Andika tabia usiyoipenda ya baadhi ya member wa JF

Andika tabia usiyoipenda ya baadhi ya member wa JF

Mimi sipendi mtu anaanzisha simulizi flani kisha anaingia majukwaa mengine kutyp na wakati ile simulizi analalamika anatohoa neno kwa neno kwa mfano hadithi ya Adili na nduguze.
Ha ha haaaa , najua unanisema mimi japo sijakuelewa unazungumzia kero gani hasa. hebu fafanua nikuelewe.
 
Sipendi tabia ya watu kusimamia kitu ambacho hawajakieleza vizuri kama wewe.

Mipaka ya kusema huyu anajadili ndani ya mada, na huyu anavuruga, unaiwekaje?

Na kwa nini uone anayevuruga mada ni mtu mbaya badala ya kumchukulia kama changamoto ya wewe kuonesha ukomavu wa kifikra kwa kuweza kuendelea na mada bila "kutoka relini" hata baada ya mtu kutaka kukuvuruga?

Na kwa nini ujione una ulazima wa kumsoma mtu wakati ushaona anavuruga mada? Unajua kumblock mtu usione posts zake tena? Mimi kuna watu wengi nimewaona hawana mada za kujadili zaidi ya vurugu, ama nawachukulia kama "chuo cha ukomavu wa uvumilivu wa kitabia" ama nawa block nisione mada zao kabisa. Sijawahi kulalamikia hawa, kwa sababu teknolojia na kujielewa kwangu kiakili haviniruhusu kulalamika juu ya hawa.

Kwenye kudharau miji, kwangu hapo, kitu muhimu ni, wanachosema ni kweli au uongo?

Maana kama mji unastahili kudharauliwa, kwa ujinga fulani uliomo katika mji huo, ukisema uuheshimu mji huo na kuacha kuudharau unakuwa si tu hujitendei haki wewe mwenyewe kwa kuheshimu kitu kisichostahili heshima, bali pia unakuwa hujautendea haki mji huo kwa kuudharau mpaka ubadili ujinga huo.

Mathalan, mji una watu wanazibua vyoo na kumwaga maji ya mavi barabarani, hii ni tabia ya uchafu.

Nikisema watu wa mjii huu wana tabia ya uchafu, wenyewe wakisoma na kuona kweli huu ni uchafu, na ni ukweli, kwanza kabisa kauli yangu inakuwa si dharau, ni ukweli. Wengine wanaweza hata kusema ni kauli ya upendo. Mtu asiyejali hili hana upendo, anayejali kiasi cha kuliongelea anaweza kuwa kaongea kwa sababu hapendi kuona mji huu una uchafu.

Sasa unachoweza kuona kwamba ni dharau wewe, mwingine anaweza kukisema kwa nia safi kabisa na upendo.

Unajuaje hii ni dharau bila kuangalia ukweli uko wapi?

Mtu akikwambia ukweli mchungu ambao hupendi kuusikia, utasema kakudharau?

Mimi naona kakuheshimu sana mpaka kukuambia ukweli, angekudharau angejifanya hauoni ukweli.
Sawa wewe umeeleza hivi halafu mtu anakuqote na kukwambia thibitisha kama Mungu yupo?
Hii ni tabia ya hovyo maana swali lake halihusian na comment yako na ameuliza makusudi.
 
Sawa wewe umeeleza hivi halafu mtu anakuqote na kukwambia thibitisha kama Mungu yupo?
Hii ni tabia ya hovyo maana swali lake halihusian na comment yako na ameuliza makusudi.
Anayeniuliza mimi nithibitishe kwamba Mungu yupo atakuwa ameniingilia kazi yangu.
 
Bila ubishi kakuna maendeleo.

Tuangalie tu kama ubishi una tija au ni zogo tupu.
Ubishi mwingine ni wakipumbavu. mfano kupoteza muda kubishana kuhusu makabila ni ujinga. nimeona sehem watu wanabishana kuhusu wabena vs wasukuma eti kabila gani ni wajanja na watafutaji zaidi.
 
Tabia ya kulazimisha ligi ya ubishi uliyonayo Kiranga inakera
Inawezekana unaona Kiranga analeta ligi ya ubishi kwa kuwa huijui ligi ya ubishi.

Kiranga akikukera kukukera huko kutamkera naye pia, ni ruksa kumuweka "ignore list" usione anachoandika, usikereke na yeye asikereke.
 
Huwa sikereki bali najifunza mengi hasa kwa haters.. Kwakuwa wananifunza kuwa makini na bora zaidi.... Bila kufahamu kuwa wananishape wao hudiss, hukejeli na kutusi...
Lengo la uzi ni kuonyana, kuna tabia nyingi humu si nzuri mfano watu kuendekeza matusi. Uzi huu una lengo la kuwataka watu kuacha tabia za ajabu ajabu.
 
Ubishi mwingine ni wakipumbavu. mfano kupoteza muda kubishana kuhusu makabila ni ujinga. nimeona sehem watu wanabishana kuhusu wabena vs wasukuma eti kabila gani ni wajanja na watafutaji zaidi.
Inawezekana ulipo wewe mambo hayo hayana maana kabisa, na walipo wao mambo hayo yana maana sana.

