Andika mkoa na mtaa uliopo uwajue wanaJF walio karibu na wewe

Ahaa.
Siku nyingine ukipita pale usiache kuwapa hii madogo
Madogo nawaona tu wanacheza soka pale...Nakumbuka game Azania na Pugu 2007 Tuliwapiga PUGU 2-1 Ukatokea bonge la ugomvi.Sasa wakati wa kuzichapa ikawa shida kumjua yupi Azania yupi PUGU maana Uniform ndio hizo hizo aisee...

iLIKUWA MPAKA U ZOOM MUHURI
 
Hahahahaaaaa.

Ugomvi mashuleni ni mtamu sana.

Kipindi nipo O-level tuliwahi kugombana na wanakijijini kwenye mpira ilikuwa kombe la Kata lilidhaminiwa na Diwani.

Shule yetu ilipata nafasi ya kushiriki kutokana na mechi kuchezewa kwenye uwanja wetu wa shule.

Tulikuwa na timu imara sana maana kulikuwa na Wanafunzi wa Advance ambapo waliunda timu imara ya shule, tuliwavuruga kuanzia hatua ya makundi hadi fainali.

Siku ya fainali wakaamua kuipanga kwenda kuchezewa uwanja wa kijiji kingine tofauti na uwanja wetu wa shule maana tangu hatua za makundi waligundua ukorofi wa wanafunzi.

Sisi tulijihakikishia ushindi kwa asilimia zote, tukaenda kucheza tuliongozana takribani wanafunzi wote kwenda kushangilia.

Mechi ilichezwa hadi penalti japo wanakijiji walibebwa kiaina hadi hatua ya penalti.

Zikapigwa tukashinda, halafu vurugu zikaanza baina yetu na wanakijiji. Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa kwa mawe na pia tukawajeruhi na wao.

Sasa wakati wa kurudi shuleni tukaandamana barabarani, kuna daladala zikawa zinazingua kutuachia njia tukawapiga mawe viyoo vikavunjika sana.

Walimu wetu wakaja kukamatwa wakaenda kulala kituoni.

Kesho yake ilikuwa jumamosi tukagoma kula lunch na tukasema hadi walimu wetu waachiwe.

Habari zilipofika kwa kituoni walimu wakaachiwa wakaletwa hadi shuleni, wakatukuta tupo kwenye mgomo wa kutokula.

Walipofika tukashangilia sana, alikuwepo ticha mmoja tulikuwa tunampenda sana japo alikuwa anatuadhibu sana, wanafunzi walipomuona tu walifurahi sana na kumshangilia huku wakilitaja jina lake.

Baada ya hapo ndio tukaelekea jikoni kusaka menu.

Habari ya kuvunja viyoo vya daladala ilirushwa ITV siku ya tukio saa 2. usiku.
 
Naitwa Tom Chandler, captain wa meli ya Nathan James, naishi marekani. Kwa sasa niko kwenye kuandaa 'The last ship season 5'
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Hahahahaaaaa.

Ugomvi mashuleni ni mtamu sana.

Kipindi nipo O-level tuliwahi kugombana na wanakijijini kwenye mpira ilikuwa kombe la Kata lilidhaminiwa na Diwani.

Shule yetu ilipata nafasi ya kushiriki kutokana na mechi kuchezewa kwenye uwanja wetu wa shule.

Tulikuwa na timu imara sana maana kulikuwa na Wanafunzi wa Advance ambapo waliunda timu imara ya shule, tuliwavuruga kuanzia hatua ya makundi hadi fainali.

Siku ya fainali wakaamua kuipanga kwenda kuchezewa uwanja wa kijiji kingine tofauti na uwanja wetu wa shule maana tangu hatua za makundi waligundua ukorofi wa wanafunzi.

Sisi tulijihakikishia ushindi kwa asilimia zote, tukaenda kucheza tuliongozana takribani wanafunzi wote kwenda kushangilia.

Mechi ilichezwa hadi penalti japo wanakijiji walibebwa kiaina hadi hatua ya penalti.

Zikapigwa tukashinda, halafu vurugu zikaanza baina yetu na wanakijiji. Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa kwa mawe na pia tukawajeruhi na wao.

Sasa wakati wa kurudi shuleni tukaandamana barabarani, kuna daladala zikawa zinazingua kutuachia njia tukawapiga mawe viyoo vikavunjika sana.

Walimu wetu wakaja kukamatwa wakaenda kulala kituoni.

Kesho yake ilikuwa jumamosi tukagoma kula lunch na tukasema hadi walimu wetu waachiwe.

Habari zilipofika kwa kituoni walimu wakaachiwa wakaletwa hadi shuleni, wakatukuta tupo kwenye mgomo wa kutokula.

Walipofika tukashangilia sana, alikuwepo ticha mmoja tulikuwa tunampenda sana japo alikuwa anatuadhibu sana, wanafunzi walipomuona tu walifurahi sana na kumshangilia huku wakilitaja jina lake.

Baada ya hapo ndio tukaelekea jikoni kusaka menu.

Habari ya kuvunja viyoo vya daladala ilirushwa ITV siku ya tukio saa 2. usiku.
Hapo mkuu lazima mlichangishwa hela ya kulipia vioo
 
Nakaa kijiji kinaitwa NGENDE almaarufu kwa utajiri wetu ulee karibuni wote
 
Back
Top Bottom