Ancient Footprints discovered in Tanzania

Ancient Footprints discovered in Tanzania

Sasa Wasomi wetu nao ni Villaza? Tuna Maprofesa uchwara nadhani hawajui nchi yao zao ni siasa tu... ni aibu kubwa sana... wao zao ni kuhakiki tu wenzao akili zao wamezikalia... hadi waje wa wasomi wa Nje...

Kweli Elimu yetu ni bure tu... najisiakia faraja kuwadharau wasomi wa Tanzania haswa Maprofesa uchwara
 
01-Worlds-Oldest-Footprints-Engare-sero.ngsversion.1476115208177.adapt.885.1.jpg

Mudflats in the shadow of the Ol Doinyo Lengai volcano captured a huge trove of ancient human footprints.
 
Napata utata wa nafasi ya Mungu katika Uumbaji ...!!

Sayansi imejiweka thabit kuonyesha usahihi wa uumbaji,

Japo ....!!

Vyovyote vile lazma kuna nguvu ambayo imesababisha upate utata(reasoning) ambayo wengine bado tunaamini ni mungu tu ndo anaweza akaiumba

Vingine ni mfumo Tata wa mwili wako na viumbe wengine ; si lazima kubakia ktk vtabu vya dini Mara zote
Hakuna jambo la nasibu ukichunguza mambo hayo
 
Kwahiyo wanasayansi wanataka kutuaminisha kwamba hayo madubwana ya kale yalikuwa yana uwezo wa kutembea juu ya ujiuji wa volkano bila kuungua?

Eti! Mbona ni ajabu sana

Kuna sehemu niliwahi kwenda mkoa wa rukwa ; kule kuna nyayo chache na alama ya fimbo aliyokuwa anatumia muhusika
My assumption ; kuna viumbe walioumbwa kwa moto; akikatisha juu ya jiwe ni lazma liyeyuke tu;
Nafikiri ndo hao walikatisha na huko
 
Kwahiyo wanasayansi wanataka kutuaminisha kwamba hayo madubwana ya kale yalikuwa yana uwezo wa kutembea juu ya ujiuji wa volkano bila kuungua?
Moja kati ya swali zuri sana, mi huwa naangaliga tu, ipo siku watagundua kwamba hao viumbe walikuwa erupted pamoja na hiyo volcano, ila tuwaache tu waendelee kufanya excavations tanzanite ikiisha wataondoka wenyewe,
 
Yaani nimefikia mahali hata waseme Mungu anaishi Tanzania kwenye bustani fulani haitotusaidia kitu ,tuna kila kitu lakini sioni msaada wake kwetu
 
Hizi rasilimaki zinaweza kutumika na kutuletea utajiri mkubwa Tanzania lakini bado tuko nyuma na tutaendelea hivyo hadi itakapotokea serikali yenye akili kamilifu na kuwekeza kwenye mapinduzi ya maendeleo kwa faida ya watanzania.
 
Kwa hyo miaka yote hyo jamii za karibu na apo walikua hawazion hizo nyayo??
 
Napata utata wa nafasi ya Mungu katika Uumbaji ...!!

Sayansi imejiweka thabit kuonyesha usahihi wa uumbaji,

Japo ....!!
Pole sana, Mungu alishaumba na kumaliza kazi yake, sayansi inatafiti kazi za Mungu kama muumbaji na mwanasayansi wa kwanza, Na kwa taarifa yako huwezi kumtafuta Mungu katika kitu alichokiumba kwa sababu hakai hapo, Japo anaweza kukaa hapo akitaka.
TAFITI ZA WANADAMU NI ZA KAZI ILIYOPO TAYARI.
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Wana geologist njooni mtusaidie, maana hadi hapa sijaelewa kama lava huwa inapoa na mwanadamu anaweza kukanyaga bila madhala yoyote.
Nadhani hapo hiyo Lava haikuwa ya moto bali ni majivu yaliyopoa tu, na inaonekana hayo majivu yalinyeshewa na mvua na yakawa kama tope vile, kwa hiyo hao Binadamu walikanyaga wakati hiyo Lava Ash ikiwa kwenye hiyo hali ya utopetope, kisha inaonekana hizo foot print zilibaki hapo baada ya hiyo lava Ash kukauka na kisha zikafunikwa labda na ash zingine au mchanga?
 
Kwahiyo wanasayansi wanataka kutuaminisha kwamba hayo madubwana ya kale yalikuwa yana uwezo wa kutembea juu ya ujiuji wa volkano bila kuungua?
Umri wa hzo nyayo (19,000 yrs uliotajwa) unakinzana na uhalisia kwamba walikuwa wanatembea juu ya ujiuji wa volcano maana katika miaka hyo hakuna mlipuko uliotokea kwenye Oldonyo Lengai kusababisha ujiuji wa moto. Nakubaliana na fikra zao kwamba nyayo hzo zilikuwa kwenye tope litokanalo na mafuriko ya maji na si volcano.
 
Mimi swali langu nauliza ,hao watu wasayansi kwa nini wanasema kuna viumbe vimetoweka duniani na hapo hapo kuna viumbe vyengine vimebadilika kutoka hali moja kwenda nyengine na kwa nini hali hiyo ya kubadilika haiendelei .sisimizi ageuke kuwa ng'ombe.
Inabidi ufahamu sababu zao walizotoa za kwanini viumbe vingine vilipotea kabisa na vingine kubaki..

Mfano kwa sasa duniani kuna viumbe wengi ambao wako kwenye hatari ya kupotea kutokana na kuwindwa au kuathiriwa na shughuli za binadamu, mfano faru weusi na Tembo ambao inakadiriwa baada ya miaka 20 kama hali itaendelea kuna uwezekano tembo wakapotea kabisa.

Vile viumbe vilivyopotea vilipotea kqa sababu nyingi kwa mfano Ice age
 
01-Worlds-Oldest-Footprints-Engare-sero.ngsversion.1476115208177.adapt.885.1.jpg

Mudflats in the shadow of the Ol Doinyo Lengai volcano captured a huge trove of ancient human footprints.
Kuna anaweza kukanyaga
Inabidi ufahamu sababu zao walizotoa za kwanini viumbe vingine vilipotea kabisa na vingine kubaki..

Mfano kwa sasa duniani kuna viumbe wengi ambao wako kwenye hatari ya kupotea kutokana na kuwindwa au kuathiriwa na shughuli za binadamu, mfano faru weusi na Tembo ambao inakadiriwa baada ya miaka 20 kama hali itaendelea kuna uwezekano tembo wakapotea kabisa.

Vile viumbe vilivyopotea vilipotea kqa sababu nyingi kwa mfano Ice age
Swali jengine hivyo viumbe vilivyogunduliwa nyayo zao walikuwa hawana hisia,namaanisha hawakuogopa kuungua na volcanic lava?
 
Back
Top Bottom