya Marekani ina kitengo maalumu kinachosimamiwa na serikali ambacho kazi yake ni kutengeneza pesa. Lakini pia zipo nchi ambazo ni kawaida kutengeneza pesa nje ya mipaka yao, mfano nchi kama Liberia haina kabisa mitambo ya kutengenezea pesa zake. Sijui Tanzania kama tuna hiyo mitambo au kampuni yenye hiyo mitambo.

MH! ASA KWANINI NCHI ZINATENGENEZA PESA UGHAIBUNI - BADALA YA KUNUNUA HIYO MITAMBO?

Kwa kifupi, ni zoezi gumu na ni gharama sana.Kampuni nyingi zinazohusika na utengenezaji wa pesa zimekuwa zikifanya biashara hiyo kwa karne kadhaa. Kwa hiyo wamebobea - wana teknolojia, uzoefu na wamejijengea rekodi nzuri katika ulinzi/usalama. Na kwasababu ya tenda nyingi wanazopata inakuwa ni biashara yenye faida kwao.

Kwa mfano; kampuni mojawapo inaitwa De La Rue - hii ilianza kutengeneza pesa mwaka 1860 mpaka sasa ni moja ya kampuni zinazoongoza kwa kutengeneza pesa nyingi zaidi duniani.

Kwa nchi zinazoendelea kiuchumi haileti maana kutengeneza pesa zake yenyewe. Kwanza inagharimu pesa nyingi sana kununua mitambo, ilhali idadi ya pesa zinazohitajika ni kidogo. Yaani ni sawa unaamua kununua YUTONG kwaajili ya mitoko ya kifamilia wakati una familia ya watu 6 tu... 🀣hehehe!. Lakini pia gharama zaidi ni zoezi la kuhakikisha mitambo hiyo inaendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia ili kukabiliana na pesa bandia.

Kwa kawaida kampuni moja ya kutengeneza pesa inachapisha noti zipatazo bilioni 1.4 kwa mwaka. Kwa hiyo kama nchi inahitaji noti chache chini ya hapo kiuchumi haileti maana. Marekani wao wanachapisha noti zisizopungua bilioni 7 kila mwaka (Hii ni idadi ya noti sio thamani ya noti).

NIMEKUELEWA, LAKINI..., KWANI KUNA HATARI YOYOTE KWA NCHI KUTENGENEZA PESA UGHAIBUNI?

Mwaka 2011 serikali ya Uingereza ilizuia pesa zenye thamani ya takribani Dinari Bilioni 1.86 (Karibu Trilioni 2.6 TZS) ambazo zilikuwa zimechapishwa na De La Rue kwaajili ya Libya, hali iliyopelekea upungufu wa pesa kwa nyakati za mwisho mwisho za utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.

Hivyo kuna mida flani mamlaka za nchi ambako pesa zinachapishwa zinaweza kuzuia pesa za nchi nyingine lakini ni nadra sana kutokea. Ile ishu ya Libya liliwashtua wadau wengi lakini haikuwa na madhara makubwa kwani bado nchi nyingi zinatengeneza pesa nje ya mipaka yake. Hata kama hawapendi, watafanyaje - uwezo wa kuendesha mitambo hawana.

Kinadharia, nchi inaweza 'kuzamishwa' kwa kutengeneza pesa nje ya nchi kama mtengenezaji 'aki-snitch' - akachapisha noti nyingi zaidi ya zile zilizoagizwa, bila ruhusa ya benki kuu. Unajua kitakachotokea?... pesa zitakuwa zingi kinyama kitaa (Oversupplying an economy with cash). Pesa zikizidi mojawapo ya madhara yanayotokea ni mfumuko wa bei (inflation.) - na mfumuko wa bei una madhara mengi kuliko faida. Wazungu wanasema 'inflation is a big NO'

Nadharia nyingine ni kwamba, kuna hatari kuwa taifa ambalo linachapisha pesa za nchi nyingine linaweza kuzifahamu alama za siri/za ulinzi za noti fulani, hivyo wanaweza kutengeneza noti bandia. Nasema ni nadharia kwasababu hakuna ushahidi unaothibitisha kutokea kwa matukio ya aina hii.

Na kuna tatizo la uadilifu kwa nchi zile ambazo rushwa imetawala - yaani nchi ya mafisadi na wanachapisha pesa zao wenyewe.(Kichaa kakabidhiwa rungu!). "Do you trust people in your own country to print your own money?" alisikika mzungu mlevi mmoja pale Sinza Mori akimuuliza mzee mlevi mwenzake.

Yote kwa yote ukweli ni kwamba, hakuna chombo cha kimataifa kinachosimamia utengenezwaji wa pesa.

