Andiko la Mwisho la Ole Mushi;Ukoloni unarudi Tanzania

Huwa nawaambiaga watu ukijifanya wewe ni shujaa wa kalamu iko siku tu watakufuta na ukabaki historia
 
Andiko la mwisho la Ole Mushi hebu lipitie👇🏿

....Vijana tuliopo ndani ya CCM ni wakati wa kujitafuta sasa tuache kusifia ujinga wakati taifa limekwama. Tuzungumze, tukatae kabisa kuwa Chawa wa mtu, wakati ni sasa….. kila mtu kwenye familia yake atoe elimu ya Uraia.

Tumekwama kama Taifa….. share

Ole Mushi
0712702602
Hii aya bdo ikawa exit door ya ndugu yetu.

Kuna kijana anaitwa Lucas mwashambwa tangu Ole Mushi awe confirmed anaugua, amekuwa anajitahidi sana kupambania pengo lililokuwa linaenda kuachwa wazi na kijana Mushi. Sijawahi kumsoma akimtaja kada mwenzake zaidi ya kusifia upuuzi wa watawala.

Nchi imeharibiwa na CCM mbele yetu. Tunashangilia chama kama mazuzu vile.

Tufike mahala tukatae kuwa manamba wa CCM, tuisaidie nchi
 
Kuandika na kuongea na kusimulia vya wengine ndio Tanzania tunaweza akiwepo huyo bwana Mushi.

Niliyegemea aoneshe mfano wa juhudi alizofanya kwenye kuwezesha hayo anaholaumu badala yake anadhani Kuna Mtanzania somewhere wa kufanya hivyo ila sio yeye.

Watanzania tuhame kutoka kwenye hadithi na masimulizi tuende kutenda then kwenye kutenda ndio tuwe tunawasema wale wanaotukwamisha badala ya kuviziana.
Hivi unayeandika unajitambua. Yeye ameandika mawazo yake akimaanisha lahiti kama angepewa nafasi ya hao viongozi hivyo ndivyo vingekuwa vipaumbele na strategies zake. Kwa sasa yeye kama yeye hawezi kwa sababu vitu vingi ni wajibu wa serikali na yeye yuko nje ya serikali
 
Upuuzi, kwani kufanya aliyosema Hadi awe Kiongozi? Uongozi unapiganiws sio kupewa.Apewe kama nani?
 
Andiko la mwisho la Ole Mushi hebu lipitie👇🏿

UKOLONI UNARUDI TANZANIA?

Na Thadei Ole Mushi.

Miaka 60 ya Uhuru tumeshindwa kabisa kusimamia rasilimali zetu wenyewe.

Migodi tumeitoa kwa Wazungu, Misitu tumeitoa kwa Mwarabu, Posta tumeitoa kwa Mwarabu, Misitu tumeitoa kwa mwarabu, Gesi tumeitoa kwa Mzungu, Uwanja wa ndege wa KIA nao tumeutoa, TPDC tumeitoa, Bandari tumeitoa kwa mwarabu, Loliondo tumeitoa kwa Mwarabu, karibi maeneo yote Muhimu tumeshatoa…. Sisi tumebakia na nini?

Maswali ni Mengi mno….

1. Tulidai Uhuru wa Nini?

2. CCM imeshindwa kuiongoza Nchi? Maana kila eneo tuliloliwekeza tunasema kuna wapigaji hivyo bora tumpe mwekezaji. Je Serikali ni dhaifu imeshindwa kuzuia upigaji?

3. Vyuo Vikuu zaidi ya 31 nchini vimeshindwa kutengeneza wasomi wa kusimamia hizi rasilimali za taifa? Kazi za Graduate wetu kubwa ni kuendesha Bodaboda, kama taifa tunajua tunakoelekea?

4. Tanzania tunaweza jambo gani kubwa hapa nchini? Mambo yote ya muhimu tunaona ni Magumu tunawapa wawekezaji je sisi ni kitu gani tunaweza? Wenzetu wanawezaje sisi tunashindwa? Huu uvivu wa kufikiri tumeutoa wapi?

5. Baada ya Bandari tunaenda kuwekeza rasilimali gani tena? Ukiona wabunge wetu wanavyovaa Suti Pale Bungeni na taifa linapoelekea utatamani kulia. Hawa watu (wabunge) tunawalipa mishahara, tunawanunulia mafuta ya magari, watoto wao tunawasomesha na bado wanatuibia kupitia mikataba hivi nani alituloga tukawa waoga hivi?