Si lazima ukweli wako kwa elimu uliyo nayo, sehemu uliyopo etc uwe ukweli wa kila mtu kwa elimu yake na eneo alipo.

Afrika tunajitahidi kufuta nguvu za makabila, lakini ni ukweli usiopingika kwamba mila na tamaduni za makabila zina nguvu mpaka lep.

Kwa hivyo, wewe ukifikiri kivivu tu "mjadala wa makabila ni ujinga", kuna watu walipo mila na tamaduni za makabila zina nguvu sana mpaka zinafanya mtu wa kawaida wa kabila fulani awe na tabia fulani na mtu wa kawaida wa kabila jingine awe na tabia nyingine tofauti.

Wazungu wanafanya Ph.D kujua habari za makabila ya Afrika.

Kwa hiyo, pinga kwa hoja za kina. Kwa mfano, ukiongelea habari za makabila sehemu zenye watu waliojaliwa elimu na kuwa mijini kwenye mchanganyiko wa watu wengi, habari hizo zinaweza zisiwe za muhimu, lakini habari hizo hizo za makabila sehemu za vijijini, kwa watu ambao hawana elimu rasmi sana, zinaweza kuw amuhimu sana.

Kwa hiyo, kuangalia muktadha wa mjadala ni kitu muhimu.

Ndiyo maana mimi naweza kuwa si mshabiki wa dini, lakini nikimsikiliza Askofu Desmond Tutu akitumia dhana za kidini kupinga uonevu wa watu wanyonge naweza kukubaliana naye kabisa.

Au anweza kuwa sipendi kushabikia dini, lakini nawaheshimu sana Rastafarians katika counterculture yao inayotaka mtu mweusi apewe heshima na kupingana na mifumo ya serikali dhalimu.

Kwa hivyo, mambo mengine yana "layers" hutakiwi kukataa au kukubali moja kwa moja bila uchambuzi wa kina.

Ndiyo maana nikauliza, tunajiwekea viwango gani kusema huyu kaharibu mada hapa, na huyu hajaharibu mada, kaleta chachu kufanya mada iwe pana zaidi?

Kwa sababu kuna wengine tuna fikra tofauti, hatupendi kwenda kwa kukariri, tunaweza kuona mada, tukaleta hoja ambayo inaonekana inapindisha mada, kwa mtu asiyeelewa mchango.

Kumbe mchango haupindishi mada, unaipanua na kuipa kina.

Muktadha ni jambo muhimu sana.
 
Inawezekana ulipo wewe mambo hayo hayana maana kabisa, na walipo wao mambo hayo yana maana sana.

Si lazima ukweli wako kwa elimu uliyo nayo, sehemu uliyopo etc uwe ukweli wa kila mtu kwa elimu yake na eneo alipo.

Afrika tunajitahidi kufuta nguvu za makabila, lakini ni ukweli usiopingika kwamba mila na tamaduni z amakabila zina nguvu mpaka lep.

Kwa hivyo, wewe ukifikiri kivivu tu "mjadala wa makabila ni ujinga", kuna watu walipo mila na tamaduni za makabila zina nguvu sana mpaka zinafanya mtu wa kawaida wa kabila fulani awe na tabia fulani na mtu wa kawaida wa kabila jingine awe na tabia nyingine tofauti.

Kwa hiyo, pinga kwa hoja za kina. Kwa mfano, ukiongelea habari za makabila sehemu zenye watu waliojaliwa elimu na kuwa mijini kwenye mchanganyiko wa watu wengi, habari hizo zinaweza zisiwe za muhimu, lakini habari hizo hizo za makabila sehemu za vijijini, kwa watu ambao hawana elimu rasmi sana, zinaweza kuw amuhimu sana.

Kwa hiyo, kuangalia muktadha wa mjadala ni kitu muhimu.

Ndiyo maana mimi naweza kuwa si mshabiki wa dini, lakini nikimsikiliza Askofu Desmond Tutu akitumia dhana za kidini kupinga uonevu wa watu wanyonge naweza kukubaliana naye kabisa.

Au anweza kuwa sipendi kushabikia dini, lakini nawaheshimu sana Rastafarians katika counterculture yao inayotaka mtu mweusi apewe heshima.

Muktadha ni jambo muhimu sana.
@Kiranga naona unajichanganya. mada inazungumzia tabia za humu jamvini. kwa hiyo ubishi wa kimakabila kama una maana sehem fulani basi kwa humu jamvini huo mjadala hauna maana kwa kuwa hum mmejaa wasomi na watu wa makabila tofautu tofauti.
 
Si kweli.

JF ina watu wa kila aina wenye mawazo tofauti. Inapatikana sehemu tofauti, na watu wenye elimu na uchumi tofauti.

Ndiyo maana wengine wanakera wengine.

Wote tungekuwa wasomi na tuna mawazo sawa, hakuna mtu ambaye angemkera mwingine.

Unayejichanganya ni wewe.
 
Back
Top Bottom