OH OK, APO NIMEKUSOMA - LAKINI KUNA MAHALI UMESEMA MFUMUKO WA BEI "UNA MADHARA MENGI KULIKO FAIDA",.. KWANI FAIDA YA MFUMUKO WA BEI NI ZIPI? ONGEA KWA KISWAHILI NIKUELEWE.😎

Ssssh sogea nikunong'oneze!! - Ni hivi, Benki kuu mara nyingi huwa inaratibu mfumuko wa bei, usizidi wala kupungua kiwango fulani... mara nyingi huwa ni 2%. Utaniuliza kwanini Benki kuu iratibu mfumuko wa bei? Hahaha, bila shaka wewe unadhani uchumi ungekuwa mzuri zaidi kama vitu vingekuwa havipandi bei kabisa, na mwisho wa siku tuwe wakweli, kwani nani anapenda vitu vya bei juu (Ukiachana na wadangaji)?πŸ˜›πŸ˜‚ Ukweli ni kwamba BORA MFUMUKO WA BEI wa wastani na unaoratibiwa kuliko kinyume chake... yaani MPOROMOKO WA BEI (Sijui kama neno hilo ni sahihi) lakini kwa Kiinglishi wanaita 'deflation'.

Twende taratibu... Mporomoko wa bei unatokea pale ambapo bei za vitu zinashuka. Najua hapo umewaza- ah! sasa bei zikishuka si ndio fureshi kabisa ama nini??? Well, kinachotokea bei za vitu zinaposhuka 'consistently' watu wanaacha kununua nyumba, magari na bidhaa zingine kwa imani kuwa bei zitaendelea kushuka hivyo wanasubiri bei zifike chini zaidi ili wanunue. Uchumi unadorora, mzunguko wa pesa unakuwa mdogo sana.... Tuongee kiingredha kidogo kwa msisitizo au unasemaje? -"When shoppers expect prices to rise in the future, they will buy more now while prices are still low. That "buy more now" philosophy stimulates the demand needed to drive economic growth." Na ndio maana benki kuu inahakikisha inakuaminisha kuwa mfumuko wa bei utaendelea kuongezeka ili ununue vitu LEO na SIO KESHO kabla vitu havijapanda bei zaidi. Jinsi unavyofanya manunuzi, uchumi unaimarika.

Umeona hesabu hizo mdogo angu? Na umeelewa lakini?... sio unatoa macho tu!.

DAH! EBWANAEEE, NAONA TUVUTE PUMZI KIDOGO.

Sawa, tulikuwa tunaongelea mada ya kutengeneza pesa. Sasa chukua hii;

Mwezi Septemba, mwaka jana (2019) serikali ya Liberia ilitangaza kupoteza $104m (Takribani Bilioni 241 TZS) Ah hapana, hazikupotea kwasababu ya mikataba mibovu, au ufisadi hapana; bali hizo pesa - zikiwa taslimu - zilisepa katika mazingira ya kutatanisha. Yaani ni hivi: zile pesa zilikuwa zimeagizwa na benki kuu ya Liberia kutoka kwa wachapishaji nje ya nchi na zikafikishwa mpaka Liberia, na zikapitia mchakato wote wa utoaji mizigo uwanja wa ndege na kisha msafara wa kuzipeleka benki kuu ukaanza. Lakini mpaka leo hazijafika πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ zilipotea wakati zimeshatoka uwanja wa ndege wa Liberia kupelekwa benki kuu. Hahahaaa wabongo noma... oupss kumradhi, wa-liberia nouma kabisa!

Naomba kuwasilisha.
 
Kuna makampuni maalumu kwa ajili y akuprint pesa mfano De La Rue ya UK yenyewe inarint kwa mabenk zaidi ya 100 na pia kuna ile Giesecke & Devrient ya Germany inaprint kwa mabenki zaidi ya 80. Process za uzalishaji pesa ni ndefu na ngumu pia kwa materials na printing hivyo nchi nyingi zinaingia mikataba kwa hata makampuni makongwe.

Ni makampuni ambayo yamejijengea uaminifu mkubwa hivyo yameweza kuwa sokoni kwa zaidi ya miaka 100 mfano hiyo ya UK ilianza mwaka 1890 hivi kwa kuiprintia Mauritius note zake.

Shughuli yote hufanywa na kampuni husika kuanzia kidesign, materials na printing. Nchi nyingi na hata makampuni husika huwa hayasemi yameingia mikataba na nchi zipi kuziprintia pesa zao, kuna tukio limewai kutokea kwa fedha za Liberia kuibiwa zote zilipokuwa zikiingizwa nchini humo kutoka mahala zilikoprintiwa. So huwa ni shughuli ambayo ni very confidential.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kampuni zinazochapisha fedha hulipwa kwa Bonds (dhamana) au commodities.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…