Andika neno lolote chungu, zito, lenye maumivu ambalo hautakujaa kusahau mtu alikutamkia

Andika neno lolote chungu, zito, lenye maumivu ambalo hautakujaa kusahau mtu alikutamkia

Kuna ndugu yangu alinambia "kwa akili zako hizo fupi, hata form 4 hutofaulu" nilifaulu form 4 nilipata division one ya point 10 mtoto wake niliekuwa nae sawa akapata two ya mwisho.

Tulivoenda advance akasema tena sitofaulu, nilifaulu advance kwa division one ya point saba PCB na toto lake likapata division three.

Somo; Usimchukulie poa mtu hujui ndani yukoje.
Uyo ndo mtu bora kwako endelea kuwa nae karibu ili awe anakutabilia wrong alafu nature inafanya against
 
Habarini wapendwa.

Leo nimekaa nikawa nimepitia. Insta nikaona x kapost picha yake nikakumbuka neno mmoja mabalo nalikumbukka mpka leo liliniuma sana.

Alinisumbua sana ikafika mahali nilipewa mapumziko hospital, sasa kwenye kumpigia kumwambia nimelazwa ,bwana ee alinitext ".

Utajua mwenyewe siumeyataka mwenyewe,wivu tuu, kufatiliana fatiliana".

Asee sitasahau aalikuwa hana utu..sasa naa wewe. Andika Neno lolote CHUNGU ,ZITO,LENYE MAUMIVU AMBALO Hautakujaa kusahau mtu alikutamkia..
Sitasahau nilipokamatwa na wanajeshi walinipa adhabu na kunambia nibusu kalio langu.
 
Ni hatari sana mkuu! Kipindi namaliza form 4 nimechaguliwa kwenda chuo cha mifugo wazazi wote wakawa wamefariki nikawa sina pa kushika mpaka imefikia nakosa hata viatu vya shule. Nikasema wacha niende kwa sister mtoto wa baba mkubwa anipige tafu. Akaniambia nimfuate ofisini kwake (alikuwa dereva wa JWTZ baadaye akaja akahamia UN) ili anipeleke na home kwake nikapaone. Kufika sijui nini kikamjia kichwani akawa ameghairi kunipeleka kwake. Hapo ofisini alikuwa na wadogo zake tumbo moja na binti yake wa nje ya ndoa ambaye alikuwa karibia rika moja na yeye mzazi (alipata mimba akiwa mtoto) na kule kwa mme wake alikuwa anadanganya kwamba huyo binti ni mdogo wake (sasa nikawa nahisi kwamba labda aliogopa nisije nikamtibulia mipango). Basi akaniuliza nina shida gani? Nikamweleza naomba unisaidie hela ya viatu vya shule sina kabisa, likafuata tusi la Kisukuma "ALIYO GHASHI MAKOYE!" Wadogo zake wakacheka sana! sikurudia tena na nikaondoka zangu! Tangu siku hiyo nikakata mawasiliano nikapambana kivyangu mpaka nikamaliza chuo na kupata kazi nzuri tu kipindi hicho, yeye huku nyuma akawa ametengana na mmewe aliyekuwa anamweka mjini, maisha yakampiga mpaka akawa ananitafuta nimpige tafu, anapitishia ujumbe kwa sister wangu! Kwa vile mimi Mgalatia nikawa najibu hivyo hivyo alivyonijibu mimi! Mwisho wa siku anakuja kufariki almanusura azikwe na Halmashauri ya Jiji! Wadogo zake walionicheka kipindi kile wakaja wakafa kwa kujitia kitanzi kutokana na ugumu wa maisha uliowakumba! Karma is a bitch! Binadamu tupendane aisee!
Mgalatia 😂😂🙌🙌🙌🙌
 
Mimi mama yangu alinambiq sjitakaa nifanikiwe sitakaa niishi na watu nitateseka maisha yangu yote ila kwa sasa namjengea nyumba siku anahamia namkumbusha haya maneno

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Usiwe na roho ndogo haina haja ya kumwambia. Kama utamwambia tu utakuwa umefanikiwa kujenga ila hujaishinda roho ya kimqsikini
 
Back
Top Bottom