Anayeweza kuitafsiri hii ndoto anisaidie

Anayeweza kuitafsiri hii ndoto anisaidie

Under-cover

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
1,834
Reaction score
3,042
Samahani, mimi leo nimeamka nikapigiwa simu na mdogo angu akanambia kuwa mama yetu aliota usiku wa kuamkia leo kuhusu mimi, kuwa nilikuwa niko porini, alafu watu wananisemesha ila mimi siwasikii. NDOTO HIYO.

Baadae saa 11 jioni, nilikuwa chumbani peke angu alafu mlango nilikuwa nimeuegesha ila gafla nikasikia sauti inaniita kama mara mbili ivi, kupitia pale mlangoni wa chumba changu, nikatoka kwa woga kufata sauti inapotoka sioni kitu, kisha nikatoka kwenda kuongea na mama kwenye simu kumuuliza ile ndoto, akanielezea kuwa , jana mida ya saa tano usiku alijihisi mguu unamuuma, akachukua dawa akajichua ,kidogo akapitiwa usingizi gafla akaanza kuota ndoto, kuwa akiniona niko porini alafu, yeye akiwa na baadhi ya watu wananiita ila mimi nikageuka nikacheka kisha sikuwajibu kitu nikaenda zangu, pembeni katika kakibanda kadogo nikaingia , ila wenyewe wakanifata na kuniita nitoke nikakaa kimya.

Mama mwenyewe akanijia mule bandani akanibeba na kunikalisha, hapo mama akashituka ndoto ikaishia hapo, ila pia palipo kucha mguu ulimuuma tena akauchua mpka sasa hasikii maumivu tena. Sasa mtumishi nahisi nimeingia katika vita ya kiroho mimi na mama yangu , nahisi tunachezewa, ila sijajua na watu wapi wanaofanya ivyo, nimeenda kwa watafusiri mbali mbali , mmoja kaniambia ni masuala ya mizimu, mwingine kanambia kuna namna nafanyiwa na watu wa karibu, naombeni wajuzi wa mambo mnipe ushauri🙏.
 
Wale wanaokuita ni wale wasiopenda safari yako ya mafanikio.

Kucheka kwako ni kuonesha matumaini na msimamo juu ya kile unachofanya kitakutoa.

Mama kuja kukuchukua na kukukarisha ni baraka zake juu ya kile unachofanya.

Cha Msingi Simama na Mungu na fuata Ushauri wa mama juu pia jitahidi kwenye Siri zako iwe za mafanikio au laah mshirikishe yeye maana hapo Anaonekana ndio nguzo yako.

Ahsante 🙌
 
Wale wanaokuita ni wale wasiopenda safari yako ya mafanikio.

Kucheka kwako ni kuonesha matumaini na msimamo juu ya kile unachofanya kitakutoa.

Mama kuja kukuchukua na kukukarisha ni baraka zake juu ya kile unachofanya.

Cha Msingi Simama na Mungu na fuata Ushauri wa mama juu ya mama na jitahidi kwenye Siri zako iwe za mafanikio au laah mshirikisha yeye maana hapo Anaonekana ndio nguzo yako.

Ahsante 🙌
sawa asante kwa ushauri, ila kuna hii ya kusikia sauti nikiitwa na nilikuwa sijalala niko macho , nahisi mauza uza, ni kweli, imenitokea, nawaza sauti ile ni nguvu ovu au.
 
sawa asante kwa ushauri, ila kuna hii ya kusikia sauti nikiitwa na nilikuwa sijalala niko macho , nahisi mauza uza, ni kweli, imenitokea, nawaza sauti ile ni nguvu ovu au.
Hata mi nishaitwa mara nyingi Sana Ila bahati nzuri sijawahi kuitika..

Niliwahi kumueleza Mzee hili tatzo akasema Nilifanya vizuri kutokuitika.

Mpaka leo hua siitiki hovyo hovyo hata akiniita Mzee mwenyewe maana ndio nilivyozoea.

Naitika nikijiskia Tu yaan automatically walasio Kwa shinikizo la sauti ya MTU.
 
