Anayewaelewa Yanga atueleweshe

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
16,784
Reaction score
23,312
Ukifatilia post nyingi za washabiki wa Yanga wakisaidiwa na waandishi wao wenye mahaba wamekuwa wakiilaumu Simba kwa kuua vipaji vya wachezaji, wameisema sana Simba kwa kitendo cha kumdajili Ajibu wakati alikuwa anatakiwa na TP Mazembe lakini wanasahau walikataa kumruhusu Jerry There kucheza Sweden ili acheze mechi ya Simba na Yanga.

Ngasa akiwa Simba kwa mkopo alipata nafasi ya kucheza El Mereikh ya Sudan lakini wakamrubuni akajiunga nao leo tunaona anavyolalamika chambua ameeleza jinsi alivyoshindwa kucheza soka ya kulipwa Afrika Kusini baada ya viongozi wake kumbania Chuji ameongea juzi na kueleza Yanga walivyombania asijiunge na TP Mazembe waache kuwaongelea Simba kwa mifano michache wanaonyesha jinsi gani wanavyowabania wachezaji wao.
 
Hujaelewa kwa nini watu wanalalamika. Ni kwamba hao wachezaji walikuwa ni wachezaji mahiri walivyokuwa Yanga.Walikuwa nguzo za timu. Lakini wakienda simba wanapigwa benchi mpaka viwango vinafubaa na kuisha kabisa.Lakin hao wachezaji unaowataja walikuwa wanang'aa. Lakini wangeenda simba ungekuwa mwisho wao.

Msuva Yanga ilimzuia mwanzoni asiende Difaa Al Jadid.Wakamshawishi kuwa aongeze mkataba ili wakija anunuliwe kwa pesa nzuri. Msuva akakubari na wakaja tena Difaa wakapigwa pesa na Yanga ikafaidika.

Sasa Gadiel anafaidika simba au anafeli na Ajibu pia? Waambie hao akina Ajib wapambane wasilete umama kwenye mpira hawachelewi kuanza kuomba misaada wakizeeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemaliza kila kitu mkuu, uzi ufungwe sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ngasa aliyekataa timu zenye mshiko Kama Ile ya Sudan kiwango chake kikoje pia unataka kutuaminisha mchezaji akitoka Simba kwenda yanga ndio kiwango chake kinakua huyo chuji alifulia akiwa timu gani
 
Acha uongo msuva alienda as free Agent
Unaongelea Gadiel na Ajibu ambao wanapambana kutafta namba umesahau kuongelea Ally Ally,Rafael Lot ambao walikuwa bora walipotoka lakini mkawaharibu
Dante na Paul Godfrey ambao hawachezi kwa sababu wanadai



Yanga ni kijiwe cha wanywa mtukuru siku zote wanakaa kupiga majungu aliefanikiwa wakisahau wachawi wamaendeleo yao ni wao
 
Bado Dilunga, Lusajo, Mhilu wako wengi
 
Kuielewa Yanga kwahitaji akili kubwa.

Ni vigumu kwa mbumbumbu au misukule kuielewa Yanga.

Case closed.
 
Hivi ngasa aliyekataa timu zenye mshiko Kama Ile ya Sudan kiwango chake kikoje pia unataka kutuaminisha mchezaji akitoka Simba kwenda yanga ndio kiwango chake kinakua huyo chuji alifulia akiwa timu gani
Chuji hajawahi kufulia umri ndio chanzo cha yeye kushuka lakin hadi sasaivi bado yupo vizuri.Ngasa kwenda Sudan yeye mwenyewe hakutaka ukilinganisha na hali ya sudan kiusalama wakati ule haikuwa nzuri.Ni kweli mchezaji akitoka Yanga kwenda simba kiwango kinashuka lakin mchezaji akitoka simba kuja Yanga kiwango kinapanda.Angalia Yondani,Ajib,Niyonzima,Hamis kiiza Diego n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…