6. Tanzania ya watu Milioni 69 plus tumeshindwa kuchaguana miongoni mwetu tupate watu wanaoweza kutuvusha hapa tulipo kwa kuwa taifa linaelekea kutawaliwa kwa mara ya Pili?

7. Wakati Uganda ilipogundua kuwa ni kweli Taifa lao lina mafuta walichukua vijana wao wakakimbiziwa ughaibuni kwenda kujifunza kuhusu Oil Production na asilimia kubwa ya mradi wao wa mafuta ni vijana wanausimamia. Sisi badala ya kuandaa vijana tunatuma kina Steve Nyerere na kina Kitenge kwenda kukagua Bandari za wenzetu hivi nani alituloga?

8. Vijana asilimia 90 sasa hivi hapa nchini bila kujali elimu zao kazi zao kubwa za kujipatia kipato ni Kubet au kuendesha Bodaboda. Huku maeneo muhimu ya rasilimali za taifa lao zikigawanywa kwa wazungu na waarabu kwa jina la kusema ni mwekezaji. Hii ni hatari sana kwa taifa letu…. Tanzania ina wanyamapori kila mahali ila anayekula nyama pori first class kabisa hapa Tanzania ni Mwarabu hii ni aibu…

9. Je tuliwahi kupata Uhuru? Lakini mbona Kina Singapore walipata Uhuru nyuma yetu? Mbona leo ipo mbali sana na wanajisimamia wenyewe?

10. Hata kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha kwa taifa zima tumeshindwa tunaagiza nje ya nchi, Ngano tunaagiza, Mbolea tunaagiza, Maziwa ya Unga na hata ya kawaidia tunaagiza, pale Bandarini asilimia 95 ni bidhaa zinaingia nchini badala ya kutoka hivi tunaelekea wapi?

CCM ikubali sasa kutumia watu ambao wapo nje ya familia zenye Connection kwenye Uongozi wa nchi hii. Babu alikuwa kiongozi, mtoto akatafutiwa connection akawa kiongozi, mjukuu naye akawa kiongozi nk …. Hizi DNA kwa mazingira ya Sasa zimechoka au CCM ikubali kuwaachia wengine wajaribu kutusogeza tulipo.

Kuna siku nilisema kama Africa itaheshimu Sanduku la Kura katika kuchaguana tutafika mbali sana. Na kama askari polisi wa Mataifa ya Africa watatimiza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria hili bara linapiga hatua kubwa. Askari anamlinda mtu mwenye V8, Mke ana gari, watoto wa huyo Mtu wanachukuliwa na School Bus wanakupita getini unawachekelea kama Zuzu, huku kwako ukiwa unafukuzana na Baba Mwenye nyumba anakudai kodi, kijana wako wa kwanza aliyehitimu Chuo kikuu anashinda vibanda umiza anabet, wanao wanasoma shule za makabwela kabisa huku akiwa hana uniform za kubadilisha lakini bado unaendelea kupiga Salute kwenye mageti ya viongozi.

Vijana kwa Rasilimali zilizopo hapa nchini hampaswi kukesha mkiwa mna Bet na kuendesha Boda boda. Wafanyakazi kwa rasilimali zilizopo Hampaswi kulipwa mishahara mnayolipwa. Hivyo basi watu kama kina Steve Nyerere na kina Maulid Kitenge ni wa kuwatenga kwenye jamii yetu…. Tunatakiwa tuanze kutokomeza hizi chawa kwanza kabla hatujawafikia Viongozi wetu.

Wakati ukoloni ukibisha Hodi Africa ulikuja kwa njia ya Mikataba. Ndiko tunakoelekea…..

Vijana tuliopo ndani ya CCM ni wakati wa kujitafuta sasa tuache kusifia ujinga wakati taifa limekwama. Tuzungumze, tukatae kabisa kuwa Chawa wa mtu, wakati ni sasa….. kila mtu kwenye familia yake atoe elimu ya Uraia.

Tumekwama kama Taifa….. share

Ole Mushi
0712702602
Ukoloni haupo
 
Sasa mbona yule Gilbert A Massawe alisema Ole Mushi alikuwa akiitetea DP world na mama Samia?

Naanza kuhisi tuhuma dhidi yake ni za kweli.

Mafioso anakuuwa baada ya kujisogeza karibu yako akijidai ni rafiki yako wa hali na mali.

May his soul rest in peace.
 
Daaah andiko lenye hisia Kali lenye ukweli mchunguu!!
Hakika Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana na himidiwe!!

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Kwa Andiko hili he couldn't be safe anymore

Graduate kuendesha bodaboda honestly it hell

Nothing to say but see you again Thadei ole Mushi.
 
Back
Top Bottom