huu mtindo wa kutaja namba za simu za watu na kuzianika katika mtandao sio uungwana hata kidogo! nadhani kumtaja mtu, kuweka picha yake, kutaja kosa lake ambalo ni tuhuma na halijathibitishwa, na kueleza namna ambavyo ungependa uma umchukie sio busara wala mada kama hii haiwezi kujadiliwa na waungwana kabisa. ungetaja na jina lako pia, uandike na namba yako ya simu, na ueleze na makosa yako na pia utueleze umepataje habari zote hizo! jamani tusitumie mitandao hii kuwa demonize watu tuliotofautiana kazini!