Andaa chakula cha fasta! Fasta!

Andaa chakula cha fasta! Fasta!

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,151
Inawezekana ukapata mgeni wa ghafla nyumbani kwako, na ukawaza sana nini cha kumuandalia, au kama si ghafla basi hata kwa appointment, usifanye complication sana, tafuta kitu simple kitakachokufanya uandae kwa haraka umkampan mgeni, si unazamia jikon masaa matatu mgeni anabak sebuleni aking'aa macho kwenye TV tu, si vizuri, usimboe mgeni wako, siku nyingine hatakuja,. najua kuna aina nying za vyakula vya express, a.k.a fasta fasta, hebu leo tujaribu na hiki.Karibuniiiii!!!
FIRIGISI NA NDIZI ZA KUKAANGA!

Nilipata mgeni ikabidi niingie jikoni kumuandalia chakula cha mchana.Chakula kilikuwa firigisi na ndizi za kukaanga na salad kidogo.Nilihitaji vitunguu na karoti kama zinavyoonekana pichani.

Firigisi zenyewe

Nikaweka sufuria jikoni na mafuta ya kupikia,mie natumia mafuta ya alizeti.

Mafuta yalipopata moto nikatia vitunguuu nikavikaanga mpaka vikawa brown.

Nikaweka firigisi zangu,unaweza kuzikata vipande vidogo vidogo ila mie nilipendelea kuweka kama vilivyo.Nikaziacha zichemke kidogo kama dk 5 hivi...

Kisha nikatia limao,sikuongeza maji hata kidogo maana sikuwa nahitaji mchuzi.

Baada ya hapo nikaweka chicken masala ya aina hii naipenda sana maana ina harufu na ladha tamu sana.Huu ni mchanganyiko wa karafuu,tangawizi,kitunguu saumu,pilipili,chumvi,mdalasini,binzari,pilipili manga n.k

Nikaweka kijiko kimoja

Nikakoroga na kuongeza maji kidogo,chumvi kisha nikafunikia ziweze kuchemka na kuiva vizuri.

Baada ya dk 10 hivi nikaweka karoti na kukoroga kwa dk 1 kisha nikaipua zikiwa tayari zimeiva.

Pia nikakaanga ndizi kwa kuanza kuweka frying pan jikoni na mafuta ya kupikia.

Ndizi niliziweka chumvi kabisa.

Mafuta yalipopata moto nikaweka ndizi na kuzikaanga.Zilipokuwa tayari nikaipua tayari kumuandalia mgeni chakula.

Ni chakula kitamu,haraka na rahisi kuandaaa...tayari kwa kuliwa.
 
Chakula kitamu sana (japo ndizi fried, mmh! Ningezibwaga kwenye oven nikazisahau). Nimependa presentation yako, inavutia haswaa. Hapa naskia harufu kabisaa. Asante sana.

Chakula changu cha fasta ni spaghetti (zile nyembambaaaaa kama mchele) kwa nyama ya kusaga. Ama na combinenga ya sausage. Kuna smoked sausage, nazikata kimshazari hivi. Nakaanga kitunguu, followed by nyanya then sausage. Pembeni sufuria yenye mafuta nusu kijiko, naweka tambi na kuzitoss kidogo. Naweka maji ya moto kidogo sana na kufunika.

Baada ya dk tano naweka rojo ya sausage kwenye tamvi na kuvuruga kwa dakika chache. Matango ya kurashia, violaaaa!

Hii dish haichukui dk 20 kama unatumia.majiko mawili (namaanisha plates mbili)
 
...asante..mie ugali yai, kwa muda mfupi kabisa "mgeni" anakula.
 
thanks, hata cha kwako nimekipenda pia
 
Asante emeline,je hii chicken masala ya sanfaz naipata wap hapa mjini?
 
Nashukuru Kama upo arusha, nenda Rushda supermarket, au shoprite,.. maeneo mengine kwakweil mi mgeni
 
Jamani mi natafuta mke anayejua hayo makitu, Amelina r u occupied!
 
Last edited by a moderator:
Uwasilishaji umetulia,picha ya kila step,inafanya mtu unaelewa somo kwa haraka.
 
Back
Top Bottom