Hata mi nishaitwa mara nyingi Sana Ila bahati nzuri sijawahi kuitika..

Niliwahi kumueleza Mzee hili tatzo akasema Nilifanya vizuri kutokuitika.

Mpaka leo hua siitiki hovyo hovyo hata akiniita Mzee mwenyewe maana ndio nilivyozoea.

Naitika nikijiskia Tu yaan automatically wa sio Kwa shinikizo la sauti ya MTU.
kwahiyo mkuu, kuitwa ivyo inakuwa aale wabaya ndio wanafnya huo mchezo?
 
na
Hata mi nishaitwa mara nyingi Sana Ila bahati nzuri sijawahi kuitika..

Niliwahi kumueleza Mzee hili tatzo akasema Nilifanya vizuri kutokuitika.

Mpaka leo hua siitiki hovyo hovyo hata akiniita Mzee mwenyewe maana ndio nilivyozoea.

Naitika nikijiskia Tu yaan automatically wa sio Kwa shinikizo la sauti ya MTU.
pia mkuu samahanj, ina maana kuna watu walishajua vile mbele nitakavyokuwa ndio maana wanaanza kunishambulia?, kwakua sijawahi kuongea chochote kuhus ndoto zangu, huw ni mkimya, au wamejauje, au kuna mambo ya mizimu huko nakinzana nayo?
 
Rekebisha mlango Mangi, kuhus ndoto kua makini
yaani mlango sikuukaza, nikama vilr unauchaa alafu upepo ukipita unakuwa unajifungua na kujifunga, hapo sass na sauti nikasikia mara 2 ikiniita.
 
na

pia mkuu samahanj, ina maana kuna watu walishajua vile mbele nitakavyokuwa ndio maana wanaanza kunishambulia?, kwakua sijawahi kuongea chochote kuhus ndoto zangu, huw ni mkimya, au wamejauje, au kuna mambo ya mizimu huko nakinzana nayo?
Ndio hivyo
 
Wanasoma mawazo yako so sio lazima uwaambie watu shetani anajua unataka uwe nani mbeleni,kama ni hatari kwa ufalme wake lazima akubomoe kabla
 
Ndoto ni ndoto ambayo haina kitu... Tatizo tunaiman potofu sana kuhusu ndoto.

Ndoto ngapi tumeziota na hazina uhalia wowote...

Hapo usipo kuwa makini utaingia mitego ya manabii feki au Mashekhe uchwara na Waganga.

Ushauri ni jitahidi usijiwazie mabaya na hata mama asikuwazie mabaya, unachowaza sana ndo ambacho ubongo uhifadhi na kukirudia usiku kama ndoto.
 
Hauchezewi mimi nimtafsiri tena nibure kabisa si uongo wa mitandao, anayekuchezea ni mama yako sali sana kwasababu mama yako yupo kwenye makundi ambayo amejiunga nayo na sasa yanakuhitaji, kwa lolote wanachotaka kufanya , ukiona mama yako anaumwa mguu ujue wameshindwa ukiona amepona ujue unatumika mwombe mungu sana ukiwa kwenye taja hata jina la BWANA YESU KRISTO MWOMBE MUNGU ALIYE HAI AKUTOE MAZINGIRA hayo kwani unapocheka inamaanisha hauwaogopi wanapokufuata inamaanisha wanakuhitaji kwa kazi yao unapoingia kwenye banda ni umejificha alipokubeba inamaanisha walifanikiwa kukupata kisha ukapotea ndiyo maana unasikia sauti ikikuita kwasababu huonekani kwenye ndumba zao sali sana mpendwa hiyo ni hatari, akiumwa tena zidi kusali uko kwenye mazingira mabaya kiimani , unapoambiwa na watafsiri kwamba unachezewa na mtu wakaribu inamaanisha huyo unayoongea naye, uswambie mama yako ndoto zako tena jaribu kuwaambia watu wengine Mungu akubariki sana na akulinde kila baya linaloendea kuharibu maisha yako ninakemea kwajina la YESU KRISTO Aliye hai.
 
Back
Top Bottom