wanaJF,
Ninamchallenge kizazichadotcom, aweke hadharani hizo emails anazotaja! Vinginevyo ni upuuzi tu.
Naomba niwajulishe WanaJF kuna watanzania wema, wenye dhamira safi, wanaoelewa utawala bora, na wenye uchungu na Taifa hili. Ndio wanaotoa Taarifa ya aina zozote za uhalifu. Kumbuka uhalifu ni uhalifu, kutoa siri ya uhalifu ndani ya chombo chochote cha sheria au kupitia chombo cha Serikali ni jambo na kitendo cha kizalendo. Asiyekubali kuwa sehemu ya bozo na uchafu ni jukumu na wajibu wake kuweka hadharani.
Kumbukeni Marmo aliposema Bungeni Dr Slaa tutakukanata, jibu langu lilikuwa jepesi, "Marmo" tutakukamata wewe kwa kuwa ndani ya kabuki za Serikali haitakiwi kuwe na uozo wala uchafu wowote ule. Hivyo Chadema hatuhitaji kulipa wala kununua document yeyote ile kwa kuwa watanzania wengi bado wana dhamira safi hivyo wanapotoa wanatoa nyaraka kwa uzalendo.